Tv sibuka kuonyesha mechi za ligi ya uingereza na ujerumani live!

Apr 13, 2011
8
0
Kituo cha televisheni cha Sibuka kinachorusha matangazo yake kupitia Startimes kitakuwa kinarusha live mechi zilizobakia za Barclays Premiere League, UEFA na Bundasliga!! Habari hizo za uhakika zinatokana na mipango ya muda mrefu ya Kituo hicho kuwaburudisha na kuwapa wanacho kipenda watazamaji wake.

Wiki iliyopita walionyesha mechi mechi za Bundasliga pia wiki hii wameonyesha mechi za robo fainali za UEFA. Leo tusubiri, tuone Mechi za ligi ya Uingereza.
 
Ngoja niishi kwa matumaini kama Watanzania wengine!! Nakwenda kununua hicho king'amuzi chao angalau nione kama nitaona mechi ya Man U ikicheza na City leo!!
 
Mbona walisitisha vipindi vya dini lakini? They will be blessed if they continue to be attached with Religions hasa wakimtumainia Yesu kristo|
 
Sibuka mwish naangalia man u na man cty now, sijui wamepata wapi hk kibali.
 
Man City 1 Man United 0, city wako 11 uwanjani united wako 10 baada ya Scholes kulimwa kadi nyekundu!!! Sasa ni dakika ya 77 na mechi inaendelea kwenye TV sibuka
 
Ngoja niishi kwa matumaini kama Watanzania wengine!! Nakwenda kununua hicho king'amuzi chao angalau nione kama nitaona mechi ya Man U ikicheza na City leo!!

hii sio mechi ya ligi bosi, hii ni FA na jamaa sijaona kama kaorodhesha FA
 
Man City 1 Man United 0, city wako 11 uwanjani united wako 10 baada ya Scholes kulimwa kadi nyekundu!!! Sasa ni dakika ya 77 na mechi inaendelea kwenye TV sibuka

mi nilijua mbwembwe zako tu, dah asante sana itabidi tufanye mpango wa sibuka
 
Kama Sibuka TV wataendelea hivi, watakuwa ndio jibu la kiu zetu. Hongera Sibuka!
 
Back
Top Bottom