Uamuzi wa kufufua IPTL uongozi wa Tanzania unafahamu haya?

Nakwambia tutashuudia JK akijiuzuru kabla ya 2010 kama ana akili kwa sababu nchi imemshinda na washauri wake ni akina chiligati ambao hawajui chochote wananfikiri nchi inaendeshwa na ukada wa CCM.....hakuna babu elimu inatakiwa.
 
Katika maendeleo ya dunia hakuna short cut sasa CCM na serikali yao wanadhani ujanja ujanja utawatoa....hakuna na sasa tutashuudia kuanguka rasmi kwa serikali ya CCM.

Rais anakurupuka kutoa amri ya mambo ambayo hana utaalam nayo na wataalam wake ndo hao.....analo mkwere huyu.
 
Viongozi wetu ni short sighted, including huyo Zitto, maana alizungumzia IPTL pia kufufuliwa (don't change his words alizungumzia kutaifisha Dowans and kuwashwa IPTL) That is short sighted, undemocratic against free market economy and absolutely nonsensical. Cha kusikitisha rais anasikiliza ushauri kutoka media na amesikia Zitto kasema kitu na ye anafuata ushauri bila ku-weigh issue. Hivi ana kamati ya ushauri? I mean I am soooo curious how this man's mind work....
Naomba kuuliza hivi IPTL imewashwa au la? Maana naona mgao ghafla umeisha mjini (city center)... something is not right here....
 
Wakuu wa idara,

Mnasema JK ni shoti-saitedi? mbona hapa jamvini sikuona mtu yeyote akizungumzia hili suala la kisheria wakati wote tunatambua kwamba nchi yetu na ipiteli tuna kesi kwa pilato!

Kwanini hatukujiuliza kuhusiana na suala hilo na badala yake tukawa bize kuzungumzia ni jinsi gani mafuta ya kuwashia mitambo yalivyofika bandarini haraka!!

Okei labda tujitetee kwamba tuliambiwa na sirikali kwamba wameshafikia makubaliano ya kuwasha mitambo na ipiteli!!! oooh kumbe basi hao ipiteli niwale wa pale bongo ambao ni sheaholda wadogo ambao wanagombana na sheaholda wakubwa ndo maana wao walikubali harakakaraka (labda ni kau-uzalendo kalichangai pia!).

Ahnhaa na msimamizi wa ipiteli kwa sasa si ni RITA na si pia yuko chini ya JK sasa tulitegemea wambishie bosi wasiwashe huo umeme mmh.

Jamani ki-ufupi suala zima liko hivi; JK na watu wake walisha yajadili masuala ya kisheria naaa, ... naa, msimamo wao hautofautiani sana na ule wa kijana zito kabwe! (iwe isiwe umeme utawashwa tuuu)

Ndo maana hata jaji mzalendo ametupilia mbali pingamizi liliowekwa na mwanasheria wa hao ipiteli wakubwa, kwani jaji gani anayetaka kukaa kizani, kukaa ofisini bila ya kiyoyozi, kwenda ofisini bila kupiga pasi vazi lake, kupiga pasi kwa kutumia ile pasi ya mkaa ama kuhamishiwa ofisi ya sumbawanga!

Amani
 
Hvi Presidaa hana washauri???????????!
Washauri anayotokea yanaonyesha aina ya washauri alio nao. Katika hili, waziri Chikawe alitakiwa kufuatilia masuala yote ya kisheria na kuhakikisha kuwa yanawekwa sawa. inaelekea huyu bwana mkubwa hajafanya hivyo na ndio maana masuala yanaibuka kila kukicha. kama hao mawakili wangekuwa wametaarifiwa na kuhusishwa katika mazungumzo tangu awali, sidhani kama wangekuja na madai hayo
 
Susuviri,
Zitto alipendekeza mitambo ya IPTL iwashe wakati mipango ya kuinunua ikifanyika.. Ni wazo ambalo serikali na hasa Tanesco na Waziri wa nishati walitakiwa kufuatilia undani wa mitambop hii kabla hawajampa Go ahead rais kutangaza au niseme akubaliane na hoja ya Zitto.
Mkuu wangu ni Zitto aliyeamsha upya hoja ya motambo ya Dowans Kutaifishwa na huko pia hukubaliani naye..Sasa sielewi ktk swala zima la Dowans na IPTL wewe una msimamo gani.. kama wahenga wanasema great minds talk about Idea nadhani ni vizuri sana ukitupa idea yako badala ya kukamatia Zitto hivi Zitto vile.. wewe unachanghia kip[i mkuu wangu pengine utatusaidia zaidi kuhusiana na 1. Dowans, 2. IPTL..
 
I think Zitto was tryin to make a counter move.Itakuwa alipata kuvujishiwa hbari kuwa serikali ina mpango wa kuiwasha hiyo mitambo then akaamua kumove forward ionekane kama amewapa mwongozo.It waz jus a political timing...Ndio madhara ya zimamoto hayo!
 
Kifupi swala la IPTL tunalifufua sisi, ni shirika ambalo tayari limekwisha ingia ktk liquidation process hivyo kuwapa tender ni kufufua mradi uliokufa. Wanachogombania sasa hivi ni KISU tu, ulaji huooo wanauona unakuja ...It will cost us huge!..
Du watu mliona mbali!, hii ni five years ago!.
Pasco.
 
Du watu mliona mbali!, hii ni five years ago!.
Pasco.
Tatizo la wadanganyika mkuu wangu huyaona mambo yalipokwisha tokea, hatuna vision wala hawaoni mbali zaidi ya marefu ya kiganja cha mikono yao yaani pale tu wanapoweza kufikia. Na hata hii hutuba ya rais jana, nilijua atakuja na kamba gani maana inayoshitakiwa ni serikali yake sio Muhongo wala Tibaijuka bali mkataba mzima wa IPTL na PAP acha mbali wizi wa fedha za Escrow. Sasa rais atakapo kubali makosa yalifanyika ina maana serikali yake ndio iloingia mkataba haramu na hili la PAP ilikuwa ktk kupozea kero nzima ya IPTL kama ilivyotokea kwa mitambo ya Richmond (Dowans) kuchukuliwa na Symbion, sii yamezimwa? japo uharamu upo palepale..

ukweli ni upi basi, miradi yote ya uzalishaji umeme ambayo ni miundombinu ilitakiwa kuwa chini ya serikali (Tanesco) na usambazaji wake ndio ufanywe na mashirika binafsi wakati serikali iki control bei ya uzalishaji kutokana na gas yetu (faida hii ni ya baadaye) lakini kina sisi tumekubali kuwa gas ni ya wageni na hata uzalishaji umeme ni wa wageni inatugharimu na itatugharimu zaidi japo guaranture wa miradi hiyo yote ni serikali sio wawekezaji... tutapona kweli?
 
Mkuu Mkandara,

Sisi Watanzani ni mijitu mijinga ajabu!, kosa la Tibaijuka sio kupokea pesa bali ni kitendo cha kujulikana alipokea pesa!.

Hili lidudu IPTL linajulikana fika tangu lilipoanza ni kwa rushwa mwanzo mwisho!. Wakati linafanyiwa lobbying, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa, aligoma kupokea rushwa, akaletewa bulungutu la minoti mpaka nyumbani kwake, kwa vile tangu mwanzo alikataa, this time wakamtaim katoka, 'Mzee wa Kazi' akabisha hodi, house boy akafungua, akakabidhiwa mzigo siku ya 24 December, kesho yake ni Krismas!. Ujumbe huo ukaletwa kama 'zawadi' ya Krismas, ukaambatanishwa na kadi ya Krismas!, na kusainiwa na Bwana Mtoa Sadaka!", akitegemea demand za sikukuu na muambo wa January, lazima atashukuru!. Rutabanzibwa aliporudi nyumbani akakabidhiwa zigo lile!.

Kwa jinsi ile ile alivyokabidhiwa, tarehe 27, akalibeba zigo lile vile vile lilivyo na kulirudisha kwa 'mwenyewe". TISS walijua kila kitu, TAKUKURU walijua kila kitu, serikali ilijua kila kitu, they were all well taken care off, why only Tibaijuka?!.

Aliyekuwa Mkuu wa nchi alipokea ile zawadi ya Krismasi, Waziri wake pia alipokea!. 'Mtoa Zawadi' akawaarifu 'wakubwa", Rutabanzibwa alikataa zadi na kuirudisha, na yeye ndiye kikwazo pekee anayekwamisha 'mradi!', huwezi amini kilichotokea!, Rutabanzibwa aliondolewa, na mradi ukapitishwa!. Jee mnamjua waziri wake ilikuwa nani?!.

Nasema Watanzani ni mijitu mijinga, tunapigia kelele tujisenti twa escrow, ambayo sio chanzo ni matokeo tuu!, malipo hayo ya IPTL ynayobishaniwa ni kiwango cha capacity charges tuu, mkumbuke IPTL bado inameza mabilioni kadhaa ya utility kila siku iendayo kwa Mungu!, nobody cares!.

Turudi kwenye mgao wa Escrow, PAP amegawa 'sadaka' kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia Stabic Bank, kwa vile majina hayajatajwa, then its ok!. JR amegawa sadaka kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia account yake iliyoko Uholanzi, majina yapo na viwango vipo, na wanajulikana!, ila kwa vile hawajatajwa, Watanzania mazuzu tunashangilia Tibaijuka amewajibishwa!.

Nahisi sio wengi wanaojua kuwa IPTL/PAP bado inaidai Tanesco nyingi kuliko fedha zote zilizokuwemo escrow!, na kwa vile bado IPTL inazalisha umeme, deni hilo linaongezeka siku hadi siku, na malipo yake yatafanyika direct kutoka Tanesco into IPTL/PAP kimya kimya!, and life goes on!, nobody cares!, watu wanashangilia ujinga kwa kuangalia tulipoangukia baada ya kujikwaa, badala ya kuangalia tulipojikwaa!.

Mkuu shukran sana kwa kukumbuka haya maana tuliyazungumzia humu humu JF na watu wakampongeza sana Rutabanzibwa, mimi mmoja wao lakini alipohamishwa na kupelekwa wizara ya ardhi sijui ya ndani hakuna Mdanganyika hata mmoja alosimama na kumtetea ama kupinga. Leo hii wala hakuna anayejua huyu Mzalendo yuko wapi ama amekwama wapi..

Hii ndiyio Midanganyika ambayo kwa kusema tu hatujambo lakini kichwani hamna kitu, elimu yetu ya kukariri tuu na kujifunza kiiungereza kwa sana kama vile ni elimu bora ili tufanane na wazungu. Athari za utumwa zipo nyingi sana japo wengi wetu ni wazito hata kukubali. Siasa za leo ni za wachumia tumbo, ni tunatongozana na ahadi za ndoa wakisha pewa nafasi na kulishwa ndoa hakuna tena!

Miafrika ndivyo Tulivyo - Nyani Ngabu
 
Back
Top Bottom