Uandishi gani huu?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
Gazeti la Mwananchi la leo (19/9/12) limeandika cuf na v4c, chadema na m4c... Likaendelea kuwa ...chadema kinachoendesha operesheni mbalimbali za kujijenga nchi nzima ikiwamo movement for change (m4c), cuf kimeibuka na mchakamchaka wa dira ya mabadiliko (v4c)...

Ugomvi wangu uko hapo. Hii v4c kirefu chake nini? Kwa kuwa nimesoma kidogo nimetafakari nikasema inaweza kuwa ni 'vision for change'. Katika makala nzima sijaona hayo maneno hapo juu yameandikwa hivyo. Nani ataelewa kuwa hiyo v4c ndio vision au kitu kingine? Mbona m4c imewekwa sawa? Uandishi gani huu? Niko wazi kukosolewa.
 
hayo uliyosema mwana ni sahihi katika gazeti linalosomwa na watu wengi huwezi kuandika hivyo hata kidogo
kule mwanalumango wataelewaje wakisoma hiyo habari enyi waandishi wa habari angalieni lugha mnazotumia katika kuandika habari zenu kwani wakati mwingine mnapotosha jamii jamani habari adadu zenu katika uandishi
 
Hili gazeti linaelekea kuwa km la udaku, hata habari ya mke wa kigogo wa polisi kutapeli inavoandikwa ni 'kimagumashi' tu, mara jina la kigogo limehifadhiwa hata la mke wake pia! Shiiit! km mnazuiwa kuandika acheni sio mnakuwa km magazeti ya she-gongo.
 
Hope watarekebisha. Pia katika hiyo habari ya mke wa kigogo nimejiuliza kwa nini wafiche majina ya mke wa kigogo na mwanae kisha waanike jina la Baraka wa ikulu?
 
Back
Top Bottom