Uambiwe?!

Mwenzio nilisha unbuka nilipomwambia rafiki yangu kuwa mkewe anagawa chakula cha usiku kwa wasela. Si alikwenda kumambia mkewe kuwa mie ndio ource ya hiyo habari na matokeo yake nikawa adui ktk familia ile. Lakini baada ya kipindi cha miezi kadhaa si akawafumania laivu jamaa wakila kile chakula. Na sasa hivi wameachana na ma msapu wake na anaona aibu kuniomba radhi
its like that mkuu

labda kwa mbaaali badala ya kukwambia kwamba mwenzako anakula nje, ningekwenda kwa huyo mwenzako nimwambie akumbuke nyumbani, watu wakijua ni soo

asipoacha ndio unaangalia mengine lakini kwenda direct ni issue
 
Binafsi hua nafikiria siku nikiwa kwenye mahusiano alafu mwenzangu akawa sio mwaminifu...mtu wangu yeyote wa karibu akajua ningependa aniambie.Na ikitokea asipofanya hivyo nikaja kugundua alijua akanyamaza ntamkasirikia.

Faida ya kuambiwa ni kwamba unajua kinachoendelea na unajipanga kukabiliana na ulichoambiwa.Ubaya ni pale unapotembea kichwa juu ukijua umepata kumbe kila mtu anajua umepatikana.Wanakuchora kwa maana nyingine.
Je wewe unaonaje?Uambiwe au uachwe kizani?

Mbona unataka kuvuka daraja kabla hujalifikia ? Tukuambie kuhusu mpenzi wako halafu mkielewana tuonekane wambea eeeh ?
 
Kwanini tuna-focus kwenye negative tunapokuwa kwenye mahusiano??
Hebu tubadilike tunavyoyachukulia mahusiano. Kwenye mahusiano kuna raha nyingi sana, kama kufundishana, kukumbushana, kuelemishana, kutiana moyo, kufarijiana, kuonyana, na n.k.
Sio vizuri kuanza mahusiano ukiwa na wasiwasi au hujiamini au kumuamini mwenzio..

Ulicho highlight ni tofauti na unachopinga.
Kujua umepata maana yake unafurahia na kuridhika na mahusiano yako kwasababu unamwamini mwenzako na kujiamini pia.....kupatikana maana yake ni kwamba wewe unavyofikiri na kuamini sio.
Hamna aliyesema watu waanze kwa wasiwasi...swala hapa ni kwamba ikitokea mwenzako sio mwaminifu uambiwe au la!!!
 
very good Lizzy,

I was just like you when i was single, ukishaingia kwenye ndoa, ukajua maana ya ndoa na majukumu yake, siku zote utakua unasali usijue afanyayo mwenza ili ndoa yenu iwe imara na watoto wapate malezi mema

I wish ningeweza kudocument hii post halafu ten years down the road tuirejee wote, Mungu akituweka hai

:tape:

Kwa mara nyingine nisubirie ndoa ndo ntajua ehhhh??

Mi ndoani au la...popote pale ntataka kujua maana sitaki kua kicheko cha mji!
 
Mbona unataka kuvuka daraja kabla hujalifikia ? Tukuambie kuhusu mpenzi wako halafu mkielewana tuonekane wambea eeeh ?

Siwezi kumuona mtu mmbea kwa kuniambia ukweli na kwa njia ambayo sio ya kimbea!!!'
Ntapenda kujua ili nijiweke sawa....kutokujua ni sawa na kutembea na suruali ambayo imechanika matakoni mwenyewe hujui.Unatembea kwa madaha yote ukijua umetoka sana kumbe kila mtu barabarani anakuchora tu....by the time unagundua ulishageuzwa kituko!
 
Kwanini tuna-focus kwenye negative tunapokuwa kwenye mahusiano??
Hebu tubadilike tunavyoyachukulia mahusiano. Kwenye mahusiano kuna raha nyingi sana, kama kufundishana, kukumbushana, kuelemishana, kutiana moyo, kufarijiana, kuonyana, na n.k.
Sio vizuri kuanza mahusiano ukiwa na wasiwasi au hujiamini au kumuamini mwenzio..

Binafsi naona bora kuambiwa.

kuambiwa kuna faida yake, hapo wewe ndo unakuwa unamchora jamaa, ye anadhani wewe mjinga kumbe ye ndo jinga kuliko.afu pili unabadili style ya kujishaua mtaani.isije ikawa hujui mtaa mzima au rafiki zote wanajua we mashauzi meengi, ila ukiwa unajua haaa unakuwa na slow motion tu unawachora both jamaa na hao mafriends tena unawacheki machoni 90 degrees uone kama wanapeana ishara..mana sisi wakike nasi tuna mambo
 
mapenz ya wa2 wa2 ukiongezka na ww unapeleka umbeya sku wameptna utaumbka
 
Kwa mara nyingine nisubirie ndoa ndo ntajua ehhhh??

Mi ndoani au la...popote pale ntataka kujua maana sitaki kua kicheko cha mji!
na wee nawe

sikuwezi, unapenda tabu wewe, haya mdada
 
KUAMBIWA MIMI NI RUKSA,
NAPENDA UNAMBIE ILA KAZI YA KUFUATILIA,KUHAKIKISHA UNIACHIE MWENYEWE,
ILA MIMI KUKWAMBIA WEWE HAPANA HAPANA HAPANA,
SIWEZI KUKWAMBIA ,KSB NAOGOPA MUDDER CASE SIJUI KIFUA CHAKO KINA UJASIRI KIASI GANI WA KUPOKEA HABARI MBAYA,
UKIZIMIA JE?, UKIFIKA JE?, UKIPATA KICHAA JE?, aaakha naogopa kuambiwa eti mimi ndiyo source ya taarifa.
NAPENDA SANA KUWA MSIKILIZAJI KULIKO KUWA MSEMAJI ,,,lol.
 
Mi sitaki kabisa kuambiwa, kama lipo nitalijua tu mwenyewe na kujua ni deal nalo vipi. Kwani mimi naamini jambo baya huwa halifichiki kwa muda mrefu, ipo siku nitajua tu.
 
Mi sitaki kabisa kuambiwa, kama lipo nitalijua tu mwenyewe na kujua ni deal nalo vipi. Kwani mimi naamini jambo baya huwa halifichiki kwa muda mrefu, ipo siku nitajua tu.

ha ha ha ha inaelekea MATY mwoga wewe wa kupokea habari mbaya,
ndiyo maana unaona bora ujioneee mwenyewe,,,
 
Binafsi hua nafikiria siku nikiwa kwenye mahusiano alafu mwenzangu akawa sio mwaminifu...mtu wangu yeyote wa karibu akajua ningependa aniambie.Na ikitokea asipofanya hivyo nikaja kugundua alijua akanyamaza ntamkasirikia.

Faida ya kuambiwa ni kwamba unajua kinachoendelea na unajipanga kukabiliana na ulichoambiwa.Ubaya ni pale unapotembea kichwa juu ukijua umepata kumbe kila mtu anajua umepatikana.Wanakuchora kwa maana nyingine.
Je wewe unaonaje?Uambiwe au uachwe kizani?

Lizzy inaonyesha una hisia sana na mtu wako hii inanipa picha km kweli ww unajua kupenda ni nini au kupendwa ni kitu gani.

Ukweli inapotokezea hali ya kudanganywa wakati ulikuwa unamatumaini asilimia 99.9 kuwa unapendwa na hakuna mwingine, kweli inauma sana.

lakini hulka ya binadamu ni mbaya sana, pale anapoona ameaminika sana kupita kiasi, basi huanza kugeuza mambo na kutumia mwanya wa kuaminiwa kuanza kufanya UASI!, hali ambayo inaweza kuendelea pasipo ww kujua kwa muda mrefu sana pengine hata usijue kabisaa mpaka unaingia kaburini.

Sasa picha huwa inakuja kunoga pale ukigundua kuwa uliyemwamini kakugeuza ww ZUZU!

Unajua ukiambiwa au hata ukigundua mwenyewe maumivu ni yale yale maana ujumbe ni ule ule, isipokuwa tu uwasilishaji wa habari umetofautiana.

Ukiambiwa kuna tatizo lake: Unajua Chinese communication, yaani msg ikitoka point A hadi kufika Point Z, inakuwa imebadilishwa badilishwa sana, hata km maana bado ni ile ile, mfano: msukuma ataitamka kwa mkazo... eenhe , wakati mnyamwezi ataitamka soft kidogo. Sasa penye mkazo unaweza kuhamaki sana.

Tatizo jingine ukiambiwa, unaanza kupata maumivu na kufikiria mambo mengine kuwa hujaambiwa na huyo mtu wako kwa kuwa anakuonea huruma, au anaona yanagusa sana hivyo atayameza, sasa ww utahangaika kutaka kuyajua zaidi na asikupe yote. Maumivu yatazidi.

Mambo ya kuambiwa inabidi awe mtu wako wa karibu sana na we na "Communication skills' siyo hivi hivi tu,
siyo mf. mtu anakukuta sokoni na kuropkoka eeeh shoga, mumeo looo! au eeh kaka unatafuniwa mkeo !

Sasa upande wa pili ni ule wa kugundua ww mwenyewe: Hapa km ww una busara hutakiwi kukurupuka km kicheche au ndege kiotani, unatakiwa uvute pumzi, kisha ufuatilie kwa makini kubaini ukweli wote kiundani. Uzuri wa kugundua mwenyewe unakuwa jambo ni lako na unalisimamia ww bila kukimbilia ushauri kwanza. Ukiridhika na uchunguzi wako unafanya maamuzi mazito.
Unaweza kufanya mazungumzo,na km inashindikana basi UNAVUA GAMBA, hapa gamba nalozungumzia siyo km lile la sie sie emu, No. Hapa naamanisha unaachana kabisa na huyo mtu na kuanza mipangilio mipya.

Hapa inabidi uwe jasiri wa Moyo au uwe na kitu kinaitwa "Iron Nerves" ili usije pata Pressure.

Nadhani nimekusaidia kwa kiasi fulani.
 
na wee nawe

sikuwezi, unapenda tabu wewe, haya mdada

Hehehehe nakumbuka sana...ila nimesahau kitu gani kingine kile uliniambia nisubirie.Siku nikizashinda majaribu lazima nikutafute maana ntakudai soda zangu mbili!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom