Tyson "Wassira" kuwa Waziri Mkuu?

# Member of Parliament - Mwibara Constituency 1970 - 1975

# Deputy Minister of Agriculture 1972 - 1975

# Regional Commissioner Mara Region 1975 - 1982

# Minister Counselor at the Embassy of Tanzania, Washington, DC, USA - 1982 - 1985

# Member of Parliament - Bunda Constituency 1985 -1990

# Deputy Minister for Local Government 1987-1989

# Minister of Agriculture and Livestock Development 1989- 1990

# Regional Commissioner Coastal Region 1990 - 1991

# Member of Parliament - Bunda Constituency 1995 -1996

# Member of Parliament - Bunda Constituency 2005 -Present

# Minister for Water - Jan 2006 - Oct 2006

# Minister of Agriculture and Food Security - 2007 - Present


Education ya Wassira inaonyesha,mwanasiasa huyo ana shahada kama nne alizopata nchini Marekani

BA in Economics, American University in Washington, DC, USA.

BA in Political Science, American University in Washington, DC, USA.

MA in Economics, American University in Washington, DC, USA.

Masters in Public Administration, American University in Washington, DC, USA.



Mkuu Serengeti,

Ahsante sana mkuu kwa facts, ambazo kama kawaida ya JF huwa hazikosekani, ingawa tayari mkuu alishaanza kuhukumiwa kuwa hafai hana elimu, kumbe huyu ni nunda wa elimu na kichwa vile vile, maana huwezi kuwa na vitu vyote hivyo kwenye CV bila kichwa.

Heshima Mbele Mkuu, na endeleea kutuwekea vitu vya Mkulu Tyson, kumbe anafaa huyo! Na by the way hawa kina Wassira, ni majirani zangu kule Segerea nimejenga nyumba yangu karibu nao, kwa hiyo kuwa karibu na "Waziri Mkuu" itakuwa safi maana siwezi kukosa vya kutupiwa huko kwenye u-PM, unajua ujirani tena!
 
Ndugu wanabodi, bila kuona noma naomba mnisaidie kunipigia ndogo ndogo ili mkuu JK anichague mimi kuwa waziri mkuu wa TZ. Upuuzi wote huu unaondelea nitahakikisha wahusika wanakatwa vichwa mchana kweupe na itakuwa live kwenye TV. Na nitapangua baraza la mawaziri lote. Kila waziri nitakayempa wizara kwanza ni lazima atangaze mali zake zote mbele ya Watanzania wote (live TV) na pia atakayeshikwa wizi ama rushwa ni kukatwa kichwa tu hakuna cha kupelekana mahakamani kwani kupotezeana muda na kuingia hasara.
Nitaongea na serikali za kiarabu zinipe wakataji vichwa. Na kila aliwaye kuwa kiongozi ambaye tutamwona ana mali kuliko kipato chake cha halali tutamwomba atueleze kazipataje na kama maelezo hayaingii akilini basi kichwa chake ni mali ya taifa (Panga litafanya kazi)
 
Ndugu jamaa na marafiki wa JF. Siko hapa kupika majungu dhidi ya "Tyson" kama baadhi ya post hapo juu zinavyoashiria. Nina bahati ya kumfahamu "Tyson" binafsi kwa undani sana. Record niliyoweka hapo juu ni sahihi subject to minor errors katika baadhi ya miaka na majina ya Wizara alizoongoza.

Facts ambazo napenda nizirudie tena ni kuwa:
  • "Tyson" ana hamaki sana na anatunza visasi vya kisiasa kwa nguvu sana. Ni hamaki hii hii ndiyo iliyomfanya ampige mwandishi wa habari pale Maelezo na hapo kuanzisha jina la "Tyson."
  • "Tyson" ni mpiga kampeini mkubwa sana ambaye hutumia resources zozote alizonazo (hata za haramu) kujihakikishia ushindi. Ametumia uwezo wake huo katika chaguzi kadhaa ama zilizomhuhusu yeye mweyewe binafsi au mtu mwingine aliyempenda. Uwezo huo umekuwa unalipa au unabackfire; ulibackfire mara mbili: mwaka 1980 alipokuwa anampigia debe Meneja wa Mara Coops kwenye kinyanganyiro cha ubunge wa Musoma, na mwaka 1995 alipogombea ubunge dhidi ya Waryoba kwenye kiti cha Bunda.
  • Jina la "Tyson" lilianza mwaka 1996 wakati wa kesi ya Waryoba dhidi ya ushindi wake wa ubunge kutokana na kumpiga Mwandishi wa habari.
  • "Tyson" hana rekodi chafu za rushwa kama viongozi wengine walipo madarakani sasa hivi; ni kati ya viongozi wachache sana walio na rekodi safi sana. Hata hivyo miaka takriban 20 iliyopita alihusika na utoroshwaji wa majora ya vitenge kwenda Kenya kwa kutumia madaraka yake kama Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kuna sababu ya msingi kuhoji kuwa rekodi yake usafi kwa sasa hivi inawezekana inatokana na kuwa hajapata nafsi nyingine nzuri ya kufyonza. Nasema hivi kwa sababu ufisadi ni matokeo ya tabia mtu zaidi ya rekodi yake. Mwaka 1995 tuliuziwa Mkapa kuwa alikuwa na rekodi safi isiyokuwa na doa la rushwa, lakini kumbe alikuwa na tabia ya ufisadia ambayo alikuwa hajaipatia nafasi ya kuinyoesha.
  • Sikusema kuwa "Tyson" hakusoma; alimaliza darasa la nane kutoka Nyambitilwa Middle School na kuanza kazi serikalini hadi mwaka 1983. Kati ya 1983 na 1985 alipata digrii tatu; inawezekana kweli kuwa yeye ni genious sana anayeweza kuzikwapua haraka hivyo; hata hivyo sioni kosa kwa mtu kuhoji uhalali wa digrii hizo hasa kwa kiongozi ambaye historia yake inajulikana wazi vile katika mazingira haya ambayo kumekuwa na digirr nyingi za uzamili zenye mashaka. Taarifa za elimu yake nilitaja hapo juu aliziweka yeye mwenyewe kwenye maelezo yake binafsi kama mgombea ubunge mwaka 1970 na yale ya mwaka 1985. Hiyo record ya elimu yake mnayosoma pale pale Wikipedia haionyeshi ni lini alipata hizo digrii za American University at Washington DC; zilipatikana kati ya mwaka 1983 na 1985.
 
Kichuguu,
Mengi uliyosema kuhusu elimu na Tyson nakubaliana nawe. Mimi tulifahamiana alipokuwa mwanafunzi American University. Katika darasa la local government yeye alikuwa anatoa mifano hai kutokana na experience zake kama mkuu wa mkoa. Nina hakika aliondoka na A katika darasa hilo. You could tell the difference in his intellect after he graduated.
 
Unajua wakuu sometimes tunaongea kama vile tuko UK, eti bongo unahitaji nini kuwa waziri mkuu?

Usii-underate Bongo hivyo. Bongo tunahitaji PM au president mwenye maadili, busara, na usikivu. Tangu Sokoine alipotutoka, Tanzania hatujapata nafasi ya kupata kiongozi mwingine mwenye sifa hizo; hata Nyerere hakuwa nazo zote, alikosa usikivu. Tyson naye hana usikivu. Watu pekee waliobaki na sifa zilizo katika kiwango hicho ni Dr. SAS na Dr. JM.
 
Kichuguu,
Umetaja hasira za Tyson ukanikumbusha episode moja. Alipokuwa anasoma American U alikuwa pia akifanya kazi ubalozini. Wakati huo hakuwa na gari na kwa hivi watoto wake walikuwa wanapelekwa shule na gari la ubalozi. Siku moja Mariki alimkataza dreva asiwachukue watoto wa Tyson shule, ikabidi akodishe taxi kuwapeleka nyumbani. Kesho yake alipofika ubalozini alimshika shati Mariki karibia ampige konde ikabidi balozi Bomani aingilie kati. I hope ameshapunguza hasira.
 
Kichuguu,
Mengi uliyosema kuhusu elimu na Tyson nakubaliana nawe. Mimi tulifahamiana alipokuwa mwanafunzi American University. Katika darasa la local government yeye alikuwa anatoa mifano hai kutokana na experience zake kama mkuu wa mkoa. Nina hakika aliondoka na A katika darasa hilo. You could tell the difference in his intellect after he graduated.
Kwa hiyo aliondoka pale AU na digrii tatu katika kipindi hicho cha miaka isiyozidi mitatu? Yaani zile zilizokuwa zimeonyeshwa nyuma ya karatasi ya maelezo yake binafsi kwenye uchaguzi ubunge wa mwaka 1985. Kwa vile hadi mwaka 1989 nilikuwa na kopi za karatasi za chaguzi za bunge katika majimbo yote ya Mkoa wa Mara kuanzia Mwaka 1965 hadi mwaka huo 1985 (yale ya Nyumba na Jembe), niliona kabisa kuwa historia yake ilikuwa imepindishwa sana mwaka 1985.
Nimeendela kuhoji hilo hadi leo.

Kama Jasusi, ambaye ulikuwa naye darasa moja na ninakuamini sana hapa JF, ukinithibitishia kuwa kweli jamaa alikuwa genious kiasi kile cha kuondoka pale AU na digrii tatu wakati akiwa ofisa wa ubalozi, sitahoji elimu yake kabisa ingawa nitaendelea kuongelea temperament yake.
 
Kichuguu,

Fact zako zingine haziwi facts sababu ya serious contradiction: unasema Tyson ni Safi sana lakini anatumia Pesa Haramu kushinda Chaguzi mbali mbali..ni safi au sio safi (which is which)..Anarekodi safi lakini ana issue ya majora ya vitenge miaka 20 ilipita akiwa mkuu wa mkoa, CV yake inaonyesha contradiction alikuwa Naibu Waziri Local Govt miaka 20 sio RC-Mara. Makucha ya Vitenge MUTEX tu, mbona alikuwa position nyingi nyeti zenye pesa zaidi ya RC-Mara?...Watu wanasema hajawa na sifa ya Rushwa inayoweza kuwa proved ndio maana anasifiwa. Facts ziwe sahihi Mkuu.

Unaweza kuwa hatari na Visasi ukiwa hata Mbunge sio lazima PM..au Kwenye Kilimo kisasi kinapungua au hakiwezekani.. Jadili credible facts na credentials, tusiwe wepesi wa kusema jambo bila uthibitisho.

Mwanzo ulisema kuwa alijiita "Tyson", alafu sasa unasema alimpiga mwandishi ndiyo akapewa hilo Jina..alijiita au alipewa..(which is which?)

HIZI HAPA FACTS NYINGINE ZA KESI YA WARIOBA VS WASIRA

1996 hakuwa na kesi mbili, moja ya kupiga na ya uchaguzi, Ilikuwa 1 tu, ya Uchaguzi!!..alijiita Tyson 1996 likaendelea, Mwandishi alipigwa 1999..mida tofauti, unachanganya matukio tofauti

Kesi ya Mwandishi ilikuwa tofauti na Uchaguzi, mwaka 1999, na ulipatia ilikuwa solve nje ya court..alishaitwa Tyson, ungali Tyson maarufu, ila magazeti yaliongelea sana kesi sababu hakuwa CCM at the time..Opinion yangu he was a credible threat alivyokuwa upinzani in terms of Experience and Leadership nje ya system.

Jasusi yuko Sahihi kuhusu AU, Tyson alikuwa na familia yake yote akiwa Minister Couselor Ubalozini Washington, DC, ilikuwa kuanzia mwaka 1982 mpaka 1985...alipata Bachelor Degree mbili (in 3 years), na MPA 1985 mpaka 1986 (1 years0. (alikuwa USA for 4 years sio 2 years)..Yule mzee ni kichwa, a good communicator/campaigner, kasoma ukubwani, lakini kasoma Chuo cha Heshima, AU..

Alishinda uchaguzi Bunda mwaka 1985 akarudi Masomoni Marekani baada ya kushinda, na kuendelea masomoni kwa mwaka mmoja...Kawa deputy Minister Local 1987 baada ya kupata Master Public Administration American University... Na Uchaguzi wa Bunda 1990 alimuachia Jaji Waryoba aliyekuwa PM at the time na kumfanyia Kampeni..

These are facts...

Resume Hiyo Hapo

# Minister Counselor at the Embassy of Tanzania, Washington, DC, USA - 1982 - 1985
# Regional Commissioner Coastal Region 1990 - 1991

kati ya 1992-1995 alipata MA ECONOMICS American University tena

1995 alirudi na kumshinda Waryoba, akiwa na degree hiyo ya NNe ya uchumi, na baada ya huo Uchaguzi ndio Jina Tyson lilianza..
 
Serengeti,

Ngoja kwanza nifanye masahihisho katika matumizi yangu ya maneno fulani fulani ya kiswahili na typos kwa vile unayatumia kama utetezi:

(a) Niliposema "takriban miaka 20 iliyopita" nilifanya makosa. Lugha sahihi ilikuwa ni "takriban miaka 25 iliyopita;" hata hivyo nilikuwa nimesema kuwa ni wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, na nilishaonyesha time frame aliyokuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Situtegemea kuwa hiyo itakuwa ishu sana.

(b) Nimefanya makosa kusema "alijiita" halafu nikasema "alipewa" jina la Tyson; ukweli ni kuwa "alijiita" Tyson baada ya kusema kuwa anaweza kumpiga mwandishi yule kwa vile yeye ni kama Tyson. Hakuna aliyempa jina la "Tyson" ila alijiita mwenyewe. Ikumbukwe kuwa aliyekuwa Waziri mkuu wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995 alikuwa ni David Msuya na wala siyo Waryoba ambaye alishaishiwa madaraka kabisa ya kiserikali; nadhani alikuwa waziri wa aliyeshughulika na serikali za mitaa hivi. Kwa hiyo Waryoba hakuwa kigogo wa kusababisha umma wote ushangae eti kwa kushindwa uchaguzi na Wassira hadi hadi Wassira kuitwa "Tyson."

Sasa tuachane na wordsmith turudi kwenye facts:

(a) Niliposema usafi wa "Tyson" katika rushwa, nilisema in relative terms. Nimeweka wazi kabisa kuwa ni safi kulinganisha na wengine wote walioko Mdarakani; sikusema kuwa hana doa. Doa lake nimelitaja kuhusiana na majora ya MUTEX na kuweka shaka kuwa inawezekana usafi huu unatokana na kuwa hajapata nafasi nyingine ya kufyonza.

(b) Visasi na hamaki ni tabia za mtu ambazo hazitegemei madaraka yake. Kwa kawaida kama una hasira na hamaki wakati huna madaraka, basi ukishakuwa na madaraka hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa vile utataka mambo yote yafanyike kwa utashi wako tu.

(c) Mambo ya elimu ya Tyson pale AU kweli siyajui na ndiyo maana ninaya-question. Ninafahamu kuwa Mwaka 1970 alisema alikuwa amemaliza darasa la nane Nyambitilwa, halafu mwaka 1985 akasema amemaliza darasa la 12 Bwiru na kupata digrii tatu pale AU katika kipindi cha miaka miaka isiyozidi mitatu. Ninajua utaratibu wa elimu katika vyuo vikuu vingi sana hapa US na sehemu nyingine duniani; ndiyo maana nina shaka sana na digrii hizo. Kama kweli yeye ni kichwa hivyo basi ni bahati kwa Watanzania, lakini kumbuka kuwa amekuwapo kwenye system miaka yote hiyo na wala hatujaona matokeo ya kichwa hicho. Ingawa ninajua kuwa alikuwa akijitahidi sana kujiendeleza kielimu hata wakati akiwa Mkuu wa mkoa wa Mara ambapo alikuwa akifundishwa somo la English na mtu ambaye baada ya kuvurugana wakati kwa uchaguzi wa mwaka 1980 walishitakiana kwa Nyerere; "Tyson" hakuwa exceptional kiasi hicho.


===============================
NB:

Wakati Nyerere alipopigiwa kelele na wananchi wa Musoma kwenye mkutano wa hadhara pale Mkendo Shule ya Msingi mwaka 1982 wakimtaka "amwondoe mtu wake" Wassira, Nyerere hakumwondoa mara moja hadi ilipofika mwishoni mwa mwaka 1982 au mwanzoni mwa mwaka 1983, kwa hiyo haingewezekana Tyson aanze masomo pale AU mwaka huo huo wa 1982 hasa kwa vile bado hakukuwa na internet.
 
Kichuguu,
Umetaja hasira za Tyson ukanikumbusha episode moja. Alipokuwa anasoma American U alikuwa pia akifanya kazi ubalozini. Wakati huo hakuwa na gari na kwa hivi watoto wake walikuwa wanapelekwa shule na gari la ubalozi. Siku moja Mariki alimkataza dreva asiwachukue watoto wa Tyson shule, ikabidi akodishe taxi kuwapeleka nyumbani. Kesho yake alipofika ubalozini alimshika shati Mariki karibia ampige konde ikabidi balozi Bomani aingilie kati. I hope ameshapunguza hasira.


Hahaaaaaaaaaaa!! Mzee Jasusi na mwenzio ES mna matata sana,nway ni vizuri mnatupa historia interms of hadithi za hawa vijana wenzenu wa zama hizo na mambo yao, I remember for the first time I came closer to him 2004 pale UN hq za zamani Samora ,nilikuwa na shughuli zangu za kiofisi na ofisi mate wangu ambaye naye anatokea Bunda Mara,mwenzangu alionyesha mshtuko mkubwa sana ndipo nikabaini aah la kumbe ni mzee wa Bunda Wasira,he was tired kiuchumi lakini a very strong minded person,he talked to us very friendly pasipo hofu wala unyonge wowote.

Tulipoachana naye nilifurahishwa sana na jinsi alivyo,nikamuuliza mwenzangu imekuaje mzee na CCM tena? Akaniambia amerejea tayari na ninadhani 2005 atarudi bungeni kwani huyu ndio kipenzi chetu wana Bunda.

All in all kama binadamu ana mapungufu yake na pia mazuri yake ,the same formula iwe applied to Edward Ngoyai Lowasa,kama binadamu ana udhaifu wake na mazuri yake.

Mwacheni achape kazi hiyo ambayo hata miaka mitatu haijatimu,yanini kumuandama na kushawishi aondolewe?

Ni maoni yangu binafsi kwa kuzingatia ile dhana ya kila mtu anayo haki ya second chance to maintain .............

Mpeni muda afanye kweli .
 
Si mchezo amekula kuku since the 1970's mpaka leo. Sito shangaa nikiambiwa hana Investment yoyote ya maana na huko kwenye jimbo lake hakuna maendeleo yoyote ya yeye kujisifia nayo...kweli ukishajua siasa za CCM zinachezwa vipi...ni uongozi mpaka kufa (Wakenya hutumia sana ule msemo (political survivors) yani piga ua hawachomoki, hawa ndo wazee ukikaanae utake kuandika biography yake unaweza kuchanganyikiwa ili ku establish were exactly their political policies stand...kaaazzzz kweli kweli...

HUYU BWANA WASIRA NI MTU ANAESIMAMIA MAWAZO YAKE NA NDIO MAANA ATA ALIPOPISHANA UONGOZI WA CCM ALIVUKA MPAKA KWENDA UPINZANI.ANAAMINIWA WILAYANI KWAKE NA ATA UBUNGE ALIPITA BILA KUPINGWA.KUHUSU MAENDELEO NAPENDA KUKUMBUSHA KUWA WILAYA YA BUNDA ILIJENGA ZAHANATI KILA KATA TOKA MWAKA 2005,PIA WALIJENGA SHULE KILA KATA TOKA MWAKA 2005 WAKATI WATU WANAHANGAIKA KUJENGA SHULE YEYE TAYARI AMEJENGA NA YUKO ANAJITAHIDI KUZIHIMARISHA ZAIDI.KIWANGO CHA KUFAURU DARASA LA SABA BUNDA INAONGOZA MKOA WA MARA.
 
Nyongeza:

Wasira alisoma elimu ya secondary (Form 1-iv) kwa njia ya posta na kufanya mtihani wa form four wa baraza la mitihani la Tanzania katika kituo cha Bwiru kama private candidate. Hiyo inakubalika kabisa hapa tanzania na watu wengi wa Darasa la nane la mkoroni walifanya hivyo ili ku-upgrade elimu yao.
 
Mkuu FDR,

Heshima mbele mkuu, Tyson, ni jirani yangu tu sina umri wake wa kuwa intern naye mkuu maana usije ukaniletea noma hapa JF baadaye, nimejenga karibu sana na Clan yake, hapa Kinyerezi/Segerea, ndio maana ninasema ninasubiria tu akiula nimeula, maana siwezi kukosa ma-deal(joke)!

Anyways, kama ni uwezo huyo mkuu anao kuanzia kielimu mpaka kikazi, ninawashukuru JF kwa kunisafisha macho kwenye CV yake, sikujua kuwa CV yake ni nzito hivi, Mungu amsaidie maana nasikia ni kiongozi asyependa masihara bongo tumewahi kuongozwa mpaka na kina Kisoki, itakuwa Wassira!
 
kichuguu,masatu,serengeti,

..Mtu alikuwa na guts za kuiba wakati wa Mwalimu, sasa anataka kumjaribu wakati wa Kikwete? Hivi mnategemea mtasalimika nyie?

..Haikuiba wakati wa Mwinyi kwasababu hakuwekwa kwenye nafasi yenye ulaji.

..kama ni mtu wa hasira za kukunja watu mashati basi hatufai. hizi siyo zama za kukunjana mashati na kupigana kabari na ngwala.

..he is also too old, and doesnt seem to have new ideas. jamani toka 1974 uko kwenye uongozi tuuu, kana kwamba hakuna watu wengine.
 
jokaKuu,
Kama aliiba wakati wa Mwalimu mbona amekuwa hoi namna hiyo? Kuna wakati alinyanyaswa sana na biashara yake ya kuuza samaki nje ikabidi arudi CCM. Sidhani Wassira alikuwa mwizi.
 
Haya jamani sasa mnaposema Tyson kuwa waziri mkuu mna maana tayari kutoka vichwani mwenu hiyo CCM imeshashinda uchaguzi wa mwaka 2010?..
Mbona mnanikatisha tamaa jamani mweeee! si ndio haya tunayoyasema kila siku kuwa tumekuwa wazembe kufikiria nje ya CCM, yaani kweli tunaridhika na utumwa huu wa kutofikiri nje ya chama hiki?..
Huyo Tyson hata kama ni msafi tatizo sio usafi wa mtu mmoja ama wawili ndani ya chama kwani watu kama hao wapo CCM hivi sasa tunavyozungumza lakini ubavu wa kusema hawana kwa sababu ya matumbo yao. Mtu yeyote anayekubali kuinua mikono kukubali kushindwa na shetani wa siasa basi huyo sii kiongozi.
Nachotaka kuelewahuyo Tyson ataweza badilisha nini?.. na yuko wapi leo wakati usisadi huu umeshamiri mbona amekaa pembeni kimyaaa anakula bado meza moja na hao mafisadi?
 
Mkuu FDR,

Heshima mbele mkuu, Tyson, ni jirani yangu tu sina umri wake wa kuwa intern naye mkuu maana usije ukaniletea noma hapa JF baadaye, nimejenga karibu sana na Clan yake, hapa Kinyerezi/Segerea, ndio maana ninasema ninasubiria tu akiula nimeula, maana siwezi kukosa ma-deal(joke)!

Anyways, kama ni uwezo huyo mkuu anao kuanzia kielimu mpaka kikazi, ninawashukuru JF kwa kunisafisha macho kwenye CV yake, sikujua kuwa CV yake ni nzito hivi, Mungu amsaidie maana nasikia ni kiongozi asyependa masihara bongo tumewahi kuongozwa mpaka na kina Kisoki, itakuwa Wassira!

Mkuu Field Marshall,
Heshima mbele. Ningependa sana kupata historia fupi ya huyu Mhshimiwa Kisoki, kwani mzazi wangu (RIP) alishawahi kuwa kigogo wa sisiemu enzi za Mwalimu na alikuwa akimtajataja sana mheshimiwa huyu kwamba alikuwa naye katika siasa kwa muda mrefu enzi za utawala wa mwalimu Nyerere,sema tu mzee wangu (huenda na Kisoki pia) hakuwa "Mwerevu wa Wizi" kiasi kwamba hadi leo nisingekuwa masikini. Binafsi umri wangu sio mkubwa sana kumjua mheshimiwa huyu Kisoki. Hivyo basi naomba wewe ama mwana JF yoyote anipe mwanga kidogo.
Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom