TV za dini kuanzishwa.Hii inaashiria nini?

Hivi Tanzania kuna tv station ya kiislamu? Nimeuliza tu ili nijue wakuu.

hawaihitaji, wao hutumia nguvu za ulinzi usioonekana. Supika iliyopandishwa juu ya alama ya nyota na mwezi inatosha, imani itasambaa tu.
 
hawaihitaji, wao hutumia nguvu za ulinzi usioonekana. Supika iliyopandishwa juu ya alama ya nyota na mwezi inatosha, imani itasambaa tu.

Posted via Mobile.....vipi foleni ya jangwani na magomeni imekuwa kubwa namna hiyo?
 
Mara nyingi hizi tv ni mahsusi kwa mijini tu ambako ndiko kwenye biashara kubwa kubwa. Vijinini haitalipa na kawaida mungu wa dini huangalia masilahi zaidi. Vijinini kuna nafsi nyingi lakini hazina uchumi kigezo ambacho kimemsababisha asiwekeze huko.
.

post zingine utadhani zinaandikwa na walevi wa gongo. Sasa vijijini kuna wenye tv wangapi? Na kama lengo lako ni kufikisha ujumbe kwa njia ya televisheni una invest vijijini ili iwe nini? Ujumbe wako utawafikia walengwa? Ndoi maana kuna redio station za FM za kidini kila mkoa ili kuwafikia hao wasio na uwezo wa kuwa na tv.
 
ndio maana tunasema umeme uende kijijini uone kama hawatanunua tv.tatizo kubwa kule ni umeme, vinginevyo wangekuwa na tv hata wao.
 
Hizi Tv za dini si za kibiashara nijuavo.ATN haitangazi biashara ni neno la Mungu waumini na watu wenye mapenzi mema ndo huchangia.TV Tunaini hivo hivo parokia zinachangia na waumini wake, Trenet hivo hivo zipo kueneza neno la Mungu zaidi.Sioni ubaya kwa wengine wakianzisha.Niwape tu kionjo cha WWW.CBN.COM hapo mtaona CBN news live na pia mtapata nyimbo za xmass radio for free hakuna kudownload wao pia inachangiwa na waumini.Ndugu zangu waislam sijaelewa hadi leo kwanini hawana TV wakati tunajua waumini wapo wengi wanaoweza kuchangia.Naona waamke sasa.HIzi TV zingine zitapata matanagzo ya biashara kama TBL nk watasonga mbele.
 
Leo nimeangalia kwenye taarifa ya habari channel ten kuwa kanisa la Mch. Rwakatare wanataka kuanzisha Television yao itakayoitwa Ebenezer Tv. Naona kila kanisa liko ize kuanzisha Tv kila kukicha, hii ina maana gani wanaJF, kwamba ndio tunakaibia mwisho wa dunia hivyo wanatumia kila njia kufikisha ujumbe ili baadae Mungu asiwalaumu aliowatuma kuongoza kondoo wake? Naomba majibu wanaJF...nawakilisha...

kueneza neno kwa mataifa yote
 
post zingine utadhani zinaandikwa na walevi wa gongo. Sasa vijijini kuna wenye tv wangapi? Na kama lengo lako ni kufikisha ujumbe kwa njia ya televisheni una invest vijijini ili iwe nini? Ujumbe wako utawafikia walengwa? Ndoi maana kuna redio station za FM za kidini kila mkoa ili kuwafikia hao wasio na uwezo wa kuwa na tv.

.
Na ile mikutano mikubwa ya wainjilisti wanaojiita wa kimataifa mbona haifanyiki vijijini? Takwimu ya taifa zinaonyesha asilimia 80 ya raia wake wapo vijijini. Jiulize kinacholengwa mijini ni wingi wa nafsi zitakazookolewa ama unono wa pato litakalopatikana? Nakubaliana na wewe kudhani kuwa naandika kama mlevi. Pombe yangu ninayolewa kila wakati ni ile divai waliyokuwa wamelewa kina Petro siku ya pentekoste. Hivyo wakati wowote ninapohisi mtu kuidhuru hiyo divai yangu na mafuta yake, nazungusha uzio(seng'enge) kwa sana.
.
 
Unajua kueneza injili sio swala la kueleweka.Bwana Yesu alisema enendeni kote ulimwenguni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu.

Hii ni biashara na Bwana Yesu sio na wanadamu.Kwa hiyo hapa unatakiwa uwe na akili pia uwe na ufahamu si kwa namna ya ulimwengu huu.Wengi huwekeza hazina zao hapa duniani lakini Bwana Yesu anakupa shauri kuwekeza kwake ambapo hakuna nondo wala mchwa wakula hazina yako.Na hazina yako inategemea unaiwekeza wapi.Kwenye mabenki au kule mbinguni.Hivyo ukipata ufahamu usio wa namna ya dunia hii utapata vision.Ni bora kuwekeza huko tunakotarajia kuweko milele na milele.Yaani mbinguni kwani yapo maisha baada ya kufa.

Hawa watumioshi wao wameamua kumkopesha Bwana Yesu na kuweka hazina yao katika benki ya mbinguni.Hivyo faida yao wataipata baadaye.Kwani unapofanya biashara na Bwana Yesu na ukawaleta wengi katika ufalme wake inamaana unawekeza kwake.Kama vile Hisa.Hivyo faida ya hao wanajituma kwa kufungua radio na televeni au lolote wanalolifanya ili wengine wasikie injili na kisha kuamua either kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wao,Hao ndio biashara .Na biashara hii ni nzuri sana kwani tunaahidiwa mafanikio mengi tukiwa hapa duniani lakini pia kule mbinguni .Neno la Mungu linasema ni heri kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na kisha anatuahidi kuwa na haya mengine atatuzidishia.

Mfalme Suleimani katika uhai wake yeye aliamua kufanya kazi na Mungu.Na hata alipoulizwa kuwa apewe nini yeye alichagua Hekima.JInsi ya kuwatawala wale watu aliokabidhiwa baada ya baba yake Daudi kufa.Sasa alipotafuta Hekima Mungu alimwongezea na utajiri ambao kwa wakati wake hakuna mtu aliyemzidi kwa hekima na utajiri ndio maana tukasoma kuwa hata malkia alitoka mbali sana kuja kuona hekima na utajiri wa suleimani.

Hata wakati huu ni muhimu sana kwa watawala wetu kutafuta hekima ili waongoze nchi kwa hekima ya kimungu vinginevyo tutawalaumu sana kwa vile wengi wanajitumainia nafsi zao na kukosa hekima ya kimungu.Pia sisi wana Jamii tunapaswa pia kuomba hekima ya kimungu ili maisha yetu yaendane na Mungu mwenyewe na usipokuwa na hekima ya kimungu huwezi hata kunielewa na utapingana na haya niliyoyaandika lakini namwomba Mungu akufunulie upate kuyaelewa haya na kuyatafakari.

TAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU na mengine yote utazidishiwa.Elimu ya dunia tuliyonayo mbele za Mungu ni UPUMBAVU mtupu kama huna NIA ya kumtafuta Mungu na unashindana na Maneno ya Mungu NA WATUMISHI WA MUNGU
 
Ndio maana yake............na huenda wanaanzisha TV stesheni ili kupunguza gharama za kurusha matangazo kwenye tv stesheni nyingine.

Kumiliki kituo cha redio au stesheni kuna gharama kubwa, kwani kuna malipo unayotakiwa ufanye kila baada ya miezi sita na gharama za kurusha matangazo katika kituo kingine kwa saa na kumiliki kituo chako moja kwa moja ni heri ununue muda kituo kingine. Sema kikubwa walichoona ni biashara, kuna fedha za matangazo hapo, tena mengi tu.
 
Kumiliki kituo cha redio au stesheni kuna gharama kubwa, kwani kuna malipo unayotakiwa ufanye kila baada ya miezi sita na gharama za kurusha matangazo katika kituo kingine kwa saa na kumiliki kituo chako moja kwa moja ni heri ununue muda kituo kingine. Sema kikubwa walichoona ni biashara, kuna fedha za matangazo hapo, tena mengi tu.

Ukiondoa ntn ni station gani ingine inamatangazo?
 
ndio maana nimesema hadi uwe na ufahamu wa kutosha hasa kwa namna ya roho na si kwa namna ya dunia hii.Ndipo utaelewa.Kufanya biashara ya matangazo sio msingi na huwezi kurusha kila tangazo.ni vigumu sana kurusha tangazo la TBL au Sigara ndugu yangu ni bora usiwe na hiyo TV kuliko kurusha matangazo kama hayo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom