Tuzo ya Mwana JF anayepambana na Ufisadi kwa Dhati

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
We need to reflect and recognize special talents, undetered committments, courage, and determination of a few of us in the fight against corruption in our country, by way of blogging. To start, and because of my recent addiction to JF, we may nominate and award one or two amongst JF members.

Kuna watu wachache wanapata kujulikana kama wapambanaji kwa sababu wanapata media coverage kutokana na nafasi zao za kisiasa. Lakini kuna wato wanablogu humu na vyombo vya habari havichukui habari zao na kuweka ukurasa wa kwanza na kusema fulani kasema kadha. Wenye nafasi wanatambuliwa na wananchi wa kawaida ambao hawana access na internet, na bloggers wanatambuliwa tu humu kwenye blogu.

Nina imani kwamba wengi wetu tutakubali kwamba kuna baadhi yetu humu JF wamefanya kazi kubwa sana, usiku na mchana kufichua na kuchokoza mijadala ya kadhia mbalimbali za ufisadi hapa nchini. Tutakubali pia kwamba hata taarifa nyingi zilizochapishwa kwenye vyombo vingine vya habari ama zimeanzia hapa JF au zilishika kasi zaidi hapa JF.

Pengine swali la kwanza litakuwa ni vigezo gani vitumike kumpata mshindi/washindi? Napendekeza kila mtu atoe maoni yake.

Swali la pili pengine litakuwa, pesa za kulipa tuzo zitatoka wapi? Hapa kuna option kadhaa. Ya kwanza ni kufikiri kitu chenye thamani ya pesa. Ya pili ni kufikiri kitu chenye kuonesha heshima tu kama cheti au hata press conference tu kumtangaza. Kila mtu awe huru kutoa maoni hapa.

Hii inaweza pia kupandisha heshima ya JF zaidi, pengine
 
Mmmm, mbona kimya jamani, au inamaanisha hakuna mwenye vigezo hapa JF?
 
Toa mapendekezo ya vigezo. Then sisi kama wadau tutatoa mawazo yetu.

Ila kwa wewe kutoweka vigezo vya kujadiliwa,inakua ngumu kwa wadau kuchangia. Ndo mana wako kimya.
 
Tunzo inaweza kusubiri kwanza, mtu havishwi taji eti kwa sababu tu anakaribia kumng'oa adui.

Bado tupo kati kati ya vita! Ufisadi TOKA Watanzania nasi tukapate maendeleo kama watoto wa wakubwa. Ufisadi toka ili uzalendo wa hiari urejee nchini na wimbo wa AMANI YETU NA UTULIVU kufuatia baadaye katika haki.

Hata hivyo, huko mbeleni ninamfikiria Mzee Mwanakijiji, Fareed na Candid Scope.
 
Mzee Mwanakijiji wins hands down. Sasa maadui wake namba moja EL na kundi lake la mafisadi wakiongozwa na aliyekuwa kiranja wao mkuu ambaye aliikimbia JF bila kuaga na kujaribu kurudi kwa mara ya pili wakati wa uchaguzi kwa jina alijiita M mmmmm cha mbuzi, vile vile adui mwingine bado yumo humu ambaye anampiga vita kali hata ukazuka ule msemo wa 'Wakishindwa hoja wanaleta viroja' wengine wanataka ujari lakini naona wamesingiziwa tu hawana ujasiri wowote ila ni kutaka popularity tu na kuwatumikia Mafia wao humu ndani kwa hoja ambazo hazina upeo.

Whether you like it or not ndege ya EL ilipaa na kuwaacha wabongo solemba. Mzee Mwanakijiji is right there at the very top. Hata Bunge la UK alipiga hodi.
 
Kura yangu inaelekea kwa Mwanaitelejensia na mtoto wa mkulima kutoka Shamba la Mwanakijiji:clap2:
 
Its a good idea but vigezo ni nini? Na nani anapiga kura? Mpaka sasa hivi umeshaona kuna kura imeharibika. Implementation may be a nightmare! And, most people in here are sleeping with anonymity in one bed! Winning will uplift their incognito status! Just food for thought!
 
VIGEZO:

1. Anatupatia documents halisi za kadhia anayoichambua
2. Ameonesha upeo mpana wa kuchambua hoja
3. Amepigania hoja yake mfululizo muda mrefu bila kukata tamaa
4. Amekuwa akifanya extensive monitoring ya taarifa juu ya maendeleo ya hoja yake, na kutupatia updates on time
5. Hajajihusisha na matusi na kuchafua hali ya hewa hapa janvini
6. Hajawahi kupata bun
7. Vyombo vingine vya habari vimefaidi kutokana na uchambuzi wake na documents alizoleta janvini

jaribuni kuongeza au kurekebisha hizi
 
Sijui ni sahihi kuomba Max au one of the Mods kusimamia hili zoezi?
 
VIGEZO:

1. Anatupatia documents halisi za kadhia anayoichambua
2. Ameonesha upeo mpana wa kuchambua hoja
3. Amepigania hoja yake mfululizo muda mrefu bila kukata tamaa
4. Amekuwa akifanya extensive monitoring ya taarifa juu ya maendeleo ya hoja yake, na kutupatia updates on time
5. Hajajihusisha na matusi na kuchafua hali ya hewa hapa janvini
6. Hajawahi kupata bun
7. Vyombo vingine vya habari vimefaidi kutokana na uchambuzi wake na documents alizoleta janvini

jaribuni kuongeza au kurekebisha hizi

Muzee ya Shamba... Mwanakijiji
 
VIGEZO:

1. Anatupatia documents halisi za kadhia anayoichambua
2. Ameonesha upeo mpana wa kuchambua hoja
3. Amepigania hoja yake mfululizo muda mrefu bila kukata tamaa
4. Amekuwa akifanya extensive monitoring ya taarifa juu ya maendeleo ya hoja yake, na kutupatia updates on time
5. Hajajihusisha na matusi na kuchafua hali ya hewa hapa janvini
6. Hajawahi kupata bun
7. Vyombo vingine vya habari vimefaidi kutokana na uchambuzi wake na documents alizoleta janvini

jaribuni kuongeza au kurekebisha hizi
Unamuongelea Mwanakijiji!!
 
Nyinyi hamnipendi nyinyi... wapo mashujaa ambao juu ya mabega yao sisi wengine tunasimama; mashujaa ambao hawatuzwi kwa nyimbo au ngoma; mashujaa ambao hawashangiliwi. Ni hawa ambao wako nyuma yetu sisi wengine. Ni wale ambao wako tayari kutudokeza ubovu, kutung'oneza chemba ili sisi wengine tuweze kuwa na ujasiri wa kuyasema hadharani yale tunayoyajua. Masuala yote ambayo tunafanikiwa kuyaleta hapa nyuma yake wapo mashujaa halisi ambapo pasi ya wao sisi wengine tungekuwa tunapiga makelele kama mavuvuzela yaliyotoboka.

Ni hawa ambao wanaitwa "the unsung heroes". Hawa ndio watu ambao kwa kiasi kikubwa na kwa namna ya pekee wamefanikisha mapambano haya hadi leo hii na wanaendelea kusimama kufichua ufisadi katika sehemu zao za kazi au wanaokutana nao. So... ukiniuliza mimi kura yangu inawaendea hawa mashujaa wasio na majina wala sura, ambao hata sauti zao sisi wengine hatuzijui lakini tunajua kuwa wapo.

Binafsi sistahili kuhesabiwa miongoni mwao kwani ninachofanya chaweza kabisa kufanywa na mtu yeyote akiamua tu kuvuka mstari wa woga na kutokujiamini. Nashukuru wale ambao wamenitaja lakini naomba tuwashukuru na kuwatuza hawa mashujaa wetu wasiotuzwa bado.
 
Mnisamehe sana wana JF, lakini taarifa zisizo za kiintelijensia zinaonesha mmiliki wa Dowans pia ni mwanachama wetu humu wa kila soku na mashuhuri kwelikweli kwa kujenga hoja.

Anatumia majina matatu tofauti ili kuweza kung'ata na kupuliza. Soma sana kwa makini kila kinachopostiwa humu halafu zungusha ubongo utamgundua.

Pointi hapa ni moja tuzo hii izingatie hili.
 
Back
Top Bottom