TV ipi nzuri? Sony, SamSung au Hisense ya Startimes?

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,224
Salaams WanaJF wote na wageni pia.

Ninapata kigugumizi kuhusu 'Review' za hizi TV kuhusu ubora wake na matatizo.

Kuna Hawa Sony ambao wametamba kwenye soko Muda Mrefu, Kuna Samsung ambao wanakuja juu katika soko sasa na kuna hawa STARTIMES Wamekuja na HISENSE TV.

Sasa Nauliza Kati ya Sony na Samsung ni ipi ina picha nzuri na sauti murua?

Technology ya kuunganisha. Je inawezekana kuunganisha TV ya Samsung na Radio ya Sony (DVD)? How?

tafadhali naomba mawazo yenu.
 
1. Samsung
2. LG
3. Sony na siku hizi wanauzia kwa sababu ya Brand

Lakini Watanzania wanakasumba ya Kununua brand sio ubora kwa hiyo endeleeni kupigwa
 
OK hapo nimepata idea.

Inawezekana brand ya TV fulani ilishika chat sana katika soko, ila ikitokea brand nyingine hata kama ina ubora kupita ile brand ya Mwanzo, watu inakuwa vigumu kuiamini.

OK utafiti unaendelea Men!!
 
Tatizo ni kwamba , brand fulani inaweza kuwa ni nzuri katika series fulani, watu waki ikimbilia, ufisadi una anza. Watu wanakwenda kuchakachua kwa umbo na application za vile vile kumbe ni boya la kubumba. Watu wakinunua na likianza kusumbua wanasusia brand nzima!

Kwa sasa ukitaka kununua kitu cha uhakika nenda kwenye maduka ya ma-argent wa hiyo brand, kwingine utaingizwa mkenge.

Kwa mtazamo wangu Sumsung ni kiboko wanaongoza kisha Sony na LG.
 
zamani kidogo kuna jirani yetu alikuwa ana TV inaitwa Grundig alitoka nayo ujerumani. dah brand hii naamin ukipata version yake ya kisasa ni balaa . Hata kabla home theatre azijaingia bongo jamaa alikuwa tayari anayo theatre ya TV yenye sauti nzuri na quality ya picha ilikuwa bomba.

Sijui kwa nini brand kama hizi hazipo bongo. labda wanajua bei yake hatuziwezi.
 
zamani kidogo kuna jirani yetu alikuwa ana TV inaitwa Grundig alitoka nayo ujerumani. dah brand naamin ukipata version yake ya sasa ni alaa . Hata kabla home theatre azijaigia bongo jamaa alikuwa tayari anayo theatre ya TV yenye sauti nzuri na quality ya picha ilikuwa bomba.

Sijui kwa nini brand kama hizi hazipo bongo. labda wanajua bei yake hatuziwezi.
grundig tv yangu ya kwanza baadae niliizoea basi naikorokochoa mwenyewe ikizingua na naiunga tena inadunda km kawa.katika tv hii ni jiwe
mkuu mpaka nilikuja kumpa mtu bure na nadhani anaitumia mpaka sasa.
 
grundig tv yangu ya kwanza baadae niliizoea basi naikorokochoa mwenyewe ikizingua na naiunga tena inadunda km kawa.katika tv hii ni jiwe
mkuu mpaka nilikuja kumpa mtu bure na nadhani anaitumia mpaka sasa.

Sony BRavia au LG Flatron.
 
samsung ni bomba asikuambie mtu,tech yao inatisha. wanatengeneza wao haiko under lisence.
 
Mpaka sasa nimezidi kushawishika na Samsung kutokana na comments za watu hapa.

Nimeona pia watu wengi wamenunua simu za Samsung na wanafurahia.

Sony Bravia ni nzuri ila kwa sasa bei ni juu.

Ila Samsung ni bei poa halafu zina ubora.

Pia Samsung wanazo friji na wanazo Redio.

Kwa hiyo nina mpango wa kununua Radio Kubwa ya Sony (3 cd) dvd na ninunue TV ya Samsung.

OK another Tech ni kuwa up to 2012, Radio na TV zote zinabadilishwa kuwa Digital, je TV na Radio zilizopo madukani zinaweza kupata digital transmission au itakuwa kwa haya matoleo ya zamani ya TV na Radio.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom