Uamuzi wa Kuingia Chama Kimoja: Maelezo ya Kleruu na Nyerere

Mkandaraa nimependa sana Comments yako hasa pale uliposema tujipime sisi kwa vigezo vyetu maana naona kama kuna waliotaka nisema sisi ni wavivu lakini fulani na fulani siyo wavivu! Labda Chapakazi alitaka niseme kuwa kulingana na hii michango fulani na fulani ndio wanaoneka hakusoma hizo nyaraka kwa uvivu wao wa kusoma lakini Chapakazi siyo Mvivu na amesoma hizi nyaraka!

Ahaa haa Chapakazi Bwana; anaweza kupitia michango yote kuanzia mwanzo kama shida yake ni kuainisha majina ya watu maana kuna wengine hata ukiwataja hapa haisaidi wao wamekuwa kama ugongwa kujiandikia lolote ilimradi mkono uende kinywani hawafikiri juu ya Tanzania ya kesho kwa vizazi vijavyo wanafikiri leo watakunywa Bia ngapi basi siku ipite.
 
Je mfumo wa vyama vingi ymetusaidia nini hasa? Umechangia vipi maendeleo ya nchi? Ukiondoa nafasi zaidi za kuwakosoa watawala na kuwajulisha wananchi madudu ya watawala mfumo huu umechochea vipi umoja, ushirikiano na upamoja wa kukabiliana na adui ujinga, maradhi, njaa na makazi mabovu? Katika mambo hayo manne are we better today than during the Single party state?
 
Mada za kukoshana, ukiandika kuhusu mtu yeyote ambae ana dosari, lazima ujuwe kuna wengine wenye hisia tofauti kwa hiyo usilazimishe kuandika uyaonayo wewe tu uandike na au uyasome na wayaonayo wengine. Kusameheana bila kujuana makosa mnayosameheana ni uongo.
Sioni sababu za kumpamba kleruu wakati hazipo.

FF a.k.a majimshindo, please try to understand the community. I know sometime it's hard because we have different background, different attitude, belief, taboo and culture. The civilized human is the one who can balance all of these to coexist.
I'm not interested to exchange words off topic because it is too low and not serve the society at all. However it is too much to ignore or condone.

Unaposema kuwa mtu mwenye dosari tayari umeshahukumu. Ni wewe uliyewahi kusema (zipo kumbukumbu) kuwa Osama bin Laden hana makosa. Sijui kwa kauli hiyo hukuwaudhi waliopoteza ndugu zao Dar embassy na kwingineko duniani?
Je OBL hakuwa na dosari.

Kilichowekwa hapo ni habari na wajibu wa mtu kusoma au kutukusoma ni juu yake. Halazimishwi mtu kusoma, lakini pia isiwanyime watu wengine fursa za kusoma. Title ipo wazi Dr Kleruu sasa kama hutaki kusoma huna sababu ya kufungua.

Wewe unachuki binafsi na baadhi ya watu, chuki hizo usizifanye za kitaifa na kuharibu mada kila mara. Kwa kadri unavyochukizwa na habari za Dr Kleruu ndivyo wanaJF wanavyokereka na utamaduni wako wa maudhi, kukosa uvumilivu na kuharibu mada.

Kama hakuna sababu za kumpamba Kleruu it's your perspective, usiifanye ni perspective ya taifa. It's you !! Ulipompamba OBL ilikuwa ni wewe na mawazo yako na hakuna aliyekusumbua.
Hii ni forum ya kubadilishana mawazo, kupingana kwa hoja au kukubaliana kwa sababu.

Inaudhi sana unapokifanya chombo hiki kama ukumbi wa mipasho isiyo na maana. Imefika mahali kila mada unayoingia watu wanatoweka kwenda kujadili kwa njia nyingine.

Tafadhali usinijibu kwasababu ni too low!!
 
Tafadhali usinijibu kwasababu ni too low
!!

Sikujibu pumba zako kwa sababu you are too high!
 
Je mfumo wa vyama vingi ymetusaidia nini hasa? Umechangia vipi maendeleo ya nchi? Ukiondoa nafasi zaidi za kuwakosoa watawala na kuwajulisha wananchi madudu ya watawala mfumo huu umechochea vipi umoja, ushirikiano na upamoja wa kukabiliana na adui ujinga, maradhi, njaa na makazi mabovu? Katika mambo hayo manne are we better today than during the Single party state?

"Men are born ignorant, not stupid. They are made stupid by education."
-Bertrand Russell
 
Sikujibu pumba zako kwa sababu you are too high!
Zipi ni pumba na zipi hoja will remain debatable. Bado naamini ingekuwa mada ni kumjadili Dr Kleruu kusingekuwa na haja ya kuweka nakala za maandishi yake. Waliopata muda wakasoma nakala zilizoambatishwa watakubali yapo maswali ya kujibu kuhusu hoja za Dr Kleruu na maamuzi ya serikali kuu wakati huo hususan Demokrasia.

Katika mfumo wa chama kimoja au vyama vingi vya siasa demokrasia yaweza kuenziwa au kudidimizwa kwa juhudi za waliopewa dhamana ya jamii. Kwa taifa changa kama tulivyokuwa Tz baada ya uhuru, mfumo wa chama kimoja ulikuwa muhimu kuzuia wakoloni kuwatumia vibaraka wao na kuendelea kuiyumbisha nchi kwa kisingizio cha demokrasia. Ilikuwa muhimu kwa wakati ule kuwa wamoja na kuendeleza harakati za kudai uhuru wa maendeleo uchumi na jamii baada ya uhuru wa bendera. Hata hivyo baada ya muda tatizo la ukiritimba lilipelekea walafi wachache kuyahodhi madaraka na kuendekeza ubinafsi/ufisadi wao. Hapo ilikuwa sahihi kuingiza mfumo wa vyama vingi vya kitaifa kwa lengo la kuwapa wananchi mfumo wa kukosoana kwa hoja ikitegemewa kuhimiza uadilifu serikalini. Kwa bahati mbaya waliokuwa na madaraka kwenye serikali ya chama kimoja hawakuridhia kwa vitendo mfumo wa vyama vingi. Wamefanya kila wawezalo kuupa sura potofu ili kulinda maslahi yao na wametumia madaraka vibaya kuhakikisha uhuru wa kweli katika malumbano ya hoja kisiasa haupatikani. Wametumia nafasi na rasilimali za taifa kuhakikisha uchaguzi wa huru na haki hauupo Tz. Katika hali hiyo ni vigumu kutadhmini mafanikio ya mfumo wa vyama vingi kwani bado haujaruhusiwa kuwepo Tz. Tunao mfumo jina tu mpaka sasa.
 
dr kleruu kiukweli mi sina shida na maandiko ya juha kama huyu, na bora aliuwawa maana alikuwa dikteta haswa, viva mwamwindi hata kama hukutungiwa wimbo wewe kwetu sisi wahehe unabaki kuwa shujaa daima, tunafahamu ulipotea kama mwanga wajua usiku lakini wanamapinduzi wa kihehe daima utakuwa mfano wa kuigwa kwetu, japo historia yako hawataki iandikwe lakini itadumu milele, hakika uliwakilisha na kuuonyesha ushujaa wa mhehe na kufanya iringa iheshimike maana baada ya hapo hakuna hata mtu mmja aliyeletwa akfanya uonezi kama wa mshenzi kleruu. nakumbuka harakati za wahehe walipokua wakipinga chuo kile kubadilishwa jina yaani kutoka iringa tearchers college hadi kleruu. Niliongea na dokta magoti aliyekuwa mkuu wa chuo wakati huo akaniambia ilikuwa ni shida sana kutembea na magari yaliyoandikwa kleruu maana yalikuwa yanapigwa mawe kwasababu ya jina hilo. kizazi cha sasa tunajipanga kuhakikisha kuwa kile chuo kinafutwa jina lile kwani ni fedheha kwetu kwa dr kleruu kuendelea kuenziwa kwenye ardhi yetu. unajua daima wahehe hatupendi kudhalauliwa kiasi hiki na nimekereka mno na hii post yako mwanakijiji, eti umeweka na wimbo wa kumuenzi mshenzi kleruu, huu ni upuuzi na ni kutuabisha watu wa iringa, hafai hata kidogo kupewa sifa yoyote kichaa huyu. wewe na hao wazee wenzio bora mngeitana bar na kuusikiliza huo wimbo. na ingekuwa amri ya watu wa iringa mwili wa huyu mkono wa chuma wangepewa mbwa wale kuliko kuimbiwa buriani.EHE! MUNGU KAMA KWELI KUNA MOTO BASI HUYU SHETANI KLERUU MFANYE KUWA KUNI NA MAJIVU YAKE MPE LUCIFERI ATUMIE KAMA KIUNGO KWENYE MBOGA ZAKE. mwamwindi fikra zako za ukombozi zidumu daima nadaima hata na vizazi vya sasa visimuliwe ili navyo vifanye maamuzi magumu kama haya.
Bhela, ndauli? Ubhanzite!? Hoja ya msingi ni kutazama pia "mazuri" ya Kreluu. Anzia pale miyomboni-posta-tanesco ya zamani-7 7-lugalo-sambala-majembe-kihesa sokoni-kilolo-mgongo-kising'a-mkungugu(kwao mwamwindi na mnarani alipouliwa Dr. Kreluu), umeupuuza uhehe! Think outside the ()!
 
Bila kuyasoma maelezo ya Dr Kleruu na Nyerere ni vigumu kuyakosoa kama yalivyo. Tutabaki kuandika hisia zetu kuwahusu wao na siyo hoja zao. It may never be fair to all and remains uncalled for.
 
Maandiko si vitendo.
 
tunachangamoto kubwa sana ya usomi; yaani ni changamoto kubwa kuliko tunavyofikiria na ndio maana nimekuwa si muumini wa siasa za "vijana" kuwa ndio wataleta mabadiliko kwa sababu ni hawa hawa waliosimuliwa vitu wakaviamini na wala hawajaweza kufanya intellectual criticism. Hata hapa tukianza kukosoa hilo simulizi la mauaji ya Kleruu utashangaa ni jinsi gani simuliza zima linavunjika kirahisi tu.

Hoja ni je Vyama vingi vimeimarisha kweli demokrasia tukilinganisha na wakati wa chama kimoja? Je, are we better katika kupambana na maadui wa maendeleo yetu kama ujinga, maradhi, njaa na malazi bora? Bado sijapatiwa jibu kama kulikuwa na makosa ya kuingia kwenye mfumo wa chama kimoja kama Nyerere alivyoelezea au kama Kleruu alivyoelezea. Kukwepa kuzungumzia hoja za kuingia chama kimoja ni kushindwa kuwa wa kweli wa historia na badala yake kuendeleza simulizi lisilo sahihi kuwa "nyerere alifuta vyama vingi".

a. Mfumo wa chama kimoja uliamuliwa na TANU
b. Ukapitishwa na Bunge
c. Ukaundiwa tume kuona demokrasia itaendaje chini ya mfumo huo
d. Na kwa muda mrefu tukaishi chini ya demokrasia ya chama kimoja.
 
Bila kuyasoma maelezo ya Dr Kleruu na Nyerere ni vigumu kuyakosoa kama yalivyo. Tutabaki kuandika hisia zetu kuwahusu wao na siyo hoja zao. It may never be fair to all and remains uncalled for.
mwisho wa siku hata ukisoma maelezo yao utaconclude it is a failure so tusome ya nini? wangekuwa walifanikiwa na hoja zao labda. MIMI NITAZIDI KUWA MKSOAJI WA HUYU MSHENZI KRLERUU DAIMA NA KWA HILI SITOFICHA HISIA ZANGU KAMWE, KWASABABU HULKA YANGU NI YA UKOMBOZI WA WANYONGE KITU AMBACHO MWAMWINDI ALIKIFANYA.
 
Wana agenda ya kumfanya nyerere kuwa a Saint he was not.
wape pole. maana kitendo tu cha kuidhinisha kifo cha our hero mwamwindi ni uthibitisho tosha kabisa kuwa hana hata chembe ya utakatifu anyway kama utakatifu hugawiwa kama vyeo vya ukuu wa mkoa au wilaya au ukurugenzi vinavyogawiwa hapa bongo basi atapata
 
Hoja Moja ya Kleruu: anadai Chama Kimoja kitaguarantee Umoja, ambao ni muhimu sana Kupambana vita vya "kubaki hai", sasa sijui hivyo vita vya kubaki hai haviwezi kupiganwa katika Vyama vingi?, au anataka kutuambia kuwa kuwepo vyama vingi hakuwezekani kuwepo na umoja wa kitaifa katika mambo ya msingi yanayohitajika katika "vita vya kubaki hai".

Kleruu anamnukuu Mwalimu Nyerere kuhusiana na hii dhana ya Umoja ili kupambana katika hii "vita ya kubaki hai" sasa cha kujiuliza ni hiki, je Mwalimu Nyerere baadae alikuja kufahamu kwamba kumbe hata Umoja wa nchi unawezekana hata ndani ya vyama vingi na hivyo kuvipigia debe mwaka 1992?, au je ilie vita ya kupambana na maadui wetu wakubwa , maradhi, ujinga, umasikini n.k haikuhitaji umoja tena?.

Kwa maoni yangu binafsi ni kwamba, kama wananchi wenyewe waliowengi kwa uelewa, bila ya vitisho wanataka chama kimoja, basi hiyo ni demokrasia, lakini ni lazima iwepo mechanism ya mara kwa mara kuonyesha kwamba bado wananchi wanataka hicho chama kimoja au wanataka system mpya, kiufupi ni lazima iwekwe mechanism flexible ambayo kila baada ya wakati fulani wananchi wataweza kuamua wanataka system gani.

mathalani kama tunaamini wananchi wetu wana uelewa mpana na tunawaamini, basi ilikuwa ni kosa kutowasikiliza mwaka 1992 waliposema wanataka Chama kimoja. lakini hofu yangu ni kwamba katika miaka ya 60 tulipofuta vyama vingi hatukuwauliza wananchi kama tulivyowauliza mwaka 1992 kwamba wanataka chama kimoja au vingi, TANU iliamua kuvifuta bila kuitisha referendum ya nchi nzima.
 
Je, leo hii katika vyama vingi tuna umoja wa kupigana vita ya kuwa hai? Unafikiri vyama vingi vimejenga umoja wa Watanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za ujenzi wa taifa kuliko ilivyokuwa wakati wa chama kimoja? Kwa maneno mengine, je Watanzania ni wamoja zaidi sasa hivi kuliko wakati wa chama kimoja?
 
tunachangamoto kubwa sana ya usomi; yaani ni changamoto kubwa kuliko tunavyofikiria na ndio maana nimekuwa si muumini wa siasa za "vijana" kuwa ndio wataleta mabadiliko kwa sababu ni hawa hawa waliosimuliwa vitu wakaviamini na wala hawajaweza kufanya intellectual criticism. Hata hapa tukianza kukosoa hilo simulizi la mauaji ya Kleruu utashangaa ni jinsi gani simuliza zima linavunjika kirahisi tu.

Hoja ni je Vyama vingi vimeimarisha kweli demokrasia tukilinganisha na wakati wa chama kimoja? Je, are we better katika kupambana na maadui wa maendeleo yetu kama ujinga, maradhi, njaa na malazi bora? Bado sijapatiwa jibu kama kulikuwa na makosa ya kuingia kwenye mfumo wa chama kimoja kama Nyerere alivyoelezea au kama Kleruu alivyoelezea. Kukwepa kuzungumzia hoja za kuingia chama kimoja ni kushindwa kuwa wa kweli wa historia na badala yake kuendeleza simulizi lisilo sahihi kuwa "nyerere alifuta vyama vingi".

a. Mfumo wa chama kimoja uliamuliwa na TANU
b. Ukapitishwa na Bunge
c. Ukaundiwa tume kuona demokrasia itaendaje chini ya mfumo huo
d. Na kwa muda mrefu tukaishi chini ya demokrasia ya chama kimoja.

Ivi mwanakijiji unaamini tupo kwenye mfumo wa vyama vingi? Au ni kwa vile wamesema hivyo na tunavyama vilivyoandikishwa ndio unaamini kuwa tuna mfumo wa vyama vingi?
Lets get serious, Tanzania bado ipo katika mfumo wa chama kimoja. Ndio maana kila siku tunaimba hapa ccm, ccm. With that argument, it means today's failures can be solely attributed to the single party state formed by Nyerere and co, as all failures are attributable to ccm.
How do you expect vyama vyenye less around 5% bungeni vilite mabadiliko? Mfumo wa vyama vingi upo in paper alone, na hili linajulikana wazi!!!!
 
kama unalosema ni kweli kwanini tusiuimarishe huu mfumo wa chama kimoja kwa kufuata misingi iliyomo katika hiyo hotuba ya Nyerere? Mapendekezo yaliyotolewa na tume ya kupitisha mfumo wa chama kimoja ni kwa kiasi gani yalifuatwa na kuzingatiwa? Je tuyaangalie tena na kuona jinsi ya kuboresha huu mfumo wa chama kimoja?
 
mwisho wa siku hata ukisoma maelezo yao utaconclude it is a failure so tusome ya nini? wangekuwa walifanikiwa na hoja zao labda. MIMI NITAZIDI KUWA MKSOAJI WA HUYU MSHENZI KRLERUU DAIMA NA KWA HILI SITOFICHA HISIA ZANGU KAMWE, KWASABABU HULKA YANGU NI YA UKOMBOZI WA WANYONGE KITU AMBACHO MWAMWINDI ALIKIFANYA.
Utawakomboaje wanyonge kama unatunza chuki na visasi moyoni mwako? Tangu lini mtu anayeongozwa na hisia badala ya busara akafanikiwa?Mwamwindi unaye mtetea wala hakuwa mtetezi wa wanyonge kama unavyomtetea wewe, bali alikuwa mtetezi wa wakulima matajiri(kulaks) waliokuwa wanamiliki mashamba kule Ismani na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kupelekea tishio la jangwa. Ukame mkubwa kule Ismani ulisababishwa na wao kukata miti kama hawana akili nzuri. Uko wapi ushujaa wa hawa waharibifu? Tuache hisia turudi kwenye busara(reason), yako wapi maandishi ya Mwamwindi kutetea tabaka lake lililoundwa na watawala wa kiingereza? Kleruu hata kama unamchukia aliacha maandishi ambayo ndio msingi wa mjadala huu.
 
Hoja Moja ya Kleruu: anadai Chama Kimoja kitaguarantee Umoja, ambao ni muhimu sana Kupambana vita vya "kubaki hai", sasa sijui hivyo vita vya kubaki hai haviwezi kupiganwa katika Vyama vingi?, au anataka kutuambia kuwa kuwepo vyama vingi hakuwezekani kuwepo na umoja wa kitaifa katika mambo ya msingi yanayohitajika katika "vita vya kubaki hai".

Kleruu anamnukuu Mwalimu Nyerere kuhusiana na hii dhana ya Umoja ili kupambana katika hii "vita ya kubaki hai" sasa cha kujiuliza ni hiki, je Mwalimu Nyerere baadae alikuja kufahamu kwamba kumbe hata Umoja wa nchi unawezekana hata ndani ya vyama vingi na hivyo kuvipigia debe mwaka 1992?, au je ilie vita ya kupambana na maadui wetu wakubwa , maradhi, ujinga, umasikini n.k haikuhitaji umoja tena?.

Kwa maoni yangu binafsi ni kwamba, kama wananchi wenyewe waliowengi kwa uelewa, bila ya vitisho wanataka chama kimoja, basi hiyo ni demokrasia, lakini ni lazima iwepo mechanism ya mara kwa mara kuonyesha kwamba bado wananchi wanataka hicho chama kimoja au wanataka system mpya, kiufupi ni lazima iwekwe mechanism flexible ambayo kila baada ya wakati fulani wananchi wataweza kuamua wanataka system gani.

mathalani kama tunaamini wananchi wetu wana uelewa mpana na tunawaamini, basi ilikuwa ni kosa kutowasikiliza mwaka 1992 waliposema wanataka Chama kimoja. lakini hofu yangu ni kwamba katika miaka ya 60 tulipofuta vyama vingi hatukuwauliza wananchi kama tulivyowauliza mwaka 1992 kwamba wanataka chama kimoja au vingi, TANU iliamua kuvifuta bila kuitisha referendum ya nchi nzima.
Tunafanya makosa ya kihistoria kulinganisha hali iliyokuwepo hapa miaka ya 1960 na ile ya 1992. Nchi yetu enzi ya miaka ya 1960 ilikuwa bado inavidonda vya "divide and rule" sera za wakoloni wakiingereza. Watanganyika walikuwa wamegawika mno kima kabila kama waingereza walivyotaka. Kwa hiyo umoja wawananchi ulihitajika sana ndio maana ukabila ulipigwa vita kwa nguvu zote. Kwa wakati huo demokrasia ya vyama vingi ingeweza kuhatarisha umoja huo kama ilivyokuwa Uganda ambako vyama vya siasa vilijikita kwenye udini au ukabila na ikawa vurugu tupu. Miaka ya 1990 watanzania walikuwa wamechanganyika sana kiasi kwamba mambo ya kikabila au udini yalikuwa hayana nguvu sana japokuwa sasa baadhi ya watu waovu wana anza kuyaanzisha kwa manufaa yao.
Isitoshe ndani ya siasa ya chama kimoja demokrasia ilikuwa kubwa na yenye nguvu kuliko sasa, tulishuhudia wabunge wakijadili hoja kwa umakini zaidi kuliko sasa, wala hakukuwa na wabunge ambao waliokuwa wanaisemea saerikali kama ilivyo sasa. Ni kweli bunge halikuwa na wasomi wengi kama ilivyo sasa, lakini michango yao ilikuwa inaoneka na wilikosoa serikali barabara. Wabunge walipita kwa kura halali bila kuchakachua kama ilivyo leo. Viongozi walikuwa wazalendo hawakuiuza nchi kama leo hii. Kuna kiongozi alipokea 10% kwenye ununuzi Panton, yalimkuta.
 
Back
Top Bottom