Tuzo ya Mwana JF anayepambana na Ufisadi kwa Dhati

Mimi nilikuwa na wazo dogo, kwa nini tusiwe na category kama tatu hivi

1. special talents, commitment on fight agaisnt corruption (Wazee wa nondo za maana)
2. Most commited reporters-Wenye kutumia resources zao to keep us informed on time
3.Member mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua maada na kumwaga point za maana on balanced basis

Tuzo, Tunaweza kuwapa kazi MOD wakaongea na asasi za kiraia and NGO'S ili waweze ku sponsor awards but JF itatoa certificates of apreciation
 
Mwanakijiji, you are being selfish here. Your uncomfortability should not override the wish of many who have decided to nominate you not necessarily for the award or recognition but as a symbol of appreciation of the good work that you have been doing.

Instead of being uncomfortable I would advice that you remain humble and keep doing the good work. You have dared and crossed the line which most dont cross so accept the appreciation.

The unsung heroes are not ignored. Through you they get what they deserve. They will definately see how good their work has been through you and others!

Let the votes flow in. Some other people may be nominated or mentioned. As for that allow it to go on!

I am nominating Gurudumu for only one reason i.e. his thoughfulness to start this thread and bring the idea forward which has helped contributors to nominate MwanaKijiji for his fantastic work in here. Mwanakijij deserves the nomination as rightly made by members.


Msando, naunga mkono mawazo yako kuhusu mwanakijiji lakini nikuombe gurudumu asiwe mmoja wa watakaopendekezwa kwa tuzo hii. Tuzo hii ni kwa ajili ya mpambanaji mahiri wa ufisadi kupitia JF. Gurudumu hana sifa hiyo kabisa. Samahani sikuisoma hii post jana.

Asante kwa kunielewa mkuu
 
Nilitahadharisha kwa mwelekeo huo huo wa Mzee Mwanakijiji kwamba zoezi la KUMTAWAZA MPAMBANAJI MASHUHURU dhidi ya Ufisadi na Mafisadi kwa hapa JF bora tukausitishe kwanza.

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba BADO TUPO KATIKATI ya vita hivi hivyo tukiaanza kupeana taji tungali bado tupo maeneo ya KAGERA na fisadi wetu kama alivyokua Nduli Iddi Amin mwenyewe bado yuko hai Kampala.

Hata kama tumewadhoofishwa kiasi gani, busara zinatuelekeza kwamba hawa MAADUI WA USTAWI WA TAIFA LETU mpaka pale tutakapowatia mikononi ndio watu tutaweza kutapisha juu hewani Shampen zetu lakini si kwa wakati huu. Endapo tutaendelea kulazimisha sana hili na basi tutambue kwamba MAFISADI NAO TUNAKESHA NAO HUMUHUMU - hakuna haja ya kuwatafutia wenzetu a POSSIBLE REST IN PEACE kwa bei rejareja kiasi hiki.

Unamuelekeza adui wako nguvu zako ziliko halafu baada ya hapo unategemea nini??? Haya mapambano tunayoyapigania leo hii, nionavyo mimi, wala si MCHEZO WA DENSI watu tukaanza mzaha mbele ya MAFISADI ambao kama tulivyo na uchungu na taifa, wao uchungu wao ni kung'olewa na ndio maana wanakesha nao kama sisi tuuuu, amkeni jaama!!!

Usiwape nguvu wasizo kuwa nazo. Hawana hizo nguvu pamoja na ufisadi wao. Narudia tena mauti na uzima uu mdomoni mwa mhusika, ukitishiwa nyau ukaingiwa hofu unawapa uwezo wa kutimiza kukiri kwako. Ukiamini na kusimama katika haki hata mawe yatakulinda kama wanadamu watashindwa.
 
Nyinyi hamnipendi nyinyi... wapo mashujaa ambao juu ya mabega yao sisi wengine tunasimama; mashujaa ambao hawatuzwi kwa nyimbo au ngoma; mashujaa ambao hawashangiliwi. Ni hawa ambao wako nyuma yetu sisi wengine. Ni wale ambao wako tayari kutudokeza ubovu, kutung'oneza chemba ili sisi wengine tuweze kuwa na ujasiri wa kuyasema hadharani yale tunayoyajua. Masuala yote ambayo tunafanikiwa kuyaleta hapa nyuma yake wapo mashujaa halisi ambapo pasi ya wao sisi wengine tungekuwa tunapiga makelele kama mavuvuzela yaliyotoboka.

Ni hawa ambao wanaitwa "the unsung heroes". Hawa ndio watu ambao kwa kiasi kikubwa na kwa namna ya pekee wamefanikisha mapambano haya hadi leo hii na wanaendelea kusimama kufichua ufisadi katika sehemu zao za kazi au wanaokutana nao. So... ukiniuliza mimi kura yangu inawaendea hawa mashujaa wasio na majina wala sura, ambao hata sauti zao sisi wengine hatuzijui lakini tunajua kuwa wapo.

Binafsi sistahili kuhesabiwa miongoni mwao kwani ninachofanya chaweza kabisa kufanywa na mtu yeyote akiamua tu kuvuka mstari wa woga na kutokujiamini. Nashukuru wale ambao wamenitaja lakini naomba tuwashukuru na kuwatuza hawa mashujaa wetu wasiotuzwa bado.
Kigezo peke yake kinachoweza kumpima mtu kama ni mpambananji dhidi ya uovu na ukandamizaji ni pale mtu huyu anapokosa mshipa wa wogana anakuwa tayari kusema chochote hata mbele ya muuaji wak. Tanzania tumefika hapa kwa sababu hatuna watu waliokatika mishipa ya woga.

Wapo wanaojaribu lakini baadaye huja kuwagundua kuwa hawawezi kuendelea na harakati zao wakiwa na njaa. Wanaposhikwa na njaa watu hawa huwa wapo tayari kugeuzwa kwa kupewa eti tu chakula. Tumewashuhudia watu waliojiita wanapanduzi lakini baadaye tumekuja kuwaona wakiingia kwenye kashfa ya kuhongwa na watawala na kuanza kulegeza misimamo yao na kwa maara nyingi wamejionyesha wazi kuwasaliti wenzao kwa singizia wamekua na wanfanya mambo kwa busara hivyo wanaweza kukaa tena hata na watu waliowapinga zamani wakaelewana ili hali watu hawa bado wanawanyonya watanzania.

Ni nani aweza kujiita mpambanaji akiwa na tabia hii ya kukosa consistance kwa sababu ya njaaa. Hawa ni watu wabaya kuliko hata wale ambao wameamua kuwanyonya waliowengi tangu mwanzo na kuendelea na msimammo yao. Wanamapinduzi uchwara tuwaogope kama ukoma na hakuna haja ya kuendelea kuwakumbatia, waende kwa wenzao tujue moja.

Tuzo ya uanamapinduzi ni lazima itolewe kwa mtu ambaye ameonyesha msimamo usiobadilika mpaka ukombozi unapatikana.
 
Mwanakijiji,
Unastahili tuzo na heshima hii. Unapambana sio humu JF pekee. Jiulize kwa nini mimi au mwanaJF mwingine hatutajwi! Tuambie tukusaidieje ili uendelee na kazi hii takatifu inayoweza kufanywa na wachache sana humu Tanzania. Hao wanaokupatia hizi taarifa wamekuamini sana kama ambavyo baadhi yetu humu tunakuamini.
 
Naona Mwanakijiji ameungwa mkono na wengi, mimi nikiwa mojawao. Sidhani hilo lina mjadala tena.

Lakini tutaomba mods watuambie ameungwa mkono na wachangiaji wangapi, just for record.

Pengine tujiulize kama ni yeye peke yake kafuzu hivyo vigezo kisha tuamue tena kama tuongeze idadi, jumla wawe wangapi?

Kisha tuamue tuzo yenyewe itaitajwa na ni nini?

Halafu tujiulize kama kutakuwepo na garama za kifedha, zitapatikanaje na nani atazitunza.
 
Mkulima Maskini Mwanakijiji (a.k.a Mzee Mwanakijiji) you are my idol, your are my champion. KEEP IT UP BRODA, I salute you!
 
Malaria sugu labda kama angepewa tuzo ya fisadi mkubwa na mtetezi wa mafisadi........ kisha nyingine angepewa mwiba na kibunango kwa utetezi wa ufisadi! Rest in havoc malaria sugu
 
Jamani tunapotaka kusifu mtu tumpe kwanza angalizo ili kumsifu kwetu kusimpore uwezo wake wa kufikiri na akili...waasisi wa harakati za kutoa elimu ya uraia kwa njia ya kusaidia udadisi wa fikra wasimamie tu mawazo yao mpaka demokrasia ya kweli itakapoanza kuota mizizi na kukomaa katika nchi
 
1.Mzee mwanakijiji
2.Dr.W.Slaa

These two make a good pair,i think conceptually what they do is like a team and its a winning team!
+ the others i don't know behind the scene
 
VIGEZO:

1. Anatupatia documents halisi za kadhia anayoichambua
2. Ameonesha upeo mpana wa kuchambua hoja
3. Amepigania hoja yake mfululizo muda mrefu bila kukata tamaa
4. Amekuwa akifanya extensive monitoring ya taarifa juu ya maendeleo ya hoja yake, na kutupatia updates on time
5. Hajajihusisha na matusi na kuchafua hali ya hewa hapa janvini
6. Hajawahi kupata bun
7. Vyombo vingine vya habari vimefaidi kutokana na uchambuzi wake na documents alizoleta janvini

jaribuni kuongeza au kurekebisha hizi

Mimi ningempa hii tuzo Invisible au Max Shimba. Kutupatia hii jamii forum mahali ambapo tunaweza kujadili na kupata taarifa za kuhusu huo Ufisadi. Huyo mwanakijiji amepata umaarufu au documents zake huwa zinatufikia kupitia hii jamii forum.

So wa kwanza kabisa kumtambua na kumpatia tuzo hii nafikiri awe Max Shimba. He is just extra ordinary, committed, patriotic, dedicated, ambitious and a truly Tanzanian.
 
Mimi ningempa hii tuzo Invisible au Max Shimba. Kutupatia hii jamii forum mahali ambapo tunaweza kujadili na kupata taarifa za kuhusu huo Ufisadi. Huyo mwanakijiji amepata umaarufu au documents zake huwa zinatufikia kupitia hii jamii forum.

So wa kwanza kabisa kumtambua na kumpatia tuzo hii nafikiri awe Max Shimba. He is just extra ordinary, committed, patriotic, dedicated, ambitious and a truly Tanzanian.

nakuunga mkono aisee! phew.. thanks.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom