Uamuzi gani utachukua??

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,083
1,135
Habari zenu wakuu.
Je!?shemeji yako akimpiga dada yako mbele yako uamuzi gani wa kwanza utachukua??
 
subiri itokee nitakuja na jibu, lakini pia naomba Mungu isitokee
 
Chukua jembe ukalime.
Kijana mkubwa bado unakaa kwa dada yako
Tena wewe ndo unasababisha apigwe, maana hufanyi kazi yeyeote zaidi ya kuangalia TV, jioni unaenda mazoezini kwa ajili ya kuandaa tumbo kupokea haki yake. Anza hata kuuza maji kwatoroli ukapange umuokoe dada yako

Afu uoe ili uwe bize na mkeo.
 
Lol! Yaani wewe!
Mi ntamtoa utumbo huyo shemeji! Kha! Kwake ntakaa, na kichapo atapata!
Where is my golden gun kwanza?
Chukua jembe ukalime.
Kijana mkubwa bado unakaa kwa dada yako
Tena wewe ndo unasababisha apigwe, maana hufanyi kazi yeyeote zaidi ya kuangalia TV, jioni unaenda mazoezini kwa ajili ya kuandaa tumbo kupokea haki yake. Anza hata kuuza maji kwatoroli ukapange umuokoe dada yako

Afu uoe ili uwe bize na mkeo.
 
Nitachapa wote makofi!Kwanini wasipigane chunbani waje kupigana mbele yangu.Hawana adabu kabisa.
 
baba yangu kumpiga mama yangu mbele yangu hawezi
halafu ndo aje 'kidudumtu' amguse sister mbele yangu...?
na ndoa itakufa hapo hapo...

offcourse wadada 'huwasamehe' waume zao but hakika hatarudia mbele yangu ujinga huo...
 
mie huwa siendi kuwatembelea dada zangu waliolewa na sababu nimewapa. Nalog off
 
Natulia kimya nausoma mchezo. Sina nafasi ya kuingilia mapenzi yao.
 
Ni vigumu sana kuamua maana inawezekana kukawa na sababu ambayo hata ingekuwa wewe ungeweza kutembeza kichapo kwa dada yako,ila si vema sana kuona dada yako akipigwa mbele yako na inashusha heshima,ila kwa kuwa ni mapenzi na maisha yao kuingilia si jambo jema ingawa kipigo kisizidi kiwango.
 
Kiukweli shemeji yako atakuwa hakuheshimu wewe, dada yako na familiya yenu kwa ujumla na ulilijua hilo sasa kwake ulifuata nini? muache dada yako aje nyumbani kutoa salam.

Japo akina dada nao niwakorofi sana na wakati mwingine majibu yao yanachochea hasira, ila tujitahidi jamani tusionyesha ukidume wetu kwa kuwapiga siyo vizuri kwakweli.

Napia ni kumvunjia heshima mkeo kumgombeza mbele ya mtu yeyeote, kama mnatatizo vumilia mwambie akiwa peke yake, ina uzito wa pekeyake hii
 
Lazima kutakuwa na kosa limefanyika, ila si vyema sana kuingilia mambo ya wanandoa/wapenzi mara nyingi wakipatana shutuma hurudi kwa yule aliyewasuluhisha!
 
Hapo itakuwa zinga la mtihani na nadhani ikitokea uamuzi ntakaouchukua nadhani ni wazo la kwanza ndo ntalifanyia kazi japo sijui itakuwa wazo gani
 
Ni vigumu sana kuamua maana inawezekana kukawa na sababu ambayo hata ingekuwa wewe ungeweza kutembeza kichapo kwa dada yako,ila si vema sana kuona dada yako akipigwa mbele yako na inashusha heshima,ila kwa kuwa ni mapenzi na maisha yao kuingilia si jambo jema ingawa kipigo kisizidi kiwango.

ahsante!,hili ndo jibu.*roger that*
 
Back
Top Bottom