Uandikishaji vitambulisho vya uraia unakwenda mrama

Zomba, mimi nashangaa sana tunachotaka ni nini? Au ndio mambo yale yale...ukiweza kumsumbua sana mtu ndio unakuwa mfanyakazi bora! Muda wa kufuatilia hayo yote uko wapi?
Ndahani unanikumbusha kisa cha Mzee muuza nyanya sokoni;

Kapanga fungu zake 30 za nyanya kaja mteja kauliza "fungu shillingi ngapi?" akajibiwa ""elfu moja" akamwambia "haya nitilie kwenye kikapu zote hizo", Mzee muuza nyanya akamjibu "siuzi zote, ukitaka chukuwa fungu tano tu", mnunuzi akauliza "kwa nini?" akamjibu, "mimi nimeaga nyumbani nakwenda kazini, wewe ukichukuwa zote hizi, muda wote uliobaki ntakaa nifanye nini?".

Hiyo ndio typical Tanzania, kama hujatoka jasho hujafanya kazi.
 
Wahamiaji haramu wajiandikisha vitambulisho vya taifa
Saturday, 28 July 2012 09:29
digg

Elizabeth Edward
Mwananchi

IMEBAINIKA kuwa baadhi ya wahamiaji haramu wamejiandikisha na kujaza fomu za maombi ya vitambulisho vya uraia.(Dah!)

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia kwenye kituo kimoja Mtaa wa Ali Hassan Mwinyi, eneo la Mikocheni A, wakiwa wamejitokeza kujaza fomu hizo bila vithibitisho halali vinavyowaruhusu kuishi nchini.

Hata hivyo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) ilisema wahamiaji wasiokuwa na vibali vya kuishi nchini, hati ya kusafiria au cheti cha ukimbizi hawatatambulika na kuhusishwa katika zoezi hilo na kubainisha kuwa, kwa wageni kuishi nchini bila vitu hivyo ni kinyume cha sheria.

Ofisa Habari wa Nida, Thomas William alisema iwapo itabainika kuna wahamiaji haramu wamefanikiwa kujiandikisha katika hatua za awali, mamlaka hiyo itashirikiana na Idara ya Uhamiaji kuwawajibisha.

"Kama kuna wahamiaji haramu ambao hawana vibali wala hati za kusafiria, lazima tutawabaini na kuhakikisha tunawafikisha ngazi husika kwani mchakato bado ni mrefu tutawapata tu," alisema William.

Aliongeza kuwa Mamlaka hiyo imeweka kamati ya ulinzi na Usalama katika kila kata ili kuhakikisha hakuna udanganyifu utakaofanyika kwa lengo la kupotosha zoezi hilo.

Katika hatua nyingine William alisisitiza kuwa zoezi hilo litawahusisha watanzania walio nje ya nchi ingawa alibainisha kuwa Mamlaka haijatoa muda rasmi wa wao kurudi nchini ili kujisajili.

"Hata wale walioko nje ya nchi wanapaswa kurudi kujiandikisha na kupata vitambulisho hivi, lakini ingawa mamlaka haijasema warudi sasa kwa kuwa zoezi hili litakuwa endelevu ila kujiandikisha ni lazima kwa Watanzania wote," alisema William.

Pia, aliwatahadharisha Watanzania kutotoa fedha kuandikishwa au kujaza fomu hizo, kwani zoezi hilo linaratibiwa na Serikali.

"Zoezi hili halipaswi kulipiwa na mamlaka imepata taarifa za baadhi wa watendaji wa Serikali kudai fedha kwa ajili ya kuandika barua za utambulisho kwa wakazi wa maeneo yao," alisema

Alitaja maeneo ambayo watendaji wake wamekamatwa kwa tuhuma hizo kuwa, ni Bunju, Mabwepande na Yombo Vituka.

Aliwataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika vituo wakiwa na vitambulisho vyao kushiriki zoezi hilo ambalo litakamilika rasmi Julai 30, mwaka huu.

 
BAK, Hii yote ni trela cinema yenyewe haijaanza. Yaani mpaka huu hili zoezi liishe tutaona na kusikia mengi. Nchi imesubiri mpaka tunafikisha karibia miaka 50 tangu uhuru na takriban watu Mil. 50 kuanzisha hili zoezi, basi tegemea madudu matupu. Wakimbizi na wageni kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na kati waamekaa mkao wa kula, huku wakisubiri utaifa wa bure kutoka Tanzania. WanaITUMIA vizuri ile methali ya kiswahili: "PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA."
 
Every "possible" is "impossible" in Tanzania, and vice versa.
Suala la IDs lilipaswa liwe suala endelevu, sio unaweka mwisho tarehe 30 Julai. Kama ni kutoa muda basi ingehitajika miezi sita hadi mwaka. Sasa baada ya hiyo tarehe 30, kama kuna WaTZ wngi hawajajiandikisha itakuwaje, watafukuzwa nchini kwa kuwa hawana vitambulisho na kwa hivyo sio raia?

Jengine, kwa kuwa suala la vitambulisho linahusiana na urai na uhamiaji, kwa nini kuliundia Mamlaka yake wakati Ofisi za Uhamiaji zingetosha kutekeleza shughuli hizi, pale inapohitajika vijijini wangetumia "mobile services".
 
Kweli kabisa ujazaji fomu kwa ajili ya vitambulisho una mambo.

Nilipowasiliana na Afisa Mtendaji wangu wa Mtaa ili anipatie maelezo taarifa gani zinahitajika katika kaya yangu ili nimtayarishie ahead of time ili atakapotembelea aje tu ku-verify wanakaya wangu, alikataa kata kata na kunidhihaki kwa nini nataka ninunue nepi kabla mtoto hajapatikana? Nikwamwambia kama akija mie sipo huenda akapata taabu kupata baadhi ya taarifa. Lakini wapi hakunisikiliza. Alipokuja nyumbani kwangu mimi sikuwepo. Kama nilivyohofu hakuweza kupata taarifa kamili. Mie nikaenda kwa ten cell leader kumuuliza kama kuna taarifa za ziada anazohitaji. Nakampatie. Lakini nikambana zaidi na kutaka kujua kama hakuna taarifa nyingine anazohitaji. Akasema hakuna. Siku ya pili akanifuata kutaka taarifa zaidi!

Wakati wa kujaza Form 1A, mimi nili-download hizo fomu kutoka kwenye tovuti ya NIDA. Nikajaza details zote za wanakaya wangu. Nikazipeleka kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wangu. Lakini Afisa yule akashangaa sana. Akaniuliza nimezipata wapi zile fomu? Mie nikwambia kwani tatizo nini? Kwa shingo upande akazichukua na kukubali mie nijaze fomu zake tena na na kuwata wanakaya wangu wazisaini pale ofisini kwake. Nilivyomuuliza mimi kama mstaafu nisemeje katika item ya employment: nimeajiriwa au nimejiajiri au sina kazi. Yeye akasema niji-list kama sina kazi. Lakini nikamuuliza unawezaje kusema mtu ambaye amepita age ya kufanya kazi na amestaafu na hawajibiki kufanya kaz na ukaendelea kum-list kama hana kazi? Na hata akifanya kazi ni part-time tu. Afisa aka-insist kwamba lazima niseme sina kazi! Makubwa!


Kwamba hakuna maelekezo yanayofanana kama watu wawasilishe kielelezo kimoja kinatosha au vingi iwezekanavyo ni dalili NIDA hwakujiandaa vizuri. Kuwa na vielezo vingi iwezekanavyo kuna-provide better proof ya ukweli wa vielezo hasa ikiwa majina yanafanana. Na kukataa kupokea online submissions ya fomu ya NIDA 1A hakutasidia zoezi hili. Wakati watu million tano hapa Tanzania wanasemakana wana-access to the Internet! Mbinu zingewezwa kutafutwa za kutumia njia hii. Kilinoniacha hoi zaidi ni pale one senior NIDA official aliposema on television leo asubuhi kwa Watanzania waishio nje ya nchi itabidi waje nchini kujiandikisha! Kwa nini wasisubiri wakati wajapo likizo wajiandikishe? Na kama NIDA hawapo tayari si watasubiri tu next time?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
@ Mavunja. Umeeleza vizuri hata mimi ktk kipengere cha Umejiajiri,Umeajiriwa,Sina kazi,sijui kwa nini hawakuongeza Mstaafu,Mwanafunzi/Mwanachuo!
 
@ Mavunja. Umeeleza
vizuri hata mimi ktk kipengere cha Umejiajiri,Umeajiriwa,Sina kazi,sijui
kwa nini hawakuongeza Mstaafu,Mwanafunzi/Mwanachuo!

hii ni mara ya kwanza. wanajifunza as they go along. ila hilo swala la picha ni a big omission. wangesema basi hata watu waje na picha.
 
Hivi wasingeweza kuanza na taarifa za uhamiaji kwa wenye passport, za TRA kwa wenye leseni za udereva, n.k?
 
Ni mambo ya hovyo kusema kweli. Tuna balozi zetu katika nchi nyingi nchi za nje ambazo zinaweza kabisa kutumika kukamilisha zoezi hili kwa Watanzania waishio nje lakini naona hili la kutumia balozi zetu halipo katika mipango yao.


"Hata wale walioko nje ya nchi wanapaswa kurudi kujiandikisha na kupata vitambulisho hivi, lakini ingawa mamlaka haijasema warudi sasa kwa kuwa zoezi hili litakuwa endelevu ila kujiandikisha ni lazima kwa Watanzania wote," alisema ofisa habari wa NIDA, Thomas William.
 
Hata hivyo hawa NIDA, Hawajui watatoa vitambulisho kwa watu wangapi,Fikiri kwanini wasingesubiri zoezi la sensa ambalo litafanyika karibuni ili kuwa na takwimu sahihi,ya watakaotakiwa kupatiwa vitambulisho.
 
Kwa nini wasitumie sensa kama fursa pia ya kuandikisha vitambulisho? Vilevile wangeweza kuandikisha kwa kutumia wajumbe wa nyumba kumi mkumi. Huko pia ndipo wangepata taarifa sahihi zaidi za wanamchi.

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
Mkuu NATA ni vitu vya kustaajabisha sana. Wanakurupuka katika kila jambo matokeo yake ni kujikanyakanyaga kwa hali ya juu. Wametumia zaidi ya shilingi bilioni 300 lakini angalia zoezi lenyewe jinsi lilivyo shaghala baghala. Halafu wakiitwa DHAIFU wananalama.[/QU
huu mradi ulianzishwa ili watu wapige 10% ..otherwise preparations za zoezi zima ni uozo mtupu nimeamua hata nisijiandikishe LIWALO NA LIWE
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nadhani Watanzania wengi baada ya kupata usumbufu mkubwa katika kukamilisha zoezi hili baadhi watakuunga mkono na kuamua kutoshiriki...LIWALO NA LIWE.

huu mradi ulianzishwa ili watu wapige 10% ..otherwise preparations za zoezi zima ni uozo mtupu nimeamua hata nisijiandikishe LIWALO NA LIWE
 
zomba,

Kwa Mara ya kwanza naona umeamua kutumia akili yako kufikiria positively! Hongera.

My take is very simple, si unajua project ya National Identity has been around na sheria ilipitiswa almost a quarter of century ago. Sasa the govt of all those years under ccm wangekuwa makini ingefanyika Kabla hata fisadi Mkapa hajaingia madarakani . Over those years Mawaziri wa Mambo ya ndani wamekuwa wakibadilishana kati ya Bara na Visiwani.

Ni katika awamu hii ya JK ndipo akina Masha walionyesha nia ya kufufua hiyo project , of course imekumbwa na kashfa za rushwa nyingi najua wewe unazifahamu.

The problem of NIDA lies in the wrong choice of Maimu who is corrupt kuwa CEO wa NIDA the study and project design are all wrong, just like having a new Bus with the wrong driver apparently heading in the opposite direction.

Maimu is the wrong diver going to Arusha but heading towards Mkuranga. Eti badala ya kufanya pilot sehemu ngumu kama Manzese, Keko slums or Unga limited slams in Arusha anafanya usanii na kuanza na wafanyakazi wa Serikali na Jeshini where wengi wao wana ID za kazi na ni walipa kodi PAYE pia kumbukumbu zao for raw data are available with their employers.

Hutarajii mafanikio hapa simply the means justify the end. Expect more troubles to come. Mtu anayo passport zote mpya finger prints mnazo just ask them to provide more bio data! Kuanza kuwaandikisha is waste of time...
 
Mkandara hayo usemayo sawa kabisa lakini tazama hapa kwetu, kwanza wanapita nyumbani kuchukuwa basic information, halafu unaenda kwa mtendaji kuandikisha information hizohizo, halafu unaondoka huambiwi hatua inayofuata lini au picha utapigwa lini? au kirahakisha kama ni mtu wa kusafiri safiri ufanye nini. Yaani mpango ndio huo na wanasema ukichelewa ungoje miezi 6, sasa hapo kuna kuchelewa au kucheleweshwa?

Hapo sasa, kwa wenzetu huko mlipo nadhani utajuwa kimoja kimoja unachotakiwa kufanya, kinachotakiwa na kinachofuata ni lini. Hapa kwetu hatua hiyo hiyo mara mbili kujiandikisha tu na hujamaliza na hujui hatua ya tatu inakuwa nini au lini.

Mfano ukienda kwenye website ya NIDA utakuta sample ya form ya kujiandikisha imeandikwa "FOMU HII IJAZWE NA RAIA WA TANZANIA KWA WINO MWEUSI" lakini cha kushangaza ukienda kujiandikisha ukiuliza fomu unaambiwa haziruhusiwi kutolewa na inabidi usubiri ujaziwe na afisa wa NIDA, sasa kwa nini wasiseme kwenye fomu kuwa "FOMU HII ITAJAZWA NA OFISA WA NIDA KWA NIABA YA RAIA WA TANZANIA"?

Ni ukiritimba wa kijinga jinga tu. Wangeacha wanaojuwa kuandika wajaze wenyewe kama fomu zinavyojieleza.
Nakubaliana na wewe sana tu na lazima tukubali kwamba sidhani kana kuna njia rahisi hasa kwa nchi ambayo ndio kwanza tunaanza kitu hiki...

Wenzetu swala hili linaanza toka mtoto anapozaliwa, report ya Hospital inakwenda moja kwa moja Immigration pamoja na kwamba mzazi anapewa birth certicate. Mtoto tayari anatambulika kama raia, na kila form inayofuata unaijaza wewe mwenyewe nyumbani na kuituma ukielekezwa kila hatua (kunakuwepo guideline). Kama hujui unajaziwa na mtu anayejua halafu saini unaiweka wewe..Na hata wao bado watu wanafanya makosa na applications zinarudi..

Binafsi yangu kaa unakumbuka niliwahi kusema TIN namba ndizo zingeanza kwanza kabla ya vitambulisho vya Uraia. Hizi zingeweza kutengeanisha kwanza makundi ya watu. Wale wazawa, wahamiaji na kisha wale wanaoihi kwa vibali na work permit..Ukisha hakikisha kila mtu amepata TIN namba ambayo ni muhimu zaidi ktk ukusanyaji wa kodi ndipo serikali kwa kutumia hizo Tin namba inawatumia form wananchi wote waliojitambulisha kaa raia at the same time watoto wanaozaliwa wanakuwa covered na mfumo mpya unaowatambua baada tu ya kuzzaliwa.

Hii ingerahisisha kazi ya vitambulisho vya uraia na pengine hata isingekuwa muhimu maana Huku majuu Wazawa hawana vitambulisho ila wanatumia tu Social security namba na cheti cha kuzaliwa. Hivyo pengine serikali kuanza na vitambulisho vya uraia wana sababu zao japokuwa kusema kweli hakina umuhimu mkubwa kuliko TIN namba...

Kuwa na kitambulisho cha uraia haimsaidii mtu lolote wala serikali zaidi ya kuanza tena ule mpango wa kusimamisha watu a kuwaomba kitambulisho cha Uraia kutokanana kwamba wageni wamevamia nchini na kuleta madhara ktk uchumi wa nchi, hivyo tunatafuta njia za kuwafukuza au kuwarudisha makwao..Na naposikia matatizo kama haya inanipa picha kwamba hatukujianda kabisa na kitu hiki pengine hatukwenda hata kujifunza nchi za wenzetu wameweza vipi...
 
hii ni mara ya kwanza. wanajifunza as they go along. ila hilo swala la picha ni a big omission. wangesema basi hata watu waje na picha.

Kwa Mbezi beach watu waliokua hawana vitambulisho/vyeti vya kuwatambulisha walikua wanaambiwa wapeleke picha nadhani na barua toka serikali ya mtaa! Najiuliza watu wenye TIN namba ktk mfumo mpya wa TRA, Passport, Driving Licence mpya na Vitambulisho vya kupiga kura sitayari picha zao zipo ktk system?
 
Nakubaliana na wewe sana tu na lazima tukubali kwamba sidhani kana kuna njia rahisi hasa kwa nchi ambayo ndio kwanza tunaanza kitu hiki...

Wenzetu swala hili linaanza toka mtoto anapozaliwa, report ya Hospital inakwenda moja kwa moja Immigration pamoja na kwamba mzazi anapewa birth certicate. Mtoto tayari anatambulika kama raia, na kila form inayofuata unaijaza wewe mwenyewe nyumbani na kuituma ukielekezwa kila hatua (kunakuwepo guideline). Kama hujui unajaziwa na mtu anayejua halafu saini unaiweka wewe..Na hata wao bado watu wanafanya makosa na applications zinarudi..

Binafsi yangu kaa unakumbuka niliwahi kusema TIN namba ndizo zingeanza kwanza kabla ya vitambulisho vya Uraia. Hizi zingeweza kutengeanisha kwanza makundi ya watu. Wale wazawa, wahamiaji na kisha wale wanaoihi kwa vibali na work permit..Ukisha hakikisha kila mtu amepata TIN namba ambayo ni muhimu zaidi ktk ukusanyaji wa kodi ndipo serikali kwa kutumia hizo Tin namba inawatumia form wananchi wote waliojitambulisha kaa raia at the same time watoto wanaozaliwa wanakuwa covered na mfumo mpya unaowatambua baada tu ya kuzzaliwa.

Hii ingerahisisha kazi ya vitambulisho vya uraia na pengine hata isingekuwa muhimu maana Huku majuu Wazawa hawana vitambulisho ila wanatumia tu Social security namba na cheti cha kuzaliwa. Hivyo pengine serikali kuanza na vitambulisho vya uraia wana sababu zao japokuwa kusema kweli hakina umuhimu mkubwa kuliko TIN namba...

Kuwa na kitambulisho cha uraia haimsaidii mtu lolote wala serikali zaidi ya kuanza tena ule mpango wa kusimamisha watu a kuwaomba kitambulisho cha Uraia kutokanana kwamba wageni wamevamia nchini na kuleta madhara ktk uchumi wa nchi, hivyo tunatafuta njia za kuwafukuza au kuwarudisha makwao..Na naposikia matatizo kama haya inanipa picha kwamba hatukujianda kabisa na kitu hiki pengine hatukwenda hata kujifunza nchi za wenzetu wameweza vipi...

Si unaona, kwetu huku mtoto haandikishwi mpaka afike miaka 18. Sasa sijui hii dhanna ya kuwa raia ni mtu mzima tu waliitowa wapi. Mie nakwambia hii mijitu iliyowekwa kuendesha idara au taasisi nyeti kama hizi haifai hata kidogo.

Halafu sasa uwaulize kwanini hivi na hivi, wataanza kuleta porojo ndefu mpaka utawaona kuwa hawa ndio watu wanaojuwa duniani.

Kwa kifupi mfumo mzima wa kuandikisha Uraia ni ukiritimba wa hali ya juu. Nna uhakika kuna namna mbadala rahisi kabisa na bila manung'uniko zingefanyika na zingekuwa zinaendelea bila matatizo ya ziada, matatizo yangekuwepo yale ya kawaida ya makosa madogo madogo yanayotatulika.

Kilio changu kikubwa ni muda unaopotezwa kwa kufanya mambo kuwa complicated bila sababu, jamani muda ni mali.
 
Kwa kweli kuna ukiritimba sana mtu unakwenda na passport bado tena unaanza kuulizwa maswali ya uraia mara umezaliwa wapi sijui lini tena tutaitwa kupigwa picha.
 
ama hakika kwanza nina hasira sana na hao makarani wa nida ambao walipata iyo kaz just because wazee wao na jamaa ni wajumbe wa nyumba kumi. hawa jamaa wanaandika utafikir wanatumia vidole vya miguu aisee! fikiria mtu mmoja anakuwa saved kwa zaid ya nusu saa na kuna folen ambyo kila siku inaongeza, unadhan ni nini kama si kuupoteza muda wetu bure kwa uzembe wa kufikiri wa hao viongoz wa nida?
 
Wamekurupuka na hivyo hili la kutumia data ambazo zimeshakusanywa na taasisi nyingine nchini halikuwamo katika mipango yao.

Kwa Mbezi beach watu waliokua hawana vitambulisho/vyeti vya kuwatambulisha walikua wanaambiwa wapeleke picha nadhani na barua toka serikali ya mtaa! Najiuliza watu wenye TIN namba ktk mfumo mpya wa TRA, Passport, Driving Licence mpya na Vitambulisho vya kupiga kura sitayari picha zao zipo ktk system?
 
Back
Top Bottom