Uaminifu katika biashara

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
Wakuu salamu zangu kwenu:

Nimekuwa na wafanyakazi kadhaa katika biashara ambao kitu kikubwa cha kukosana nao ni kutokuwepo kwa uaminifu katika pesa,,si mimi tu ila watu wengi sana wamewafukuza wafanyakazi wao kutokana na tatizo hili.

Hivi ni kwa nini watu wengi wanadharau uaminifu,,halafu huku ikijulikana wazi kabisa kwamba mwenyewe atajua.??

Uaminifu ni kitu kizuri sana kwa watu wenye fikira ndefu tofauti na wale wenye mitazamo mifupi,,mimi kwa mtazamo wa haraka huwa naona kama watu wa namna hii ni watu wasiofikiria kabla ya kutenda...maana kile unachomfanyia mwenzio mwenye kufikiria huwa anaimagine kama angefanyiwa yeye ingekuwaje?? Akiona ni safi basi ndio anakipitisha,,,lakini pia hufikiria hasara zake..

Kwa kutilia mkazo post hii kuhusu uiaminifu,,hebu tumnukuu raisi wa tatu wa marekani aliyejukana kwa jina la thomas jefferson aliyesema "honesty is the first chapter of wisdom" yaani uaminifu ndio ukurasa wa kwanza kabisa wa kitabu cha hekima" raisi huyu alikuwa ni mwenye kutafakari sana na alipelekea mafanikio makubwa katika nyanja nyingi sana zilizokuwa zikiwagusa wamarekani kwa kipindi hicho...kwa maneno haya ni kwamba watu wasio waaminifu ni watu wasio na hekima,na mtu akitaka kuwa na hekima basi sharti aanze kwa kuwa mwaminifu..

Msemo mwingine huu hapa "trust is the basis of all relations but a small mistake can harm all the relations just as a missing t can rust the relation" ukisisitiza mahusiano ya aina yeyote yamesimikwa katika mhimiri wa kuaminiana lakini kosa dogo katika huku kuaminiana lina madhara makubwa sana hata kuua kabisa mahusiano bila kujali yalikuwa muhimu kiasi gani..

Uaminifu,,,unazipa nafsi za watu waliokuzunguka raha na wanajisikia usalama kuwa na wewe..

Sijui nielezee vipi???? Lakini katika yoyote yale ninayozungumza namaanisha uaminifu ni kitu kizuri kuliko kutokuwa mwaminifu,,,semeni wakuu nyinyi mna mtazamo gani katika hili..

Asanteni
 
Pole sana,najua utakuwa umelizwa sehemu tu.
Any way tunapokuja kwenye neno Biashara hapa moja kwa moja ina involve pesa.
Sasa basi,ktk swala linalohusu money handling."HAKUNA KITU TRUST" Kumbuka they say we live with money , sleep with money,but we never get used to it and forever money will remain strange to all of us for generations.
Kama buddying enterpreneur,siku zote katika biashara hakikisha uko kwenye safe side hasa inapokuja kwenye
cash handling.Mara nyingi udhibiti wa biashara hutegemea na nature ya biashara.Siku zote trust technologies nasio mtu.Ila kuna biashara una hitaji ku build rapport(bond) na mteja(hii ni kitu tofauti kidogo)
Mfano,km ni biashara ya duka,hakikisha una Data base,barcode scanning,security cameras na hakikisha stock take inafanyika kila baada ya six months.km ni biashara ya magari makubwa(Trucks) funga GPS device,software sio ghali sana,hii itakusaidia kujua gari liko wapi,na utumiaji wa mafuta unaenda vipi,yaani kila activity yeyote itakayofanyika kwenye gari utaipata kwenye laptop yako.Km ni business partnership legal agreements lazima iwepo.
km uko nje omba deposit kwanza,mzigo ukifika akadeposit balance ndio apewe document za gari au mzigo.
Hakikisha pesa haipiti kwa middleman.
Kwa leo ni ishie hapa ila Dont trust people on money,invest in hi tech admn.techonologies (advanced cash registers).Km ni biashara ndogo weka utaratibu unaoeleweka ktk pesa.Ndio maana Mabenki ya
naomba securities kwa sababu haya tu trust,lasivyo your businees will go burst,jamaa watapata ajira kwingine.
 
Katika pesa ni kawaida kwa mtu kukosa uaminifu, kuna baadhi ya watu hawawezi hata kuwaonesha wake zao mahesabu yao ya kweli!
Hata hivyo usiumie sana ndugu, weka mfumo mzuri tu wa hesabu, kujua Lini umenunua bidhaa ngapi kwa bei gani na unauza bei gani ili upate faida ngapi (Hesabu rahisi sana, hata wakinga wa kariakoo wasioenda shule wanaitumia). Kisha kinachofuata ni kufuatilia stoko na mauzo regulale! Wewe angalia tu kama unaingiza faida inayotakiwa, mambo mengine mwache kijana awe huru, afanye kazi kama ni yake kwa kujua kwamba ndy kazi inayomweka barabarani. Kuibiwa kupo TU, hauwezi kukwepa, hata mkifanya kazi wewe, mkeo na watotto wenu, bado watoto watachukua chao, na mama yao pia atatia kibindoni kiasi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom