Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Mwafrika wa Kike,
Nilichosema ni kwamba mpaka mtu anihakikishie kwamba hizo component zote zilikuwa sawa wakati huo... ndio naweza... ku-bai (buy) hizo tetesi zenu... kama sina hilo... siwezi -ku-buy ingawa ni posibility... tatizo lenu mnasema almost with authority kwamba kituo cha TBC1 kiliwafanyia hujuma... kama hakuna ushahidi hakuna haja ya kusema hivyo.
NB: Hakuna kitu kinaitwa TVT siku hizo... guys it is TBC
Asante kwa correction....I meant TBC,
Mkuu, umepata statement yoyote toka TBC inayosema kwa nini hawakuweza kurusha hii kitu live? Je hili jambo sio muhimu ya kulitolea maelezo.
Kasheshe,
Mimi na wewe wote tunajua spin kwa hiyo katika hili tunaweza hata kusema kuwa technician alipatwa na stroke... kwa vile ni Tanzania, hakuna mwenye kudai uthibitisho.
Mimi ninachosema ni kitu kimoja, whatever the reason, uamuzi wa kutorusha hotuba ya Slaa kwa TV zote mbili (kama ilivyoelezwa hapa) sio mzuri kisiasa na kiutendaji.
Ifikie wakati maslahi ya taifa yawe mbele zaidi ya masilahi ya vyama.