Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,440
- 113,445
- Thread starter
- #61
TLP ilikuwa na Mbunge mmoja tuu bunge lililopita, ni Benedict Mutungurehi (RIP), (Biharamulo), mara tuu baada ya uchaguzi, wakatibuana na M/Kiti wake Mrema, Mrema kamfukuza uanachama, aliopokwenda mahakamani, uamuzi ule ulisitishwa, ila wananchi wa Biharamulo, walikosa uwakilishi kwa miaka minne.Sheria hiyo kandamiziambayo hata mimi siiungi mkono inawanyima wananchi haki ya kuendelea kupata huduma ya mwakilishi wao waliyemchagua, sheria hiyo haiwaelekezi madiwani kutotii maamuzi yaliyotolewa na viongozi wao wa chama, nadhani uchore mstari kati ya hivyo viwili.
Najaribu kutaka kuelewa pendekezo lako ni lipi kwa hali kama hii iliyotokea kwa madiwani kukaidi maelekezo ya kamati kuu. Labda kwa ufupi tu,unaweza kuniambia wewe kwa mtazamo wako kamati kuu ya chadema ilipaswa kutoa uamuzi gani?
Hivi ndivyo nilivyosema kuhusu TLP.
Pamoja na yote aliyoyafanya Mrema, Mutungurehi bado ni mwanachama halali wa TLP na ni Katibu Mwenezi, kwa sababu zoezi zima limekiuka Katiba ya TLP, na kama kweli wajumbe waliridhia, basi TLP hakuna Chama.
Kwa kufuata principles of natural justice, 'No one is condemmed unheard', Mrema alipaswa kumuelekeza Katibu Mkuu wake kuitisha Kikao cha dharura cha Secretarieti ya Nec ya TLP na kuwasilisha agenda hiyo ya kumfukuza Mutungurehi, azmio la secretarieti hiyo ndilo lenye mamlaka ya kuitisha kikao cha dharura cha Nec ya TLP na kuijadili hiyo ajenda iliyo mbele yake, halafu Mutungurehi, angepaswa kuitwa na kuhojiwa kabla ya kufukuzwa. Hata kama angekataa, basi mamlaka ya kikao hicho ni kumsimamisha uanachama na kupeleka azimio hilo Mkutano Mkuu ambao ndio wenye mamlaka ya kikatiba ya kufanya hivyo.
Mrema yeye ndiye Mwenyekiti wa TLP, na Katibu ndiye Yeye, Kamati Kuu ni Yeye, Sectarieti ya TLP pia yeye, Halmashauri Kuu ni yeye na amejifanya pia ndiye Mkutano Mkuu kumfukuza Katibu Mwenezi ili awe yeye!. Huu ni udikiteta wa hali wa juu na naamini Msajili wa vyama halalifumbia macho hili, yaani chama chote kiko mfukoni!.