Uambiwe?!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,806
59,285
Binafsi hua nafikiria siku nikiwa kwenye mahusiano alafu mwenzangu akawa sio mwaminifu...mtu wangu yeyote wa karibu akajua ningependa aniambie.Na ikitokea asipofanya hivyo nikaja kugundua alijua akanyamaza ntamkasirikia.

Faida ya kuambiwa ni kwamba unajua kinachoendelea na unajipanga kukabiliana na ulichoambiwa.Ubaya ni pale unapotembea kichwa juu ukijua umepata kumbe kila mtu anajua umepatikana.Wanakuchora kwa maana nyingine.
Je wewe unaonaje?Uambiwe au uachwe kizani?
 
Tatizo kubwa la kuambiwa hata na watu wa karibu ni uhakika wa maneno..kuna vitu kama chuki, wivu au tabia ya mtu kugombanisha watu kwa maneno ya hapa na pale. Labda awe mzazi au siblings wako hapo unaweza kuamini!..sijui marafiki au nani wengineo, hapo pagumu!!..
Watu wengine hawapendi kuingilia mambo ya wapenzi hivyo wanakaa kimya hata kama wan uhakika na kitu, mana wapenzi wanaweza kugombana na kurudiana wao wakaonekana wabaya hata kama walikuwa na nia njema..
Upande mwingine hamna kitu kinaumiza kama kuchoreka pale utakapopata ukweli wakati ni too late...
 
Tatizo ni kwamba ukiambiwa,jamaa akakubembeleza ukamsamehe,...alokwambia atakua kama adui maana mtaona kama alikuwa ana taka kuwa tenganisha!
 
bora kuambiwa uchape lapa mapema shost,
kuliko utembee kifua mbele huku wenzako
wanakucheka ujinga, lol! inakera kweli.
unaweza ukaambiwa na usichape lapa vile vile, jamaa wakazidi kukucheka ujinga. Jibu la uambiwe au usiambiwe litategemea kama unapenda "love iz blind" au unapenda "love is passtime".
 
kuna cku tulikuwa tunaongelea hii ishu na frnds zangu, 1 akasema yeye anapenda aambiwe ili ajue anapambanaje na hiyo hali, mwingine akasema hataki kuambiwa milele coz hata akijua bado hayupo tayari kutengana na mr wake na kuleta mgogoro kwa wanae 3 bado anaipenda ndoa yake sana sana kiac cha kwamba hata akionyeshewa huyu hapa anafanya bado haitabadili chochote kwenye ndoa yake zaidi ya huyu mtu kumuumiza roho yake, huyu aliniacha hoi coz alisema ataanza kupambana na huyo aliemeletea hizo habari...., mie nipo kama napenda kuambiwa but niambiwe kistaarabu, sio ile ya kishabiki, napenda mtu ajue itaniadhiri vipi so anianzie mbali sio kukurupuka tu, na sio mtu mradi mtu, awe wa karibu yangu sana na anaenijua vzr...kuambiwa kuna faida na hasara zake pia.
 
Tatizo kubwa la kuambiwa hata na watu wa karibu ni uhakika wa maneno..kuna vitu kama chuki, wivu au tabia ya mtu kugombanisha watu kwa maneno ya hapa na pale. Labda awe mzazi au siblings wako hapo unaweza kuamini!..sijui marafiki au nani wengineo, hapo pagumu!!..
Watu wengine hawapendi kuingilia mambo ya wapenzi hivyo wanakaa kimya hata kama wan uhakika na kitu, mana wapenzi wanaweza kugombana na kurudiana wao wakaonekana wabaya hata kama walikuwa na nia njema..
Upande mwingine hamna kitu kinaumiza kama kuchoreka pale utakapopata ukweli wakati ni too late...

hiyo ni kweli kabisa kabisa, sasa huyu frnd wangu aliependa kuambiwa, juzi juzi alikuja kuambiwa, tena aliambiwa mpaka hotel mr wake anayokwendaga, alifatilia mpaka hotelin na alikuta "live"...khaa wanaume wa musoma kiboko, mwanaume hakush2ka sana sana alimbadilishia mke kibao na kasheshe juu, umetokea wapi huku na kumtimua wakutane nyumbani, kafika home kagoma mazungumzo, ni wale wanaume wa kupiga, so huwa akiwa na hacra frnd anashindwa kumuuliza lolote coz huishia kutwangwa, hapo cjaona faida ya kuambiwa/kufatilia kuhivyo coz inaumiza tu na bado ndoa inaendelea...
 
Bora uambiwe ujue namna ya kutatua tatizo mapema
swali linakuja je una roho ya kupokea hayo unayoambiwa
au ndio inakuwa chonzo cha ugomzi wa mleta habari na mwenye habari

mie kama mie huwa naogopa sana kuingilia mapenzi ya watu, ni dada yangu tu niliewahi kumwambia hii hali, kwa frnds naogopa kama ulivyosema mwisho wa cku mleta habari inakula kwake/anaonekana mchonganishi/wivu etc, sasa ya nn yote hayo?..umenikumbusha frnd wangu mmoja alikuwa anaamini mr wake ni wale"mr perfect"...cku ya cku frnd alikuja kumpa hii habari aliumwa mpaka akalazwa kabisa na ndoa haikuvunjika sana sana mr wake alimpiga marufuku makali wife wake kuwa na urafiki tena na huyo frnd wetu aliepeleka habari, sasa hivi ni maadui wakubwa....hii ishu ina faida na hasara zake nyingi sana inategemeana na mleta habari.
 
Tatizo la kuambiwa ni hili cku mnapatana jamaa atakubembeleza hadi umuambie aliyekuambia wewe utajikoki nakumueleza alisanua, baada ya hapo kuna mawili either jamaa agombane nae au amtongoze sasa hapo ndio shida yenyewe.
 
Tatizo kubwa la kuambiwa hata na watu wa karibu ni uhakika wa maneno..kuna vitu kama chuki, wivu au tabia ya mtu kugombanisha watu kwa maneno ya hapa na pale. Labda awe mzazi au siblings wako hapo unaweza kuamini!..sijui marafiki au nani wengineo, hapo pagumu!!..
Watu wengine hawapendi kuingilia mambo ya wapenzi hivyo wanakaa kimya hata kama wan uhakika na kitu, mana wapenzi wanaweza kugombana na kurudiana wao wakaonekana wabaya hata kama walikuwa na nia njema..
Upande mwingine hamna kitu kinaumiza kama kuchoreka pale utakapopata ukweli wakati ni too late...

Lets say kuna uhakika....hamna chokochoko, wivu wala unoko!!!Bora kuambiwa uamue mwenyewe kusuka au kunyoa!!!
Hata kama utasamehe itakua ni kwa terms zako binafsi na hutochoreka tena maana huwezi kutamba ama kujionyesha mbele za watu kwamba ni hivi na vile kumbe hujui tu!!!
 
Tatizo la kuambiwa ni hili cku mnapatana jamaa atakubembeleza hadi umuambie aliyekuambia wewe utajikoki nakumueleza alisanua, baada ya hapo kuna mawili either jamaa agombane nae au amtongoze sasa hapo ndio shida yenyewe.

kuna wengine hata hawahitaji kubembelezwa Lily, anakuwa straight kabisa"nyamayao ameniambia.."...wakati mwingine haya mambo ni ya kuyaacha yalivyo aisee.
 
Wewe niambie na mimi nitatumia muda wangu kwa ajili ya kuchunguza ukweli wa jambo uliloniambia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom