Uamsho na Kauli Mbiu ya CHADEMA

Hivi hawa wana uamsho wana habari kuwa wafanyabiashara wengi kutoka zanzbar wapo bara na wamewekeza mitaji mikubwa tangu kwenye kilimo, viwanda hadi biashara ndogondogo? Mmi nadhani wakivunja muungano watakuwa wamewaumiza zaidi wazanzibari kuliko wabara, kwa hiyo nashauri wafuate tu taratibu za kuondoa kero za muungano badala ya kuuondoa huuo muungano, hii ni sawa na mtu anayeumwa kichwa halafu anamwomba daktari akikate ili kuondoa hayo maumivu kwavile jino likiuma huwa linang'olewa.
 
Kama Uamsho wakithibitika kuhusika na kuchoma makanisa kabisa atakayejaribu kuwahusisha uamsho na chadema ni mlenge ( toa l weka s). Kwani Chadema hawatangazi sera za watu wa dini moja,kabila moja,au jamii moja kuwabagua ama kuwashambulia wengine. Lakini kama uamsho wanaunga mkono msimamo wa Chadema ya kwamba wananchi wa Tanganyika na Zanzibar wana haki ya kuhoji,ama kuuliza juu ya muungano hapo sawa, Chadema wanasimamia haki na misingi ya demokrasia,watu lazima wapewe uhuru wa maoni!
 
Ndugu Kwanza naomba nikusahihishe. Msemo "mpaka kieleweke" sio kauli mbiu ya chadema. ni msemo wa kiswahili uliotumika miaka mingi kabla hata chadema hawajaanza harakati, na umekuwa ukitumiwa na watu ambao hawataki kukatishwa tamaa katika jambo wanalolifanya au wasiokubali kushindwa kwa dhuluma. Mifano ipo mingi Wanafunzi wa vyuo wanapodai maslahi yao, makonda na madereva wasipofikisha hesabu utawasikia wakisema mpaka kieleweke, wanaapolo wakitafuta mawe bila mafanikio utasikia mpaka kieleweke nk.
Mtu yeyote anayetumia lugha ya kiswahili aweza kutumia msemo huu kwa maana anayofikiri yeye itamtia moyo na kufikisha ujumbe kwa wahusika kuwa hawezi kukatishwa tamaa kirahisi.
Post yako imekosa mantiki kwa sababu unajaribu kuhusianisha makundi mawili ambayo hayana uhusiano huo kwa kuwa eti wametumia misemo ya kiswahili inayofanana. Hakuna hoja yeyote ya msingi umetoa ya kushawishi kuwa chadema wana jambo wanashirikiana na hawa wana uamsho. hata kama kuna maeneo ambayo sera zinaonekana kushabihiana lakini hili haliwafanyi kuwa na ushirikiano hata kidogo.
Naamini CHADEMA watafika zanzibar kuelimisha, lakini wataenda kama chama cha siasa km vile walivyo vyama vingine na si kwa gia ya uamsho.
-Kwanza ukumbuke Motive ya CDM ni kuelimisha watu haki zao, hawa uamsho ukisikiliza hotuba zao ni kujenga chuki dhidi ya watu fulani kwa kisingizio cha kuonewa
-Pili Chadema wanapingana na Ufisadi, Uamsho wanapingana na ukristo
-Tatu Chadema wanapigania katiba mpya ya nchi nzima, uamsho wanataka tu kuvunja muungano
Hawa huwezi kuwaweka meza moja hata siku moja

Mtoa mada hawezi kukuelewa maana yeye kazi yake ni moja tu kuichafua Chadema.Amini nakuambia hata waliochoma makanisa ni asilimia 90 ni wana CCM na si uamsho,lengo lao lilikuwa kama hili la mtoa mada.Yaani waje waseme CHADEMA HAO NDIO WAMESABABISHA AU KUCHOCHEA.na baada ya lile tukio Chadema wangetoa kauli zilizokaa kiurahisi kuzitumia magamba wangelipuka fasta kuwageuzia kibao chadema wanahusika.Unaweza kusema hili ni gumu,la hasha si gumu magamba wameanza kuchinja wanachadema,kushambulia wabunge,igunga wameua jamaa kwa sasa wako tayari hata kuvuruga amani ya nchi kwani wameshaona wao kubaki madarakani 2015 ni sawa na paka kuzaa tembo.Hata Igunga waliwatumia viongozi wa dini kuingiza hoja za udini.Jamaaa wanatapa tapa mbaya huyu mtoa mada anahusisha Chadema na uamsho kwa neno mpaka kieleweke.Magamba kweli kwishnei
 
Juzi nilileta mada yenye kichwa cha habari "M4C Zanzibar" nyuzi ilisema hivi:



Wengine wakanijibu bila kufikiri, kama hivi:



Leo kwa macho na masikio yangu kupitia taarifa ya habari ya ITV saa mbili usiku huu, nimemsikia Sheikh Farid wa Uamsho Zanzibar akiirudia kauli mbiu ya CHADEMA zaidi ya mara moja "mpaka kieleweke". Hakuna ataebisha kuwa huo ni msemo uliozoeleka katika uongozi na kila kada na mnazi wa CHADEMA.

Nawapongeza CHADEMA kwa kuwaamsha Uamsho kudai haki zao na ningependelea ushirikiano huo uzidi na kama Uamsho wanavyoiunga mkono CHADEMA katika harakati zao kwa kutumia kauli mbiu ya CHADEMA kwenye harakati zao ni wakati muafaka kwa CHADEMA kuitumia fursa hii na kuungana na Uamsho Zanzibar wasaidiane katika M4C, inaonesha wazi kuwa Uamsho Zanzibar na CHADEMA wana uhusiano usio rasmi na yote ni katika kutafuta mabadiliko ya ukweli "Change".

Hongera CHADEMA, hongera Uamsho Zanzibar.

Ni mlinganisho wenye hoja dhaifu mno.
Hii ni kauli ambayo hata mtaani hutumika kwa wanaodaiana. Uamsho hawana uhusiano wowote na CDM.
 
Sidhani kama hii ni sahihi!

Inamaana anaye mwambia mzazi wake "Mama Nakupenda" na mwingine akamwambia mkewe "Mama nakupenda" wakiwa wamelala anakuwa na maana ile ile ukiachilia mbali maneno kufanana na kuwasilisha dhamira moja. Hata kama ni mtu yule yule aka2mia maneno haya haya sidhani kama atakuwa na maana ile ile, na hili litajidhihirisha pale ambapo kila atakayeambiwa hivyo kuoji ni kwanini anapendwa? Maelezo yake sasa,.............mh!
 
Back
Top Bottom