Twite atua yanga, mamia wamlaki, simba hawakuonekana

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1][/h]
Twite baada ya kutua Uwanja wa ndege akiwa na viongozi wa Yanga
Shabiki wa Yanga Babu Ally, akiwa na jezi ya Rage na4
Twite akizungumza na Waandishi huku amevaa jezi namba 4 yenye jina Rage
Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Yanga, Francis Kifukwe kushoto akiwa Uwanja wa Ndege na kigogo wa Usajili, Seif Ahmad 'Magari'

Na Mahmoud Zubeiry


BEKI mpya wa Yanga, Mbuyu Twite ametua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo, kabla ya kupakiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.


Hakuna kiongozi yeyote wa Simba wala askari polisi aliyemsogelea kama ambavyo kulikuwa kuna tishio kwamba akitua tu beki huyo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watamkamata kwa tuhuma za kuwatapeli dola za Kimarekani 30,000.

Inadaiwa, kabla ya kusaini Yanga, Twite aliyekuwa akichezea APR ya Rwanda alisaini Simba na kuchukua dola 30,000.

Hata hivyo, baadaye mchezaji huyo alighairi na kuamua kwenda Yanga na kurudisha fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, ambazo zilikuwa zinammiliki kwa pamoja mchezaji huyo.

Lakini viongozi wa Simba waligoma kupokea fedha hizo ingawa viongozi wa APR na Lupopo walifika hadi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kuzikabidhi fedha hizo, ili Simba wakazichukulie hapo.


Twite aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa anakamilisha kuhama kwake rasmi na kuja kuanza maisha mapya Dar es Salaam,

Lakini upande wa pili, Simba SC waliamini beki huyo amekwepa kukamatwa kufuatia kuvuja kwa habari za mpango wa kumtegea akitua nchini wamkamate.

Ametua na amekwenda Jangwani, maana yake jaribio la kumkamata akitua limefeli na sasa tusubiri kama Simba watamuwekea mtego mwingine.


Chanzo: Binzubery blog
 
Nchi Yetu basi tu... Nyerere hakutupa TV na Mambo ya ANASA mapema... SISI tukaangukia kwenye MICHEZO; Angalia

tunavyopenda Mpira wa MIGUU Tuna MOYO HASWA... KENYA, UGANDA na NCHI zote za Afrika Mashariki wanaona

DONGE... Na hatufanyi vizuri saaaana...
 
timu yenye mwenyekiti mwanasiasa itaendeshwa kisiasa na timu ya mwenyekiti mfanyabiashra itaendeshwa kibiashara
 
hao polisi mbona wamemzunguka 2bila kumkamata,au hawna taarifa zake!!!
 
2meona wangapi??asamoah,mwape na wengne kbao wako wapi??yangu macho..sie ngoja 2jifue for champions league,nyie komaeni na twitta.
 
2meona wangapi??asamoah,mwape na wengne kbao wako wapi??yangu macho..sie ngoja 2jifue for champions league,nyie komaeni na twitta.

twite kafata kuchukua kombe la kagame hataki hadithi za champion league wakati hata kagame umebakiza historia tu.
 
Sawa mbuyu kaja Yanga mimi njaa yangu ni vikombe Afrika, lini tutabeba ushindi wa Afrika?
 
Mimi ni mshabiki wa yanga toka niko mdogo na nimefurahi huyu jamaa amesign for young africans the best team in east africa lakini kama jamaa kweli alisign for simba alafu akapewa hela zaidi akabadilisha mawazo then thats wrong kisheria anatakiwa ashtakiwe kwenye relevant football authorities., bt we know how the game is played in africa anyways
 
hivi Twite kwanini timu yake (Lumpopo FC) ilimpeleka APR kwa mkopo????, Yanga mtakuwa mmeuziwa Mbuzi kwenye Gunia: kama si swala la nidhamu mbovu basi nina wasiwasi na kiwango chake ......mh! yetu macho.
 
Huo wasiwasi wenu umeanza sasa hv baada ya Jamaa ku'sign Yanga, wkt Rage akichukua allowance na hela ya kupiga kambi kule Rwanda kumsainisha mlikuwa na uhakika na kiwango chake,si ndiyo?
Sasa nyie endeleeni kuwa na wasiwasi naye sisi we have no doubt kuhusiana na kipaji chake cha asili,labda muingize mambo yenu, we know the guy we have seen him playing in the Kagame competition, kwahiyo hatuna shaka naye.
 
''Anselm'' kumbuka kuna mtu anatamani msichana mara baada ya mwinzie kumu-approach, na tena yuko tayari kupandisha dau la kumpata ili nayeye aonekane hayuko nyuma; that is what happened on Twite's saga: Twite ni wakaida sana'' the rate of 30Millions was quite enough for him, but simply w'have administered and full up with hypocrisy not easy to realize and accept the truth..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom