Twamuomba Mengi arudi kwenye mapambano dhidi ya ufisadi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233

Baada ya Mengi kuwatosa wananchi wanyonge waliokuwa wanamuona ni alama (symbol) ya kupambana na mafisadi, hasa baada ya ujasiri wake wa kuwataja mafisadi papa, sasa wanyonge tutampata wapi mwingine kama yeye?

Kwa umiliki wake wa vyombo muhimu vya habari – radio, TV na magazeti – Mengi alikuwa ni mtu muafaka sana katika kazi hiyo, na wengi tuliona jinsi mafisadi walivyokuwa wakipata kiwewe kutoka kwake. Lakini ghafla ameamua kuwatosa, na vyombo vyake vya habari havigusii kabisa masuala ya ufisadi.

Alipowataja mafisadi papa, CCM na serikali yake walimpa msukosuko mkubwa sana lakini alipata faraja kutoka kwa wananchi ambao walikuwa nyuma yake. What went wrong?

Hata katika kipindi cha ITV cha mapitio ya magazeti, hayasomwi magazeti yale yenye habari kuu ukurasa wa mbele kama inahusu ufisadi wa viongozi wa chama tawala.

Tunajua yeye ni CCM na anapenda kuona chama hicho kinashinda – ingawa twashangaa ni kitu gani kinamfanya aamini kama CCM inaweza kupambana kweli na ufisadi, kama tunavyoona sasa hivi jinsi JK anavyowakumbatia waziwazi mafisadi.

Lakini kupambana katika vita vya haki ilipasa kuwa muongozo wake, hata kama vita hiyo ni ajenda kuu ya chama cha upinzani – Chadema. Kwa nini anawaona Chadema adui – na hivyo kuyatelekeza mapambano yenye lengo jema – na hivyo kuwatosa mashabiki wake?

Tunaomba Mzee Mengi ajifikirie tena kuhusu hili. Kuna hatari naye ataambiwa ni fisadi kama vile wale aliowatuhumu miaka miwili iliyopita.
 
hata mimi limenishangaza hilo hazungumzii kabisaaa ufisadi kuchagua viongozi waadilifu
 
kumuomba mengi kupambana si vizuri kwani mwanamapinduzi wa kweli haombwi bali hujitoa mhanga
 
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji wakweli wanaoumizwa na umasikini wa Watanzania, hivyo hupigania maslahi ya taifa.
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wachumia tumbo, wakiwemo baadhi ya wale makamanda, waliokuwa wanapigania nafsi zao.
Na kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji maslahi, miongoni mwao ni wafanya biashara, ambao wanapambana na ufisadi sio kwa chuki za ufisadi, bali kwa maslahi ya biashara zao. Hawa ndio hutaja majina ya watu, huku wakiisifia CCM na kuisuport kwa hali na mali.
 
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji wakweli wanaoumizwa na umasikini wa Watanzania, hivyo hupigania maslahi ya taifa.
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wachumia tumbo, wakiwemo baadhi ya wale makamanda,waliokuwa wanapigania nafsi zao.

Ndo maana daima namuunga mkono mzee Pengo , kadinali. aliposema kuwa kuna watu wanapiga kelele za ufisadi kwa kuwa wao wamekosa fursa za kufisadi katika serikali .
Pengo aliongea jambo ziito sana, ndo hawa Kina Mengi na makuwadi wenzao akina Sitta. woote ni Genge na Mafisadi, Huwezi kuupinga Ufisadi ukiwa ndani ya ccm, haiwezekani, ni unafiki, bora ukanyamaza kimya.
 
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji wakweli wanaoumizwa na umasikini wa Watanzania, hivyo hupigania maslahi ya taifa.
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wachumia tumbo, wakiwemo baadhi ya wale makamanda,waliokuwa wanapigania nafsi zao.
Na kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji maslahi, miongoni mwao ni wafanya biashara, ambao wanapambana na ufisadi sio kwa chuki za ufisadi, bali kwa maslahi ya biashara zao. Hawa ndio hutaja majina ya watu, huku wakiisifia CCM na kuisuport kwa hali na mali.
....Mpambanaji maslahi!
 
Mbona mi naye namwona fisadi tuu, uwekezaji wote huu si ufisadi? mimi siku zote huwa naamini msemo wa kiswahili usemao matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno. maneno ya watu majukwaani hayanitatizi kabisa.
 
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji wakweli wanaoumizwa na umasikini wa Watanzania, hivyo hupigania maslahi ya taifa.
Kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wachumia tumbo, wakiwemo baadhi ya wale makamanda, waliokuwa wanapigania nafsi zao.
Na kuna wapambanaji na ufisadi ambao ni wapambanaji maslahi, miongoni mwao ni wafanya biashara, ambao wanapambana na ufisadi sio kwa chuki za ufisadi, bali kwa maslahi ya biashara zao. Hawa ndio hutaja majina ya watu, huku wakiisifia CCM na kuisuport kwa hali na mali.

Wewe Pasco una kesi ya kujibu hapa JF, kuna wakati ulisema hivi:

Pasco said:
Kwanza hongera zako kushinda udiwani, pili hongera kwa Bashe kumshinda mpiganaji Seleli hata kama ni kwa kutumia masalia/mabaki ya Kagoda.

Wapenzi wa Selelii wasiwe na shaka, hata kama Bashe angeshinda kwa asilimia 99% na Selelii asilimia 01%, bado CCM itampitisha Selelii na kumtosa Bashe, kuna secret agreement kwa wabunge makamanda waliahidiwa kupitishwa no matter what, nao ndio wakakubali kuitosa CCJ.

Hivyo kama wana CCM wa Nzega, wanawakilisha wakazi wote wa Nzega, na chaguo lao ni Bashe, basi atakayekwenda upinzani na awe Bashe, asimame na Selelii kwenye sanduku la kura, hivyo Jimbo la Nzega tuanze kulihesabu upinzani.

Kama na kuchekelea ushindi, kambi ya Bashe, chekeni sana, mkisubiria panga la NEC na mtalia sana, piga ua CCM haiwatemi makamanda wake, almanusura waimege ikatike vipande viwili, wakakubali kuinusuru CCM, sasa ni zamu ya CCM kuwanusuru.

Bashe ajiandae kwa safari, the only choice ni Chadema, tatizo langu kwake ni jee Chadema itawakubali hawa makuwadi wa RA?. Jee itafungua milango yake kuwakaribisha nyoka?.

Mwito wangu kwa Chadema, acha milango wazi kwa yoyote ajaye bila kujali alikuwa akimtumikia nani, concetration yao kwa sasa, iwe ni idadi ya viti vingi bungeni.

Bado unasimamia analysis yako?
 
Taasisi isiyo ya kiserikali, hivi karibuni imelitaja gazeti la Mwananchi kuwa ndio Gazeti pekee lililoandika habari za kweli na za bila upendeleo. Huu ni moja ya ushaidi juu ya kutokuwepo kwa fairness katika kuripoti habari hasa nyakati hizi za kampeni.

Tatizo ni uwoga kwamba kama sinta kuwepo upande wao watanigeuka. lakini kwa kufanya hivyo ni kuwanyima fursa na Haki wananchi wa Tanzanaia, na pia ni kukiuka misingi ya kazi za kiuandishi wa habari ambayo husisitiza Fairness, Haki na Ukweli katika kuhabarisha.

Nashangaa ni kwanini mtu ujipendekeze! Huko nyuma aliwahi kulala mika sana amechezewa rafu katika kuinunua iliyokuwa inaitwa Kilimanjaro Hotel, na alilaumu vyombo vya habari kwa kupotosha umma kwa kutokuandika ukweli juu ya sakata lile. Leo ameshasahau.. ukweli hataki kuundika, amerudi kulekule alikokuwa anakupinga, huu ni unafiki katika media.
 
Mbona mi naye namwona fisadi tuu, uwekezaji wote huu si ufisadi? mimi siku zote huwa naamini msemo wa kiswahili usemao matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno. maneno ya watu majukwaani hayanitatizi kabisa.
Kwa definition yako ya ufisadi, wafanyabishara wote ni mafisadi?
 
Mnategemea MENGI awakubalie ombi lenu?
alipoonesha msimamo wake against mafisadi, serikali walipiga za utosi mpaka akawa anakosa za kulipia mshahara watu wake. ameamua kulegeza mkanda na anapiga hesabu zake vizuri ili oktoba atoke vipi.

Lakini ni huyu huyu aliyetuonesha picha za rwanda na burundi siku moja kabla ya kupiga kura mwaka 1995 ili tuuchukie upinzani. He is not in favor of sauti ya wengi he is in favor with making more cash and reputation
 
Mengi na ITV yake pamoja na magazeti yake ni wakuogopwa kama ukoma, anzeni kukumbuka sakata lake la uuzwaji wa Kilimanjaro Hotel jinsi alivyozidiwa kete halafu akapiga kelele saaaaaana watu tukamwonea huruma weeee kumbe mafisadi wenzie walimzidia kwa kuweka cha pembeni kwa dau kubwa kuliko lake, mzee mbaya sana yule jamani amulikwe sana ingawa anatumia media zake kujionyesha kuwa yu pamoja na walalahoi
 
baada ya mengi kuwatosa wananchi wanyonge waliokuwa wanamuona ni alama (symbol) ya kupambana na mafisadi, hasa baada ya ujasiri wake wa kuwataja mafisadi papa, sasa wanyonge tutampata wapi mwingine kama yeye?

kwa umiliki wake wa vyombo muhimu vya habari – radio, tv na magazeti – mengi alikuwa ni mtu muafaka sana katika kazi hiyo, na wengi tuliona jinsi mafisadi walivyokuwa wakipata kiwewe kutoka kwake. Lakini ghafla ameamua kuwatosa, na vyombo vyake vya habari havigusii kabisa masuala ya ufisadi.

alipowataja mafisadi papa, ccm na serikali yake walimpa msukosuko mkubwa sana lakini alipata faraja kutoka kwa wananchi ambao walikuwa nyuma yake. What went wrong?

hata katika kipindi cha itv cha mapitio ya magazeti, hayasomwi magazeti yale yenye habari kuu ukurasa wa mbele kama inahusu ufisadi wa viongozi wa chama tawala.

tunajua yeye ni ccm na anapenda kuona chama hicho kinashinda – ingawa twashangaa ni kitu gani kinamfanya aamini kama ccm inaweza kupambana kweli na ufisadi, kama tunavyoona sasa hivi jinsi jk anavyowakumbatia waziwazi mafisadi.

lakini kupambana katika vita vya haki ilipasa kuwa muongozo wake, hata kama vita hiyo ni ajenda kuu ya chama cha upinzani – chadema. Kwa nini anawaona chadema adui – na hivyo kuyatelekeza mapambano yenye lengo jema – na hivyo kuwatosa mashabiki wake?

tunaomba mzee mengi ajifikirie tena kuhusu hili. Kuna hatari naye ataambiwa ni fisadi kama vile wale aliowatuhumu miaka miwili iliyopita.

i wonder ni lini tutaachakunyosheana vidole na kuchukua hatua wenyewe,ni lini tutaacha laumiana na kusubiri mpaka mtu afanyekitu kwaajili ya ukombozi wetu wenyewe,you are likely sailing in the same boat with mengi cause what i see mengi si mwanamapinduzi wa kweli kama wewe ulivo na wengi kwenye jukwaa hili walivo maana daima tunaishia ongea tu na kutokuchukua hatua yoyote......mengi aliwataja mafisadi then what aliwapeleka mahakamani?hii ilitosha kuonesha kuwa si mwana mapinduzi huyu.its high time kwa kila mzalendo na mwana mapinduzi kusimama katika zamu yake mwenyewe.
I love tanzania!!!!!
 
Siku ile RA anajibu mapigo alitoa na ushahidi wa maandishi wa jinsi Mzee Mengi alivyo fisadi nyangumi na akawapa PCCB. Nini kilifuata?
 
By 2015. Hairuhusiwi m2 kumiliki vyombo vya habari zaidi ya kimoja. Mnalijua hili??
Nafikiri Kikwete akishinda itabidi huu mkakati ufutwe ili kumpa Favaour Mengi. Ni mwana ccm Mwenzetu na ametoa Mchango mkubwa sana katika kufanikisha ushindi wa JK.
Slaa akishinda watalia wengi!! Simaanishi wengi relative to TZ population, namaanisha wengi relative to Mafisadi Percentage.
 
naona mnadanganyana sana hapa....kwanza kabisa hii jamiiforum inaonekana ni ya chadema kila ukisoma ni hadithi za DK SLAA...hamna kingine...na mnafanya watu wapumbavu sana wakati dunia nzima inajua R.a. mengi chadema...kwenye msafara wa mamba na chadema wamo...hapa kwakweli haki haitendeki kila kitu kibaya mnachosema nyinyi ni ccm...mbona hamuyataji mazuri walioya fanya ccm?.naona hapa kinacho fanyika ni brainwashing..hahaha mtu mzima hatishiwi nyau...HATUDANGANYIKI...CCM OYEEE,KIKWETE OYEEE
 
Back
Top Bottom