Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
- Thread starter
- #121
Mkuu Nguruvi3 , nimependa sana mchango wako huu, haswa objectivity na impartiality yako. Kwa maoni yangu, Chadema hivi sasa kinahitaji washauri wa calibre yako more than any other time watakao wapa mtazamo wa outside the box. Najua kwenye safu yao kuna line-up nzuri ya watu makini wenye vision na mission ila naona bado hawana right strategies to hit the bull on time na kwa vile watu hawa ni part and parcel, dhana ya collective resiponsibility ina wa blind kutoona mapungufu yao.Mkuu Pasco niruhusu nizirejee hoja zako kama ilivyozileta nikiwa na mawazo huru yasiyofungamana na siasa za upande wowote au kuwa na ushawishi.

Hoja # 1:Ni kweli sheria hiyo si sahihi kwasababu ulizozitaja. Mahakama kuu ilitoa hukumu nadhani kesi ya Mtikila(Judge Rugakingira RIP). Serikali ilikata rufaa na suala hilo bado lipo mahakamani na sijui kwanini mahakama imeamua kulikalia kimya, pengine ni kutokana na conflict of interest kati ya wateule wa mahakama. Chadema inawajibika kwa sheria za nchi hata kama haikubaliani nazo hadi itapokuwa vinginevyo. Sisi wananchi tuna jukumu la kushinikiza kuhusu mabadiliko hayo. Labda ungesema Chadema walipaswa kuonyesha mfano tofauti ,lakini pia inategmea matokeo ya majadiliano kama ulivyoyaleta katika update yako.

#2: Bado tunarudi pale pale kuwa sheria zetu zina utata sana na sio kwa Chadema tu. Chama kinapokudhamini ni sawa na mwajiri wako wa zamani anapokupa reference letter na ukishaajiriwa ndio mwisho wa influency yake. Ndivyo ilivyo kwa madiwani, wabunge n.k mwajiri wao ni wananchi na wanawajibika kwao, lakini ni sheria hiyo hiyo inayosema chama kinauwezo wa kumvua uongozi mchaguliwa bila kumpa haki mwajiri (mwananchi) kumvua uongozi. Kwa mazingira yaliyopo Chadema ilikuwa na uamuzi unaolingana na sheria zetu, kama ni sahihi au la hilo ni jambo lingine,lakini je walifanya kulingangana na taratibu zetu, jibu ni ndiyo. Hapa ndipo tunatakiwa tuangalie upya wakati wa kujadili katiba mpya.

#3: Nadhani waliitwa katika vikao halali na hawakuwa condemned.Rejea update yako.

#4: Chadema haina sababu ya kufuata mipangilio ya CCM, na inadhima kubwa sana ya kubadilisha mwelekeo wa watu kuhusu uchaguzi ili watu wachague sera za chama na si mtu au watu. Kosa hilo limefanywa na CCM na linawagharimu ni vema Chadema wakalitafutia dawa.

#5: Haa! yaani makosa yaliyofanywa na CCM ndiyo yarudiwe na Chadema! CCM kinameguka kwasababu kiliacha misingi ya uongozi (principles) na kukumbatia haiba(personalities). Uamuzi wa Chadema ni wa kuonyesha njia kuwa wao wanaweza na hakuna zaidi ya Chama. Kuendelea kuwalea watovu wa nidhani ni kufuga na kuzalisha vi-EL na vi-RA au vi-CH vidogo vidogo na vitakapo ota mbawa ndipo yatawakuta ya CCM. Kinga ni bora kulilo kuponya.

#6: Uamuzi sahihi ni ule unaofaa kwa muda muafaka. Igunga ni jimbo moja tu na pengine RA asingejiuzulu tusingekuwa na uchaguzi. Ni bora Chama kikajijengea imani ya kuaminika bila hofu ya uchaguzi kwani chaguzi zipo nyingi na zitakuja lakini credibility ya chama hutengenezwa kwa miaka mingi na kuharibika kwa saa moja. Hakuna haja ya kuogopa maamuzi magumu kama yanayoisumbua CCM na serikali yake kwa hofu ya jimbo moja au mawili, gharama za credibility ya chama ni kubwa sana.

#7: Siasa za Tarime ni very complicated, Mwera alipotemwa Chadema akarudi CCM huyu hakuwa muumini wa sera bali tumbo lake. Nashukuru mh Mbowe alikwenda Tarime na kuwapasha ukweli. Kwa hali yoyote lazima tukubali siasa za Tarime ni beyond politics, ideology na policy.

#8: Nakubaliana na wewe kuwa bado uwanja wa mapambano si sawa(level), kuhusu kuunda coalition nadhani una maanisha na wapinzani wengine, labda tujiulize Mrema ba Cheyo ni wapinzani? CUF yenye uhusiano wa karibu na CCM ni wapinzani. Nadhani ili tuwe na uwanja mzuri agenda ya katiba mpya lazima ipewe kipaumbele , ichukuliwe na Chadema kabla ya mwaka kesho.

Hitimisho

Uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama ni sahihi kwasababu hakuna mtu au watu au Organization iliyowahi kufanikiwa bila nidhamu.

Ni nidhamu inayowatesa CCM sasa hivi.

Nilishawahi kuwaonya Chadema kuwa suala la Arusha lilikuwa la kitaifa na zaidi, na kuliachia madiwani ilikuwa kosa kubwa sana.

Hata baada ya kutangazwa muafaka niliwasihi watoe msimamo cha kushangaza walikaa kimya kwa wiki mbili.

Hii inaonyesha kuwa Chadema hawana vitengo vya kutathmini hali ya kisiasa na kufanya maamuzi ya haraka na busara.

Hili lilipelekea political base' kuwa demoralized.

Mkuatano wao wa Arusha na maoni juu ya uamuzi wao katika blogs na vijiwe unatetea hoja yangu kuwa wapenzi na wanachama walikereka sana na mwenendo wa Chama chao na kwamba maamuzi magumu waliyochukua wame excite base yao tena.

Ingawaje naunga mkono maamuzi ya CC lakini nadhani kuna mapungufu ambayo hayaelezeki kwa njia ya kawaida.

Uongozi wa mkoa na wilaya ulihusika vipi katika sakata zima na je hakuna uzembe miongoni mwao.

Najua uongozi wa wilaya umejikosha kwa kufanya mabadiliko lakini CC ya Chadema inapaswa kutoa kauli kuhusu ushiriki wao.

Pili, je mbunge wa Arusha anahusika vipi na amechukuliwa hatua gani. Kama uwajibikaji wake akiwa mjumbe wa Halamshauri ya jiji la Arusha ungekuwa sahihi mambo yasingefikia hapo yalipofikia. Yeye angekuwa kiungo muhimu sana kwa mawasiliano kati ya makao makuu na madiwani.

Nadhani inabidi CC itolee kauli kuhusu ushiriki wake vinginevyo itakuwa ni double standard.

Mwisho, je muundo wa Chadema upo kamilifu? Vinginevyo habari hizi zisingekuwa za mshtuko, na hii inapelekea niamini kuwa kuna vitengo ndani ya chama haviwajibiki. Utamaduni wa kuunda tume ni ishara ya uzembe kama tunavyoona ndani ya CCM na serikali yake.

Haiwezekani chama chanye sekretariati na CC vishindwe kuelewa nini kinaendelea katika political sphere hasa mambo ndani ya chama chao.

Kuna umuhimu wa Chadema kurejea utendaji wa vitengo vyake na wawepo watu makini zaidi. Chama hakiendeshwi na tume bali facts and principles

Ahsante
Kwa maoni yangu bado wako kwenye stage ya beating around the bush for too long. CCM wameshajua suala la katiba mpya ni crucial na threat kwa mustakabali wake kuendelea kuitawala nchi hii kwa kutuswa kama kondoo hivyo delaying tactics its their only weapon hivyo katiba hiyo itacheleweshwa mpaka eleventh hour such that Chadema will dance to its tune by the time they realise the games people play, it will be too little too late to do anything worthwhile.
Nguruvi nashauri for the sake of this nation, put your idears in black and white, wape ushauri wa bure in confidence. Wakimeza au wakitema itakuwa ni shauri yao but you'll have clear concious that "they were told!".