Uamsho kushitakiwa Oktoba kwa kosa la Agosti, tunapata sura gani kwa Serikali?

Wimana

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
2,449
717
Wiki hii, Sheikh Farid na wenzake wamefikishwa kortini baada ya Sheikh Farid 'kutekwa' na kusababisha vurugu kubwa Zanzibar. Wengi tulitegemea wangeshitakiwa kwa vurugu za wafuasi wao wiki iliyopita.

Tujiulize; kwa nini washitakiwe kwa makosa waliyofanya mwezi Agosti? Serikali ilikuwa wapi wakati Masheikh hao wakivunja sheria Agost? Kwa nini Serikali inafumbia macho uvunjaji wa sheria kwa baadhi ya vikundi na watu, ni kwa maslahi ya nani?
Tabia hii ya kufumbia macho uvunjaji.
 
Upelelezi ulikuwa bado haujakamilika we mleta mada vipi huna elimu ya sheria?
huyo sheikh farid bora ashughulikiwe kisheria kwanza nina doubt uraia wake maana nimemwona front page ya tanzania daima ni mwarabu pure halafu anatuletea tabia za kigeni tanzania,, kama amechoka kukaa kwa amani akaombe uraia arabuni.
 
Hiyo ndio serikali dhaifu,kitu cha kwanza wachukue birth certificate ya sheikh farid watapata jibu.
 
Wiki hii, Sheikh Farid na wenzake wamefikishwa kortini baada ya Sheikh Farid 'kutekwa' na kusababisha vurugu kubwa Zanzibar. Wengi tulitegemea wangeshitakiwa kwa vurugu za wafuasi wao wiki iliyopita.
Tujiulize; kwa nini washitakiwe kwa makosa waliyofanya mwezi Agosti? Serikali ilikuwa wapi wakati Masheikh hao wakivunja sheria Agost? Kwa nini Serikali inafumbia macho uvunjaji wa sheria kwa baadhi ya vikundi na watu, ni kwa maslahi ya nani?
Tabia hii ya kufumbia macho uvunjaji

mhe. mnyika unakumbuka alisema nini bungeni? tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa nani?
 
Tabia za kuutumia mlango wa chai maharage kuustarehesha mwili
Nazjaz umenikumbusha Daladala zenu za Chai maharage kwa hiyo BOFYA HAPA Bendera za Uamsho zashushwa Zanzibar nzima Ahsante SMZ maana waliwadharau sababu hamkuwapa CHAI Kifo cha uhamsho kimeshafika na Pumzi imeshaanza kutolewa huku ndugu zao wakiwawekea Oxygen wapate kupuma uzur maana hali yao ni mbaya...... Katika hatua nyngne ambayo SMZ imeonesha kidogo makucha yake imeendesha msako mkali wa Bendera za Uhamsho na kuzishusha na kuondoka nazo, SMZ kutumia jeshi la polisi limekamata DVD zote na CD zinaonesha mambo ya Uhamsho.......tukio hili lilitokea pale Mlandege gari ya polisi ilpofka na kubeba kila kitu katka duka moja la wakala mkuu wa CD hizi maana ufanya biashara na kuuzwa nchi za Kiarabu na ulaya...... Ulinzi umeimarishwa Visiwani muda wote Jeshi la polisi linaonesha nguvu yake ambayo muda mrefu waliwalea Uhamsho sababu hawakupewa Ruksa....na mkakati uliopo ni kufutwa kabisa Uhamsho katka ramani ya Tanzania sababu ni Taasisi ya Kidini lakini inaingilia mamlaka ambayo si yake na kujenga chuki baina ya watu......
 
Last edited by a moderator:
kwani toka mtu ashtakiwe polisi jalada lifunguliwe, lipatiwe mpelelezi, upelelezi uanze, inachukua muda gani vile?
 
unapoleta maada kidogo uwe unafikiri siyo tu kwa sababu inakuuma sana au wakati mwingine inaona kama mtu ameonewa. soma hapa chini mifano michache ikusaidie

1. sadam hussen alihukumiwa kwa makosa aliyoyafanya mwaka 1983
2. uingereza wanafanya uchunguzi wa tv presenter (Jimmy savile) ambaye kwa sasa ni marehemu makosa ya kunajisi, nk. aliyoyafanya miaka ya 70 na 80.
3. Charles Taylor amehukumiwa kifungo cha maisha kwa makosa aliyoyafanya miaka ya 90
 
Kuna njia nyingi za kumsaidia mtu kutopatikana na hatia kisheria. Licha kinga au defences zilizomo kwenye vitabu vya sheria au presumptions, njia nyingine ni kumfungulia kesi ima chini ya kifungu tofauti cha sheria na kosa alilotenda au kwa kosa ambalo hakutenda au ambalo upande wa mashitaka hauwezi kuthibitisha beyond reasonable doubts au kutumia sheria kwenda kinyume retrogressively. Kwa hili la Farid ni mchezo wa kawaida sawa na ule uliotumiwa na polisi kumwachia yule kamanda wao aliyeua wafanyabiashara wa Morogoro Zombe. Hata kesi kama zila za akina Mahalu, Mramba, YONA na wengine ni mchezo huu uliotumiwa.
 
Kesi za jinai hazina "time bar". Hizo fani za watu sio siasa.

Ni kweli lakini wenye fani walikuwa likizo? Huoni kisiasa hilo lina gharama kubwa sana?
Kama kosa lingekuwa limefanywa dhidi ya mtu binafsi ningeunga mkono hoja yako, lakini tumetendewa jamii madhara yameenda kwa watu wengi sana.
 
unapoleta maada kidogo uwe unafikiri siyo tu kwa sababu inakuuma sana au wakati mwingine inaona kama mtu ameonewa. soma hapa chini mifano michache..

1. sadam hussen alihukumiwa kwa makosa aliyoyafanya mwaka 1983
2. uingereza wanafanya uchunguzi wa tv presenter (Jimmy savile) ambaye kwa sasa ni marehemu makosa ya kunajisi, nk. aliyoyafanya miaka ya 70 na 80.
3. Charles Taylor amehukumiwa kifungo cha maisha kwa makosa aliyoyafanya miaka ya 90
Invalid examples
 
Invalid examples

kajipange upya naona unaleta maada halafu hujui kwanini umeileta. hivi hujui kuwa farid alihojiwa na akachiliwa mwezi agosti na akaambiwa upelelezi unaendela au hilo ulikuwa hulijui?
 
Wiki hii, Sheikh Farid na wenzake wamefikishwa kortini baada ya Sheikh Farid 'kutekwa' na kusababisha vurugu kubwa Zanzibar. Wengi tulitegemea wangeshitakiwa kwa vurugu za wafuasi wao wiki iliyopita.
Tujiulize; kwa nini washitakiwe kwa makosa waliyofanya mwezi Agosti? Serikali ilikuwa wapi wakati Masheikh hao wakivunja sheria Agost? Kwa nini Serikali inafumbia macho uvunjaji wa sheria kwa baadhi ya vikundi na watu, ni kwa maslahi ya nani?
Tabia hii ya kufumbia macho uvunjaji

Huwa nasema mara nyingi kuwa Watanzania wanahitaji elimu ya uraia.
Angalia kwa mfano hii thread. Tittle inasema "Uamsho kushtakiwa".
Hapa ina maana Uamsho kama organisation.
Lakini kwenye thread ndani inasema "Sheikh Farid na wenzake wamefikishwa kortini"
Full mchemko. Uamsho haiwezi kushtakiwa na kama ikishtakiwa ina maana serikali inatambua Uamsho kama orgnisation halali.
 
sijui sheria za zanzibar zina semaje,lakini huku bara sheria ina ruhusu mtu kushitakiwa.
 
Hii ni sawa na makosa aliyo shitakiwa Shaikh Ponda na kundi lake. Ni makosa yanayotokana na Kuvamia kiwanja na kujenga msikiti, na uchochezi ambayo ni tofauti kabisa na makosa ya kuchoma makanisa.

Nafikiri kuna kitu hapo nyuma ya pazia kwani wote walikamatwa siku moja na ilikuwa wakti wa usiku.

Penye Ukweli, uongo unajitenga. Tuache mahakama zifanye kazi zake bila kuingiliwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom