U-Nchi wa Zanzibar, U-jamhuri wake, U-Taifa wake, au U-dola wake? Ni nini haswa??

Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
323
Niliipenda hii hoja, hebu tujadili.

Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu juu ya Zanzibar uliosababishwa na marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar. Mawazo mengi yameshatolewa, mengine yakirejea nyuma kwenye historia ya Zanzibar na mengine yakiangalia hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini, na mgawanyiko wa kijamii ulivyo huko unguja na kijamii, kuwepo au kutokuwepo kwake.

Mimi nataka nitoe mchango wangu kidogo katika masuala mawili, la kwanza ni dhana zinazotumika/au zilizotumika katika katiba na mjadala huu, na pili historia ya nchi inayoitwa Zanzibar na hii wengi wanaojadili wanaiita Tanganyika. Nianze na dhana: katika mjadala wa marekebisho haya humu JF na kwingineko maneno NCHI, TAIFA, JAMHURI (REPUBLIC), STATE (DOLA) yamekuwa yakitumika. Na wengi wetu tumekuwa tukiyatumia na kuonesha hisia zetu bila kutafakuri mfanano au utofauti wa maana za dhana hizo. Nchi kwa mfano, ni pande la ardhi, lenye mipaka inayotambulika, wenye nchi yao wakaitambua hivyo na majirani zao na walimwengu wengine wakaitambua hivyo. Ukiangalia maana ya dhana hii - pengine tusingekuwa na ubishi sana juu ya Zanzibar kuwa nchi au si nchi - kwa maana hii hapana shaka kuwa Zanzibar ni nchi. Na kwa kuangalia historia, Tanganyika tunayoizumngumzia imekuwa Nchi baada ya ukoloni, kumbuka Berlin Conference, mipaka yake tunayoililia imewekwa na mkoloni. Hapakuwa na Tanganyika kabla ya hapo (wajerumani walipotutawala). Na kama kutawaaliwa na wageni ndio kunatupa nchi, basi Zanzibar imekuwa NCHI awali zaidi ya Tanganyika. Hilo mosi.

Pili, kuna suala la Dola - mamlaka inayotawala katika pande la nchi, mamlaka hiyo ina vyombo vyake ambavyo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Sasa tujiulize hapa je Zanzibar ni dola kwa maana hii, tunaweza kubishana pia, lakini kilicho wazi ni kuwa kabla ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar zilikuwa Dola kamili zenye mamlaka katika masuala yote ya ndani na nje ya nchi zao pamoja na suala la Uraia. Baada ya Muungano, kinadharia, Tanganyika iliachia mamlaka yake yote na kuikabidhi dola ya Tanzania, na Zanzibar ilikabidhi baadhi tu ya masuala, yale yanayoitwa ya Muungano (yalikuwa 11 1964 sasa yako 22). Suala la kuachia mamlaka yote au sehemu ni la kawaida katika aina zote za muungano, Mathalani, tukiwa na sarafu moja ya Afrika Mashariki, tutakuwa, kama dola ya Tanzania tumekabidhi baadhi ya mamlaka na maamuzi kuhusu fedha kwa mamlaka ya juu ya Afrika Mashariki (ndio maana kwenye EU baadhi ya nchi kama Uingereza kwa kutaka kubakia na Sarafy yao hawawa sehemu ya Euro japo wao ni wana EU). Hoja yangu hapa ni kuwa hata Zanzibar wanayo dola, japo haina mamlaka juu ya mambo ya siasa za nje, usalama na ulinzi wa nchi, kati yamambo mengine. Utaifa, nayo ni dhana nyingine, Taifa ni kundi kubwa la watu - wenye historia moja, lugha moja, utamaduni mmoja, uchumi mmoja, na pande la ardhi (nchi) yenye mipaka inayotambulika. Mwalimu alitambua kuwa Tanganyika haikuwa bado Taifa ndio maana akaanza juhudi za Ujenzi wa Taifa, ili sote tulio Tanzania tujihisi kuwa tu Watanzania na tujitambue na kujitambulishaa hivyo. Mradi huu umeachwa na watawala wa baada ya Mwalimu na baadhi ya hoja zinazotolewa ni kielelezo cha kutokukamilika kwa mradi wa Ujenzi wa Taifa. Hoja yangu hapa ni kuwa hata Watanganyika, kama Mwalimu alivyokuwa akisema, bado si wamoja kwa maana hiyo ya utaifa. Hebu tuvunje muungano halafu tuone. Rwanda pale ile Genocide ilitokeaje (hili ni suala jengine kabisa japo muhimu kwetu kutafakari). Kuna dhan hii nyingine, ya Republic (Jamhuri), hii ina maana ya utawala ambao msingi wa mamlaka yake ni watu na Mkuu wa Nchi ni Rais wa kuchaguliwa na watu. Dhana hii chimbuko lake ni karne nyingi zilizopita ambapo Ulaya kwa sehemu kubwa iliamua, baada ya mapambano makali, vita na mapinduzi kuachana na utawala wa kifalme (ambapo chimbuko la mamlaka haikuwa watu bali mfalme). Sasa Tanzania, na pengine Zanzibar katika zipo katika hadhi hiyo katika hali halisi. Kweli tunayo Jamhuri Moja ya Muungano wa Tanzania, yenye mamlaka juu ya masuala yote ya iliyokuwa Tanganyika na baadhi ya Zanzibar. Sasa mgogoro uko wapi katika marekebisho haya ya katiba? Kinachojadiliwa ni nini hasa U-Nchi wa Zanzibar, U-jamhuri wake, U-Taifa wake, au U-dola wake? Ni nini haswa kinagomba?

Mara nyingi, katika masuala kama haya watu hutumia 'mtima' na sio akili kufikir, matokeo yake huwa ni kufikia hitimisho zisizo na mantiki ambazo madhara yake huwa yenye gharama kubwa. Rai yangu, marekebisho haya yameleta suala la kutufanya tujadili masuala na mustakabali wa nchi yetu, lakini tukiongozwa na ufahamu usio shaka wa kile tunachokijadili. Vinginevyo tutajikanganya tu.
 
Hizi ndio mada tunazozihitaji, mada zenye akili, mada zenye nizamu, mada zilizokwenda shule.sio zile pumba za Mwanakijiji hili darasa tosha kwa watu wa aina MWKJJ wanaotumia moyo badala ya akili.
 
Hizi ndio mada tunazozihitaji, mada zenye akili, mada zenye nizamu, mada zilizokwenda shule.sio zile pumba za Mwanakijiji hili darasa tosha kwa watu wa aina MWKJJ wanaotumia moyo badala ya akili.

Sina sababu yoyote ya kumtetea au kumsemea MKJJ, lakini nina sababu za msingi za kuhoji kauli zinazolenga kumvia kimawazo. Si mara zote nimekuwa na mtazamo au kukubaliana na hoja za MKJJ na kwakweli nimekuwa natofautiana naye kihoja na si ''personality'. Mara zote ninapotofautiana naye MKJJ amekuwa mwepesi kukubali au kukataa maoni yangu kwa HOJA tena akishukuru.
Hii mada unayosema imekwenda shule haikudondoka kama mvua,chanzo chake ni hoja za MKJJ. Kwa wale wote wanaounga au kupingana na hoja zake tunakubali kuwa MKJJ anatumia akili zake kujenga hoja. Kwa mfano amewahi kuuliza ''Hivi baraza la wawakilishi likikubali mabadiliko na bunge la JMT likaktaa itakuwaje?" hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuja na jibu. Je hii si ishara ya uelewa mkubwa wa mambo!
Nadhani tusiangalie umbile,moyo, ukubwa au udogo wa kichwa chake, tujadili hoja zake nyingi zenye mashiko na kufikirisha.
Kwa wale waliosoma ''this day'' kuhusu EL watanielewa ni kisema MKJJ anajenga hoja za kufikirisha sana hata kama hatukubaliana nazo.
Tujibu hoja zake waungwana. Mimi nasema MKJJ kejeli hizi zichukulie kama challenge na songa mbele,sema kile unachoamini wewe na si kile kila mmoja anachoamini. keep it up MKJJ!
 
