Uamuzi wa Kuingia Chama Kimoja: Maelezo ya Kleruu na Nyerere

Je, leo hii katika vyama vingi tuna umoja wa kupigana vita ya kuwa hai? Unafikiri vyama vingi vimejenga umoja wa Watanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za ujenzi wa taifa kuliko ilivyokuwa wakati wa chama kimoja? Kwa maneno mengine, je Watanzania ni wamoja zaidi sasa hivi kuliko wakati wa chama kimoja?

Ni kuturudisha nyuma nusu karme mtu kushupaza mishipa kichwani kujadili maisha ya mwaka 1960 kwa kizazi cha leo, kwani utabaki kuumia nyongo wakati mtazamo, fikra na mazingira ya leo na ya miaka ile inatofautiana mno. Kwa wakati ule kufikiri na kufanya kama walivyofanya ilikubalika na hakikuwa kitu cha kushangaza tofauti na kizazi cha leo.

Wapembuzi yakinifu wanachofanya ni kusoma yale yaliyofanyika wakati ule, kuyachuja na kuchukua yale ambayo katika kizazi cha leo yana nafasi. Kuendelea sijui kumjadili Nyerere, Kleruu na wengine na kuchukulia hoja kwamba wao ndio waliosababisha matatizo tuliyo nayo leo ni fikra finyu sana. Ndio maana nchi ye yote ile ina baraza la wawakilishi kama sisi tulivyo na bunge ambalo hupitia miswada mbalimbali mipya na kuibadilisha au kuongeza vipengere vipya kutokana na mabadiliko ya wakati kuendana na kizazi cha muda tulio nao. Tungekuwa na mfumo dume kama mawe yasiyobadilika na kubaki kama yalivyo hatungehitaji bunge liwepo muda wote. Nadhani mmenielewa.

Tunahitaji kujadili mambo yetu ya wakati huu wa sasa yanavyoenda na kizazi cha leo tunataka nini, na tunaweza bado kudonoa mazuri ya wakati uliopita ambayo bado yana mshiko, hayajachuja, kinyume cha hapo ni sawa na kumshambulia babako kwa nini alikuzoesha kunywa mbege ulipokuwa mdogo badala ya soda au bia ambayo unaoina inakufaa sasa wakati nafasi na uwezo unakuruhusu, tatizo hapo hupimi nafasi na uwezo wa baba alipokuwa anaishi bado kijijini, una unakuwa na mtazamo wa leo unapoishi mjini na hata vijijini ambako leo wanaweza kutumia simu za mkononi hata wanapochunga mbuzi.
 
kama unalosema ni kweli kwanini tusiuimarishe huu mfumo wa chama kimoja kwa kufuata misingi iliyomo katika hiyo hotuba ya Nyerere? Mapendekezo yaliyotolewa na tume ya kupitisha mfumo wa chama kimoja ni kwa kiasi gani yalifuatwa na kuzingatiwa? Je tuyaangalie tena na kuona jinsi ya kuboresha huu mfumo wa chama kimoja?

misingi look good on paper just like how communism does. Lakini waweza kunitajia nchi yenye mfumo wa chama kimoja pamoja na demokrasia na uhuru wa watu wake. Kama sijakosea Nyerere mwenyewe alituwekea marais wawili...mwinyi na mkapa. Ndio demokrasia ya chama kimoja hiyo?
 
Duh.. sasa sijatetea demokrasia ya chama kimoja - japo naweza. Hoja zangu zinaweza kulingana kabisa na zile za Kleruu. Tatizo ni kuwa watu wa Magharibi wametuambia demokrasia ni ya vyama vingi na sisi bila kuhoji tumeamini kuwa ndivyo ilivyo. Kwanini tunahusisha demokrasia na uwepo wa vyama vingi? Je kuwa na vyama vingi ndio kuwa na demokrasia? lakini vile vile tumeaminishwa kuwa demokrasia ya vyama vingi ni muhimu kwa maendeleo - kitu ambacho China na Vietnam zinaonesha kuwa si kweli. Na nina uhakika hata mabadiliko aliyoyaanza Castro China yatageuza Cuba kwenda kwenye maendeleo ya haraka bila kulazimisha kuwa na vyama vingi.

Kleruu anazungumzia "ingredients" za demokrasia na anasema vyama vingi si lazima. Ndio maana nimeuliza demokrasia ya vyama vingi imeweza vipi kutusaidia kupiga kwa haraka hatua za maendeleo?
 
Unasema Mkjj anaakili fupi, ni mtu mfupi, pia ni mkatoliki... akupinge kama hayuko vile. Hapo hapo unasema humjui na hakuju lakini huna shaka na unachokisema. Kwa mantiki hiyo, je, watu wafupi wote ni wakatoliki? Je, wakatoliki wote ni wenye akili fupi?!

Hiyo kwenye Red, jibu lake ni hapana.

Hayo mengine ndio, apinge kama anaweza na atwmbie 1) kimo chake ana futi ngapi? 2) aseme mkatoliki au sio 3) majibu ya hayo mawili yatadhihirisha la tatu, "ana akili fupi".
 
Waliondoa vyama vingi kwa sababu waliogopa kupoteza madaraka uko siku za mbele.
 
Duh.. sasa sijatetea demokrasia ya chama kimoja - japo naweza. Hoja zangu zinaweza kulingana kabisa na zile za Kleruu. Tatizo ni kuwa watu wa Magharibi wametuambia demokrasia ni ya vyama vingi na sisi bila kuhoji tumeamini kuwa ndivyo ilivyo. Kwanini tunahusisha demokrasia na uwepo wa vyama vingi? Je kuwa na vyama vingi ndio kuwa na demokrasia? lakini vile vile tumeaminishwa kuwa demokrasia ya vyama vingi ni muhimu kwa maendeleo - kitu ambacho China na Vietnam zinaonesha kuwa si kweli. Na nina uhakika hata mabadiliko aliyoyaanza Castro China yatageuza Cuba kwenda kwenye maendeleo ya haraka bila kulazimisha kuwa na vyama vingi.

Kleruu anazungumzia "ingredients" za demokrasia na anasema vyama vingi si lazima. Ndio maana nimeuliza demokrasia ya vyama vingi imeweza vipi kutusaidia kupiga kwa haraka hatua za maendeleo?

Tunahusisha demokrasia na vyama vingi kwa sababu ya maana ya neno demokrasia. Watu hawawezi kukaa pamoja na kukubaliana katika kila kitu. Ni mara ngapi tumeona ushindani including ushindani wa ideas ndio bora? Sawa, kunaweza kuwa na ushindani katika chama kimoja, kama huo uliopo ccm na chadema, lakini tunajua mwisho wa siku, siasi za chama kimoja zinapendelea kikundi kimoja kitakachoweza kukusanya washabiki ndani ya chama. Mfano hai ni ccm sasa ivi na pia ccm wakati wa Nyerere.
From there, tunapokuja katika uchaguzi, mwananchi anakuwa na option gani katika a single party country? Au tunarudi kweli system ya picha au kivuli? Maana mwisho wa siku mwananchi anakuwa hana choice between developing policies at all, maana hizo zinatungwa na chama.

Pili, katika single party state kunakuwa hakuna separation between the state and the party. hili ndilo tatizo tunaloliona leo Tanzania. Ni wapi polisi wanachunga maslahi ya chama na ya serikali? Ni wapi jeshi linalinda maslahi ya chama vs serikali? The line is blurred and the system becomes open to corruption as it happened in Tz. In case you didnt know, people are inherently corruptive. A single party system allows the abuse of this characteristic. Kama ulisikia speech ya kiongozi wa chama cha kikomunisti china juzi wakisherekea miaka 60 yao, aliongelea swala la corruption linavyoanza kuikumba China.

Mwisho, demokrasia haimainishi maendeleo. Lakini inachangia sana katika kuleta changamoto ya maendeleo.
Swali lako la mwisho litahitaji analysis ya data kupata kipimo kizuri. Lakini pia tukumbuke maendeleo yanaanza na fikra. Tumeona jinsi gani mfumo wa vyama vingi umebadilisha fikra za waTz hasa ukiangalia huu uchaguzi wa 2010.
 
sasa hivi vyama vingi vimekuwepo kwa karibu miaka ishiriini, wamepoteza madaraka?
Maswali mengine bana, yaani kama sio wewe Mwkjj.

Kilichowafanya mpaka wavipige marufuku ni nini?

Tokea vyama vingi vipigwe marufuku, imechukuwa miaka mimgapi kuvirudisha?

Tena ndani ya katiba yenye mgogoro na viraka kibao.
 
Tunahusisha demokrasia na vyama vingi kwa sababu ya maana ya neno demokrasia. Watu hawawezi kukaa pamoja na kukubaliana katika kila kitu. Ni mara ngapi tumeona ushindani including ushindani wa ideas ndio bora? Sawa, kunaweza kuwa na ushindani katika chama kimoja, kama huo uliopo ccm na chadema, lakini tunajua mwisho wa siku, siasi za chama kimoja zinapendelea kikundi kimoja kitakachoweza kukusanya washabiki ndani ya chama. Mfano hai ni ccm sasa ivi na pia ccm wakati wa Nyerere. From there, tunapokuja katika uchaguzi, mwananchi anakuwa na option gani katika a single party country? Au tunarudi kweli system ya picha au kivuli? Maana mwisho wa siku mwananchi anakuwa hana choice between developing policies at all, maana hizo zinatungwa na chama.Pili, katika single party state kunakuwa hakuna separation between the state and the party. hili ndilo tatizo tunaloliona leo Tanzania. Ni wapi polisi wanachunga maslahi ya chama na ya serikali? Ni wapi jeshi linalinda maslahi ya chama vs serikali? The line is blurred and the system becomes open to corruption as it happened in Tz. In case you didnt know, people are inherently corruptive. A single party system allows the abuse of this characteristic. Kama ulisikia speech ya kiongozi wa chama cha kikomunisti china juzi wakisherekea miaka 60 yao, aliongelea swala la corruption linavyoanza kuikumba China.Mwisho, demokrasia haimainishi maendeleo. Lakini inachangia sana katika kuleta changamoto ya maendeleo. Swali lako la mwisho litahitaji analysis ya data kupata kipimo kizuri. Lakini pia tukumbuke maendeleo yanaanza na fikra. Tumeona jinsi gani mfumo wa vyama vingi umebadilisha fikra za waTz hasa ukiangalia huu uchaguzi wa 2010.
Mkuu Chapakazi. Nimekupata vizuri kwenye uchambuzi wako wa kina
 
Utawakomboaje wanyonge kama unatunza chuki na visasi moyoni mwako? Tangu lini mtu anayeongozwa na hisia badala ya busara akafanikiwa?Mwamwindi unaye mtetea wala hakuwa mtetezi wa wanyonge kama unavyomtetea wewe, bali alikuwa mtetezi wa wakulima matajiri(kulaks) waliokuwa wanamiliki mashamba kule Ismani na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kupelekea tishio la jangwa. Ukame mkubwa kule Ismani ulisababishwa na wao kukata miti kama hawana akili nzuri. Uko wapi ushujaa wa hawa waharibifu? Tuache hisia turudi kwenye busara(reason), yako wapi maandishi ya Mwamwindi kutetea tabaka lake lililoundwa na watawala wa kiingereza? Kleruu hata kama unamchukia aliacha maandishi ambayo ndio msingi wa mjadala huu.
we maulaga hivi una uhakika na unachokisema? hisia ni sehemu ya maisha ya kila binadamu, hata wewe pia naamini kabisa kama una afya timamu basi una hisia pia. mimi wewe nashindwa kukuelewa unaposema eti mwamwindi anahusika na ukame, mwamwindi alikufa lini na ukame umetokea lini? kama utetezi wa mtu ni maandishi basi watawala wetu wa jadi waliopigana dhidi ya ukoloni nao sio watetezi, ndugu yangu kama kusoma hujui je unashidwa hata kuangalia picha? si kila mtu duniani ni mwandishi, kumbuka kuandika ni kama kipaji, wapo watu wengine wanaweza kuandika lakini kutenda hawawezi na watu wengine wanaweza kutenda na kuandika hawawezi, hivi unafahamu namna gani mwamwindi na wakulima wenzie walivyokuwa mahili kwa ukulima wa mahindi? je unaifahamu vizuri historia ya isimani? mshenzi wewe usirudie tena kwaita waharibifu. Iringa iliitwa the big 4 kwa sababu ya wakulima kama mwamwindi. we mpuuzi ukame ismani ni kutokana na population pressure ilivyoongezeka mahali pale. kumbuka kuwa watu kutoka sehemu mbalimbali za iringa na mikoa ya jirani walikimbilia ismani kwa sababu ya rutuba ya ardhi ya isimani ambayo ilikuwa haihitaji mbolea kupata mazao mengi, kama we ni msomi nafikiri unafahamu fika ongezeko la watu sehemu linavyoweza kuharibu mazingira, enzi za kina mwamwindi huo ukame ulikuwa ni ndoto kwasababu ukame ismani umeanza miaka ya 2000. ukame wa ismani ni kutokana na uzembe wa selikali yetu ambayo haikuliona tatizo hili ikawaacha watu waende kwa wingi wakafanye wanachotaka bila shida yoyote, kama selikali ingeweza kukontro ongezeko la watu ismani ambao wengi ni wahamiaji mi nafkiri tatito la ukame lisingekuwepo.kwa taarifa yako kleruu alichukiwa sana enzi zile na wenyeji kwa sababu ya unyanyasaji wake na uonezi hivyo mwamwindi kumuua alikuwa amewaokoa wengi waliokuwa wananyanyasika na kuonewa na mpambavu huyu.kumbuka alichokiandika lenin hakuwahi kukitenda ila che guevala alikuwa mtendaji zaidi na si mwandishi. hata nyerere aliyaandika mengi ila hakuyatenda ila kikwete hajayaandika ila anatenda mabo ya kuwatetea mafisadi.
 
Tunahusisha demokrasia na vyama vingi kwa sababu ya maana ya neno demokrasia. Watu hawawezi kukaa pamoja na kukubaliana katika kila kitu. Ni mara ngapi tumeona ushindani including ushindani wa ideas ndio bora? Sawa, kunaweza kuwa na ushindani katika chama kimoja, kama huo uliopo ccm na chadema, lakini tunajua mwisho wa siku, siasi za chama kimoja zinapendelea kikundi kimoja kitakachoweza kukusanya washabiki ndani ya chama. Mfano hai ni ccm sasa ivi na pia ccm wakati wa Nyerere.

Maana ya "demokrasia" haihusiani na vyama vingi. Inahusiana na watu. Soma maelezo ya Nyerere kwa tume ya kupitia mfumo wa demokrasia ya chama kimoja na ujiulize ni kiasi gani mapendekezo yale yangezingatiwa yote ingewezekana kuwa na demokrasia ndani ya chama kimoja. Kleruu anaelezea vizuri kabisa kuwa demokrasia inaweza kuwepo ndani ya chama kimoja.

From there, tunapokuja katika uchaguzi, mwananchi anakuwa na option gani katika a single party country? Au tunarudi kweli system ya picha au kivuli? Maana mwisho wa siku mwananchi anakuwa hana choice between developing policies at all, maana hizo zinatungwa na chama
.

Ukiangalia vizuri utaona kuwa wakati wa chama kimoja wananchi walikuwa na best choices kwani mambo ya msingi yalikuwa yamekubaliwa na chama. Leo hii watu wanajikuta wanalazimika kupigia kura vyama tu bila kujali kama vina mambo ya msingi ambayo wananchi wanataka. Kleruu nalo kalielezea hili vizuri tu.

Pili, katika single party state kunakuwa hakuna separation between the state and the party. hili ndilo tatizo tunaloliona leo Tanzania. Ni wapi polisi wanachunga maslahi ya chama na ya serikali? Ni wapi jeshi linalinda maslahi ya chama vs serikali? The line is blurred and the system becomes open to corruption as it happened in Tz.

Well, hata leo kwenye mfumo wa vyama vingi bado jeshi lina utii mkubwa kwa chama. Na umesema vizuri tu. Lakini kwenye nchi kama China ambayo umetumia mfano jeshi na chama vimeweka uhusiano mzuri sana kiasi kwamba China imeweza kujenga jeshi zuri sana na imara na la kisasa. Hata sisi tulianza hivi kwa sababu jeshi lilikuwa truly chini ya wananchi. Leo hii Jeshi limekuwa la wanasiasa kwa sababu limechukua upande kwenye siasa za vyama vingi.

In case you didnt know, people are inherently corruptive. A single party system allows the abuse of this characteristic. Kama ulisikia speech ya kiongozi wa chama cha kikomunisti china juzi wakisherekea miaka 60 yao, aliongelea swala la corruption linavyoanza kuikumba China.

Hili halihusiani na chama kimoja. Hivi unafikiri Uingereza na Marekani au India hakuna corruption kwa sababu ya vyama vingi? Tena yawezekana kwenye vyama vingi - kama tunavyoona Tanzania - corruption is in fact embedded in the system itself. Chama kimoja kwa kiasi kikubwa sana kinazuia corruption endapo kuna mfumo mzuri. Kama unavyosema corruption ipo na itakuwepo. Lakini utaona mfumo mzuri wa chama kimoja unaweza kushughulikia zaidi corruption kuliko mfumo wa vyama vingi - hasa kama kwenye hivyo vyama vingi hakuna kilicho na nguvu ya kuchallenge kile kilichoko madarakani kama ilivyo Tanzania.

Mwisho, demokrasia haimainishi maendeleo. Lakini inachangia sana katika kuleta changamoto ya maendeleo.
Swali lako la mwisho litahitaji analysis ya data kupata kipimo kizuri. Lakini pia tukumbuke maendeleo yanaanza na fikra. Tumeona jinsi gani mfumo wa vyama vingi umebadilisha fikra za waTz hasa ukiangalia huu uchaguzi wa 2010.

Well.. utaona kuwa tulipiga hatua za haraka za maendeleo katika chama kimoja katika mambo ya msingi labda kuliko wakati mwingine wowote. China - mfano ambao napenda kuutumai - ndio taifa lililoweza kuwainua watu wengi zaidi kutoka kwenye umaskini kwa haraka zaidi kuliko taifa jingine lolote katika historia duniani. Lakini hili limewezekana chini ya a strong one party.
 
Kwachama kimoja, hamna haja hata ya kuwa na chama. Ni changa la macho. nikuwa na serikali peke yake, labda kama unataka kuongeza ajira tu. Hukna democracy katika chama kimoja, timu moja ya mpira , redio moja, gazeti moja, NK.
 
Maana ya "demokrasia" haihusiani na vyama vingi. Inahusiana na watu. Soma maelezo ya Nyerere kwa tume ya kupitia mfumo wa demokrasia ya chama kimoja na ujiulize ni kiasi gani mapendekezo yale yangezingatiwa yote ingewezekana kuwa na demokrasia ndani ya chama kimoja. Kleruu anaelezea vizuri kabisa kuwa demokrasia inaweza kuwepo ndani ya chama kimoja.

.

Ukiangalia vizuri utaona kuwa wakati wa chama kimoja wananchi walikuwa na best choices kwani mambo ya msingi yalikuwa yamekubaliwa na chama. Leo hii watu wanajikuta wanalazimika kupigia kura vyama tu bila kujali kama vina mambo ya msingi ambayo wananchi wanataka. Kleruu nalo kalielezea hili vizuri tu.

Well, hata leo kwenye mfumo wa vyama vingi bado jeshi lina utii mkubwa kwa chama. Na umesema vizuri tu. Lakini kwenye nchi kama China ambayo umetumia mfano jeshi na chama vimeweka uhusiano mzuri sana kiasi kwamba China imeweza kujenga jeshi zuri sana na imara na la kisasa. Hata sisi tulianza hivi kwa sababu jeshi lilikuwa truly chini ya wananchi. Leo hii Jeshi limekuwa la wanasiasa kwa sababu limechukua upande kwenye siasa za vyama vingi.

Hili halihusiani na chama kimoja. Hivi unafikiri Uingereza na Marekani au India hakuna corruption kwa sababu ya vyama vingi? Tena yawezekana kwenye vyama vingi - kama tunavyoona Tanzania - corruption is in fact embedded in the system itself. Chama kimoja kwa kiasi kikubwa sana kinazuia corruption endapo kuna mfumo mzuri. Kama unavyosema corruption ipo na itakuwepo. Lakini utaona mfumo mzuri wa chama kimoja unaweza kushughulikia zaidi corruption kuliko mfumo wa vyama vingi - hasa kama kwenye hivyo vyama vingi hakuna kilicho na nguvu ya kuchallenge kile kilichoko madarakani kama ilivyo Tanzania.

Well.. utaona kuwa tulipiga hatua za haraka za maendeleo katika chama kimoja katika mambo ya msingi labda kuliko wakati mwingine wowote. China - mfano ambao napenda kuutumai - ndio taifa lililoweza kuwainua watu wengi zaidi kutoka kwenye umaskini kwa haraka zaidi kuliko taifa jingine lolote katika historia duniani. Lakini hili limewezekana chini ya a strong one party.

1. Sijasema demokrasia ni vyama vingi, nimesema kuwa demokrasia inahusishwa na vyama vingi na sababu nimetoa. Unaongelea point za Nyerere mtu ambaye ideas zake hazikufanyikiwa. Nimeshasema, hizo alizoandika hapo look good on paper lakini haziko realistic hata kidogo. Kwanza kwa nini hawakuweza kuzi-impliment? Si alikuwa na miaka 25 ya kuzifanyia kazi? It all the same, just like vijiji vya ujamaa.
Kleruu anaongelea mataifa ya magharibu ku-emphasise demokrasia ya vyama vingi huku ana argue its possible kuwa na same system katika nchi ya chama kimoja. Lakini angeanza kwa kuangalia historia ya hizo nchi na kwa nini wana-propose hiyo system. Huwezi ku-adopt ideas nusu nusu, kwa mfano; u-adopt parliamentary system, actually the whole idea of government huku uache demokrasia. Kwangu mimi hivi ni vitu vinavyoenda hand-in-hand. Katika hiyo system lazima kuwa na checks and balances. Wengi wanadhani theory ya 'separation of powers' is limited to the checks and balances between parliament, govt and the courts. Lakini political parties zina-play a critical role katika kuhakikisha kuna checks and balances. Mfano, angalia scandals zilizotoka baada ya upinzani kupata sauti bungeni.

2. Nitapingana na wewe kuhusu point ya corruption. Corruption ni mchezo unaochezwa katika system yenye uwezo wa kuficha maovu. Katika a single party state, ambayo haina ushindani, au ushindani waweza kuwa easily manipulated ndani ya chama, (kama nilivyosema mapema juu ya watu kutengeneza makundi, nk), kuna uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi nyingi za kuficha hayo maovu kupitia makubaliano. Ivi waweza kuwa na bunge linalopitisha bajeti ya serikali huku bunge hilo hilo ndio limeweka serikali? The basic idea of separation of powers itatoka wapi hapo? Hii ina link to the point kuwa huwezi ku-adopt ideas nusu nusu. Kama unaamua kuwa na parliamentary system, ni lazima uweze kuibana serikali. Ndani ya chama kimoja hilo ni impossible.

3. Nadhani Japan ndio ina rekodi ya kuwa haraka kiuchumi zaidi. But nonetheless, China ni success story katika kukuza uchumi wake haraka. Lakini ni wazi hilo limefanyika kwa kuwa na sacrifices kibao. Kama uhuru wa maoni, uhuru wa media, haki za individuals, nk. Hizo ni key values katika demokrasia. Au sio?
Pia ni wazi kuwa kuna matatizo mengi watakayohitaji kuyaangalia hivi karibuni na wasipoangalia lazima hicho chama kitavunjika. Kwa maoni yangu, sidhani kama China itakuwa a single party state miaka 25 ijayo. Soma hiyo uone hali ilivyo:
BBC News - Inequality in China: Rural poverty persists as urban wealth balloons
(off topic) Hiyo ndio price ya maendeleo. Upinzani utaanza kutokana na a strong middle class which will inherently becoming more powerful with the money which creates a voice that will need to be heard, huku bado kuna a large rural population yenye sauti just because of its numbers. Baada ya muda and with life realities, ni wazi kuwa hizi kambi mbili zitakuwa zinataka maendeleo tofauti. Na huo ndio utakuwa mwanzo wa mpasuko.

4. My view is Kazi ya vyama sio kutuletea maendeleo bali kuhakikisha points of views za watu wengine zinakuwa accounted/catered for. Umeongelea juu ya mambo ya msingi kukubaliwa. Kwani sisi ni watoto au wajinga mpaka tuamuliwe mambo yetu ya msingi na kikundi cha watu? Hudhani kwamba hakuna tofauti juu ya hayo mambo ya msingi? Na siku zote kutakuwa na tofauti jinsi ya kufanya hayo 'mambo ya msingi', na hizo tofauti zitajionyesha katika siasa ya vyama vingi. 'Kwa mfano, swala la umeme, je tujenge power stations mpya au tulete wawekezaji kutusaidia, nk'. Kushindwa kuendelea sio kwa sababu ya kuwa au kutokuwa a single party state. Ni kwa sababu ya poor policies.
I argue in favour of multi party state kwa sababu ya umuhimu wa separation of power. That to me is so important na ndio kiini cha maendeleo na inventiveness.
Imagine Kambona angeruhusiwa kubaki na kuanzisha chama chake. Leo tungekuwa wapi katika sera mbalimbali?

P.S: Jeshi halitakiwi kutii chama bali serikali. The line is blur katika nchi ya chama kimoja which can lead to abuse of power. Nadhani uliona umuhimu wa jeshi katika mapinduzi ya Uarabuni (Tunisia na Misri). Uimara wa jeshi haujalishi chama kilichopo in power, bali funding za projects zake.
 
Back
Top Bottom