Uamuzi mzito Serikalini: Viongozi wa Juu wawajibike kwanza

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Malumbano yanayoendelea ndani ya Bunge letu tukufu, serikalini na wananchi juu ya posho za vikao si jambo la kufumbia macho, wabunge, serikali na wananchi kwa pamoja wanahitaji kutolea uvivu, vinginevyo tutazidi kulea uzembe katika huduma za umma na hata kutumia vibaya misaada tunayoletewa na nchi wahisani. Mfumo huo pale inapotakiwa wahusika kupata posho uingizwe kwenye system ya malipo na kuonyeshwa kwenye pay slip ili makato ya kodi yafanyike kihalali badala ya kuletewa ndani ya bahasha ili kukwepa kodi.

Kwa kawaida malipo ya posho kama hizo ni pato la ziada baada ya basic salary, mfumo wa kukatwa kodi unatakiwa uwe wa juu zaidi kuliko makato ya kodi katika malipo ya mishahara ya kawaida. Hoja ya kukatwa zaidi kodi katika malipo ya ziada inatokana na ukweli kwamba allowances ni pato la ziada. Viongozi serikalini wamekuwa wakijipendelea kwa kujiongezea mishahara na marupurupu na kuweka kando sekta muhimu katika kukuza huduma za msingi kama elimu, afya na huduma nyingine za jamii, hali inayoshawishi wataalamu mbalimbali katika taasisi na huduma za jamii kuacha kazi zao zisizo na malupulupu na kukimbilia kwenye siasa na hivyo kusababisha huduma muhimu za jamii kudumaa na kushuka kiwango sababu ya kuchoshwa na tofauti ya kipato na mafao mengine.

Uzoefu wangu umenipa ujasiri wa kutolea uvivu jambo hili kutokana na kufanya kazi ndani na nje ya Tanzania. Mataifa makubwa na tajiri duniani nikichukulia mfano taifa la Marekani, mfanyakazi anapokuwa na overtime, kodi ya overtime ni kubwa zaidi kuliko kodi anayokatwa kwenye basic salary. Malipo ya bonus nayo hali kadhalika huingizwa kwenye system ya mapato ya mfanyakazi, na huwa na makato makubwa sana ya kodi isivyo kawaida kwa vile huo si mshahara wake bali ni extra income. Watumishi wa serikali hutumia magari yao binafsi, na inapobidi kutumia magari ya kazi ni kipindi cha kazi tu na anaposign out basi gari hubaki kwenye garage na huenda nyumbani kwa kutumia gari yake binafsi. Hata Magari ya serikali ni ya kiwango cha kawaida kabisa ambayo hayalete gharama kubwa kununua au matengenezo. Hata financial card kama food stamp nk ni za kiwango cha chini ukilinganisha na zile za makampuni binafsi. Marekani magari yatumiayo na serikali ni Chevrolet na Ford, ambayo si ya gharama na vipuri gharama nafuu.

Nashtushwa sana na mpango wa serikali kwa ajenda ya kusamehe kodi mapato ya ziada kama posho, wakati mfumo wa kupeana posho hizo ni kwa viongozi wa ngazi za juu serikalini ambao wana mishahara mizuri, malupulupu mengi kama kuishi nyumba za serikali, kutumia magari ya serikali, gas kwenye magari kulipwa na serikali, madereva kulipwa na serikali, walinzi wa serikali, na baadhi ya viongozi waandamizi hata chakula kulishwa na serikali, na kwa mfumo huo pesa za mishahara yao hazitumiki kama watumishi wa kawaida ambao nao hukatwa kodi na hawapati tuzo ya sitting, standing, chalk fumes, kutunza na kutibu wagonjwa, mazingira magumu ya vyombo vya usalama nk.

Siyo siri mfano mzuri kampeni za uchaguzi uliopita kwa upande wa CCM zilitawaliwa na mizengwe ya rushwa yenye kutoa taswira ya kwamba wengi waliopo wamepata kwa mchezo mchafu wa kununua nafasi walizo nazo. Na kinachoendelea sasa ni jitihada za kuziba pengo la pesa walizotumia kuhonga kupata nafasi walizo nazo, na kisha kukusanya nyingine kwa ajili ya kutoa rushwa uchaguzi ujao ili waendelee kuwepo katika nafasi walizo nazo au kupata nafasi za juu zaidi.

Niseme kwa uwazi zaidi viongozi wetu wa leo wa serikalini ngazi za juu na wabunge wapo kwa maslahi binafsi zaidi kuliko jamii wanayoihudumia. Tofauti ya mapato na posho ambazo zinazidi kuweka ufa kati ya viongozi na wananchi wa kawaida vinaashiria hatari ambayo kama hatua muhimu hazichukuliwi huweza kusababisha matatizo makubwa amani yetu iliyotukuka kitaifa. Tumezoea kuandika kwenye vitabu na makaratasi na kuutangazia umma mambo ambayo yanaishia kwenye wino bila utekelezaji. Kama mpango wa maendeleao wa miaka mitano ulivyoainishwa na wakati huo huo serikali ikitetea wakubwa wasikatwe kodi kwenye allowances na pamoja na kutangaza katika mpango huo kuondoa posho wakati huo huo kutetea kwa nguvu zote inatia dosari kubwa sana kwa serikali yetu.

Nahitimisha kwa kauli ya Kiongozi wa upinzani bungeni Mheshimiwa Mbowe kwamba uamuzi mzito unatakiwa kuchukuliwa sasa hivi ili kujenga uchumi wa taifa na kuondoa hali mbaya ya maisha ya watanzania ambao wengi wao 80% wako katika lindi la umaskini. Uamuzi huo unatakiwa uchukuliwe kwanza na viongozi wa juu kabisa serikalini kama alivyofanya Rais wa Malawi kupunguza safari na inapobidi kusafiri daraja la kawaida ili kuokoa pesa. Rais Kagame naye ni mfano wa kuigwa alivyofanya nchini kwake. Si rahisi kiongozi au viongozi wa juu serikali kuwanyonyeshea vidole wa chini yake wakati wao wakitumbua raha kama kawa. Ukiona viongozi wa ngazi ya juu kabisa wanaishia kusema anayejiona yuko kinyume cha maadili basi ajichunguze mwenyewe na ajiondoe inaashiria dhamiri yake inamsuta na hawezi kufanya kwa uwazi kutoa maamuzi mazito kwa vile yeye mwenyewe ana boriti na hawezi kutoa kibanzi kwa walio chini yake.
 
Naamini posho na matumizi mengine ya ziada yanaweza epukika tu pale ngazi za juu serikalini wakiwa wakwanza kuonyesha mfano, vinginevyo tutaendelea na vita vya maneno huku taifa linazidi kudidimia na vizazi vijavyo kuisha maisha mabaya zaidi kuliko sisi tuliopo leo.
 
Kama mheshimiwa Mbowe ameonyesha njia na mfano, nani atafuata nyayo ndani ya serikali kuunga mkono?
 
Naunga mkono hoja ya kupunguza baadhi ya watumishi wa umma ambao nafasi zao si za lazima bali ni shauri ya kukirimiana tu na kuziacha nafasi nyeti ambazo hazijazwi kwa miaka nenda rudi.
Bora kuondoa wakuu wa wilaya na makatibu tarafa ili nguvu hizo zielekezwe kuajiri watumishi wa wizara ya elimu na afya.
 
This is strange and unacceptable. Huwezi kuanzisha thread halafu unachangia mwenyewe. Kwa nini usinge consolidate hizo subsequent comments kuwa thread moja ndefu? Unawezaje kujitungia mtihani na kujisahihishia wewe mwenyewe?
 
Jana niliona humu jamvini thread ya Mwanakijiji iliyokuwa ikipendekeza kwa wana JF kulivalia njuga suala la posho kwa kushinikiza wafadhiri kusimamisha misaada hadi serikali ifute posho hizo. Ushauri huo umeishia wapi? Na hii kampaini ya kupinga urejeshwaji wa chengi ya rada kupitia serikalini, mbona kama inadorola!
 
Jana niliona humu jamvini thread ya Mwanakijiji iliyokuwa ikipendekeza kwa wana JF kulivalia njuga suala la posho kwa kushinikiza wafadhiri kusimamisha misaada hadi serikali ifute posho hizo. Ushauri huo umeishia wapi? Na hii kampaini ya kupinga urejeshwaji wa chengi ya rada kupitia serikalini, mbona kama inadorola!

Wengi siku hizi wanavutwa na habari za matukio na mada zinazoinjikwa jukwaani kuzijadili hazichukui uzito stahiki
 
Du nihatari sana! Mh mtoto wa mkulima alisema pesa ya posho kwa wabunge ni pesa kidogo. Chamsimgi wananchi tupaze sauti zetu kupinga matumizi yasiyo na tija kwa taifa letu. Je waweza amini kuwa matumizi ya serikali ni makubwa kuliko pato letu. Tunaweza kuleta mabadiliko ya matumizi na uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wengine wa serikali tukiamua kwa pamoja sasa. Hivyo kumaliza tabia ya utoaji majibu mepesi kwa hoja nzito. Mungu atubariki sote.
 
Kauli ya mtoto wa mkulima si sahihi kwa vile posho wanalipana wakubwa na watumishi wa kawaida wanaovuja zaidi jasho na kufanya kazi katika mazingira magumu hawapewi posho. Kumbuka walimu wanatembea umbali wa kutisha na na pengine kuvuka mapori yenye kuhatarisha maisha yao kwa miguu au baiskeli, lakini hawafikiriwi posho ila wakubwa wanaoishi kwanye viyoyozi na magari ya bure. Waganga wanaotibu na kutunza wagonjwa wenye hatari ya kuambuzwa magonjwa. Mengi tu wananchi tunatakiwa tusimame kwa pamoja na kwa kauli moja.
 
Tuanze kwa kuunganisha wizara, hii itaokoa mabilioni ya shilingi.
Haya mapendekezo huwa yanapotea kwa sababu wengi wetu tupo kimaslahi binafsi zaidi si mabosi au watawaliwa.
 
Tuanze kwa kuunganisha wizara, hii itaokoa mabilioni ya shilingi.
Haya mapendekezo huwa yanapotea kwa sababu wengi wetu tupo kimaslahi binafsi zaidi si mabosi au watawaliwa.

Hoja nzuri sana maana utakuwa wizara moja imegawanywa kuwa zaidi ya mbili au tatu, mantiki ni nini kama si kugawiana madaraka kwa sababu ya kujuana ili fulani asikose mshiko?
 
Back
Top Bottom