Uamsho waibana Polisi Zanzibar

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
[h=4]
headline_bullet.jpg
*Radio, TV marufuku kutangaza vurugu za Uamsho
[/h]

[h=4]Vurugu zinazohusisha Jumuiya ya Uamsho Zanzibar, zimeendelea visiwani humo, huku kiongozi msaidizi wake, Sheikh Mselem Ali Mselem, akisema zinasababisha kulipiza visasi.[/h] [h=4][/h] [h=4] Sheikh Mselem alisema hayo jana mjini hapa katika mkutano wa Kamishna Msaidizi wa Polisi, Yussuf Ilembo na viongozi wa Uamsho, ukifanyika Makao Makuu ya Polisi Ziwani.[/h] [h=4][/h] [h=4] Alisema vurugu hizo ni kiashiria hatari kwani zinahatarisha amani, umoja na utulivu uliopo ikiwa hazitadhibitiwa haraka. “Taswira ya mauaji inaweza kuvunja mihimili ya amani na umoja miongoni mwa Wazanzibari, hatimaye wakagawanyika na kutokea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, Mungu atuepushie msiba huo usitufike,” alisema Sheikh Mselem.[/h] [h=4][/h] [h=4] Alisema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu athari za vurugu hizo. Katika hatua isiyotarajiwa, Sheikh Mselem aliwashutumu wanasiasa (pasipo kuwataja majina), akisema yanayotokea sasa ni matokeo ya mipango yao mibovu.[/h] [h=4][/h] [h=4] Alisema halitakuwa jambo jema ikiwa kasi ya mauaji ikiachwa iendelee, ili akasisitiza haja ya kumwachia huru kiongozi wa Uamsho, Amir Farid Hadi Ahmed mahali alipo. Kiongozi huyo alikanusha kukiri kuwa Jumuiya yake inaendesha ghasia hizo na kusema Uamsho ni mfano wa jalala ambalo vyombo vya dola vinalitupia taka ngumu na maji.[/h] [h=4][/h] [h=4] Hata hivyo, Amir Mselem alisisitiza kuwa udhibiti wa ghasia hizo uko nje ya uwezo wa Jumuiya yao, na kuitaka serikali kusikiliza kilio cha wananchi wa Zanzibar wanaotaka mamlaka kamili ya nchi na kumwachia kiongozi wao. [/h] [h=4][/h] [h=4] Aliulizwa kwa nini ghasia zinazuka baada ya mikutano katika msikiti wa Mbuyuni ambapo waandamanaji wanabeba bendera ya Jumuiya hiyo na kuchoma maskani za CCM, alisema, “huo ni utaalaam wa kipropaganda uliokosa ithbat.”[/h] [h=4][/h] [h=4] Alisema kubeba bendera si kigezo cha Jumuiya yake kuhusika na ghasia hizo, kwani zinaweza kutengenezwa na kundi la wahuni kwa lengo la kuzitumia na kufanikisha uhalifu wao.[/h] [h=4][/h] [h=4] Naye Kamishna Ilembo, alisisitiza kuwa polisi haijamteka na haijui mahali alipo Amir Farid, na kuitaka jamii kutoa ushirikiano. Alisema jumla ya watu 51 hadi sasa wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kuhusika na uharibifu wa vitu na mali, miundombinu ya umma, uporaji na uvunjaji wa maduka.[/h] [h=4][/h] [h=4] Wakati huo huo Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) Pandu Ameir Kificho, amezuia hoja binafsi ya kujadili vurugu zilizotokea katika manispaa ya mji wa Zanzibar. Vurugu hizo zilisababisha askari mwenye namba F 2105 kuawa kwa kupingwa mapanga na watu wanaosadikiwa wafuasi wa Uamsho.[/h] [h=4][/h] [h=4] Hoja hiyo ilikuwa iwasilishwe kama utekelezaji wa azimio la wajumbe wa BLW wa CCM, ambao juzi waligoma kuingia barazani wakidai serikali imeshindwa kudhibiti vurugu hizo. Mnadhimu wa wajumbe wa CCM, Salmin Awadhi Salmin, alithibitisha `kutupwa’ kwa hoja hiyo na kusema hawakutendewa haki.[/h] [h=4][/h] [h=4] Alisema hoja hiyo ilitarishwa kwa kuzingatia maslahi ya umma, baada ya vurugu hizo kusababisha athari za kiuchumi katika nchi na wananchi wake. Katika utangulizi wao, azimio walilotoa juzi walitaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema na Kamishina Jeshi hilo Zanzibar, Mussa Ali Mussa wajiuzulu kwa kushindwa kudhibiti vurugu za Uamsho.[/h] [h=4][/h] [h=4] Aidha walitaka Waziri wa Sheria na katiba Abubakary Khamis Bakary kuchukua hatua haraka za kuifuta Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu (JUMIKI) kutokana na kufanya shughukli za kisiasa badala ya kazi za kiroho kinyume na Katiba yake.[/h] [h=4][/h] [h=4] Aidha walitaka serikali kufanya tathimini za vurugu na kuwalipa waathirika wavurugu hizo. Naye Mnadhimu wa CUF, Abdalla Juma Abdalla, alipongeza hatua ya Spika huyo kwa madai kuwa mazingira yanayoendelea kujitokeza Zanzibar hayatoi fursa nzuri kujadili.[/h] [h=4][/h] [h=4] Alipoulizwa na NIPASHE, Kificho alikataa kuzungumza suala hilo. “Wewe si unasali basi twende tukasali Ijumaa mambo mengine siku nyigine au sio,”alisema Spika Kificho.[/h] [h=4][/h] [h=4] Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara ya kukagua maeneo yaliyoathirika na vurugu, ikiwemo kituo cha polisi Mkunazini na Masikani Kisonge.[/h] [h=4][/h] [h=4] RADIO, TELEVISHENI MARUFUKU KUTANGAZA VURUGU ZA UAMSHO[/h] [h=4][/h] [h=4] TUME ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) imesimamisha matangazo yote yanayohusiana na vurugu zinazofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Uamsho Zanzibar.[/h] [h=4][/h] [h=4] Kwa mujibu wa barua ya Tume hiyo kwa vyombo vyote vya habari, radio na Televisheni marufuku kutangaza matukio hayo na kituo chochote kitakachokwenda kinyume hatua za kisheria zitachukukuiwa dhidi yake.[/h] [h=4][/h] [h=4] “Kutokana na kukabiliwa na machafuko ndani ya nchi kumejitokeza baadhi ya vikundi vya watu wanaojiita uamsho na kusababisha vurugu ndani ya nchi Tume inasitisha matangazo yote yanayohusiana na vurugu hizo,” imeeleza sehemu ya barua iliyotolewa jana.[/h] [h=4][/h] [h=4] Barua hiyo yenye kumbukumbu namba TUZ/ SGL2/VOL.2/ 42 imesainiwa na Mtumwa B Mzee kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume hiyo na kusabazwa kwa vituo vya radio na televisheni visiwani humo.[/h] [h=4][/h] [h=4] “Kituo chochote kitakachokwenda kinyume na agizo hili bila ya idhini ya Tume ya Utangazaji Zanzibar hatua zinazofaa zitachukuuiwa dhidi yake,” imesisitiza barua hiyo yenye kichwa cha habari ,“Kusitisha matangazo ya vipindi vya Uamsho”.[/h]
 
Back
Top Bottom