Hizi ndio mada tunazozihitaji, mada zenye akili, mada zenye nizamu, mada zilizokwenda shule.sio zile pumba za Mwanakijiji hili darasa tosha kwa watu wa aina MWKJJ wanaotumia moyo badala ya akili.

nipersonal au ndio uwezo wako wa kujadili mambo?, katika hii hoja sijaona hata sehemu ambako MWKJJ amezungumzwa, inakuwaje wewe unamwingiza kwenye hii hoja, kama una walakini nae kwa nini usifungue Thread maaluma ya kumwelezea MWKJJ na pumba zake?, HApa unatupa mashaka sana na uwezo wako wa kupambanunua mambo na uwezo wako wa kujua kinachoendelea, Hoja ni nyingine na wewe unakuja na vitu vingine
 
Hizi ndio mada tunazozihitaji, mada zenye akili, mada zenye nizamu, mada zilizokwenda shule.sio zile pumba za Mwanakijiji hili darasa tosha kwa watu wa aina MWKJJ wanaotumia moyo badala ya akili.

Hoja au mchango wako kwenye huu "uelewesho" ni nini ndugu ili tujadili na kupata ufahamu mzuri badala ya " pumba" kama unavyoziita wewe.

Binafsi nadhani hili swala la Zanzibar halieleweki vizuri na "watanganyika " kama walivyokuwa kabla ya Tanzania, na hata hao "wazanzibar" ambao wamekuwepo siku zote ( hawajabadilishwa kumbuka).

Kuhusu Zanzibar ni nchi ama la, Zanzibar ni pande la ardhi haina ubishi lakini ukumbuke kuwa unaposema
"nchi" moja kwa moja kwa uelewa wepesi unapata dhana ya "SOVEREIGN STATE"- WHICH ZANZIBAR IS NOT AM AFRAID. Zanzibar ni sehemu ya MUUNGANO na ndio maana kuna hoja lukuki za kutaka kutembelea tena framework nzima iliyoleta muungano, kuangalia kero zilizomo na kutafuta namna ya kuziondoa. Kero mojawapo ndio hii ya kutaka ZNZ ipate " sovereignty" na katika utaratibu ulivyo sasa haiwezekani maana unaharibu the essence of the union itself. Huu ni mfano mmoja tu.Sasa wewe what is your take?
 
Maneno yana maana zaidi ya moja ndio maana kwenye katiba kuna maana ya maneno yaliyo tumika kwenye katiba husika. Kuna maana ya maneno zinazopatikana kwenye kamusi kama za kiingereza, na hata za nyanja mbali mbali kama sayansi. Sasa je Wa Ndima ametoa wapi hizi maana? Je, hazina zaidi ya maana moja? Je, zinatoka kwenye Poltical Science kama somo? Je, Wa Ndima ni political scientist?

BinMgen unaweza kutuonyesha pumba za Mwanakijiji? Je, Wa Ndima hajaweka pumba hapo? Je kuna NCHI ambayo haina DOLA? Je, NCHI na STATE tofauti yake ni nini? Je, tofauti ya Country na Nation ni nini? Maana ya haya maneno yanategemea contexts na source. UN wana maana na vigezo vyake, kamusi zina maana sawa au tofauti, n.k.

Naomba Wa Ndima atupe source za maana hizo na kuzingatia katiba ya Zenj and Muungano katika context halisi sio kuleta historia tu bila back up wala evidence!

Hivi Euro haitumiki UK? Mbona kuna items zina Euro price ndani ya UK? Sio kwamba wana Legal tender - pound na euro?
 
Waacheni wa Zanzibari wa enjoy Muungano huu wao wana wabunge 50 katika
Bunge la Jamhuri ya muungano, wana Baraza lao la Wawakilishi linalifanya kazi kama Bunge,
wana Rais wao na pia wana vikosi vyao vya ulinzi.

Lakini pia wanatumia Polisi moja na Jeshi moja la Jamhuri ya Muungano nafikiri
wanafaidika zaidi jamaa hawa. Lakini cha kusikitisha zaidi bado maisha ya wananchi
huko ni duni sana pamoja na kuachiwa mambo yao ya ndani Elimu na Afya havijapewa
kipaumbele cha kutosha.
 
Back
Top Bottom