Tuzo ya MO Ibrahim yakosa tena Mshindi

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Tuzo ya Mo Ibrahim ambayo imekuwa ikitolewa kwa viongozi wastaafu wa kiafrika waliofanya vizuri katika Utawala bora kwa mara nyingine tena mwaka huu imekosa mshindi.

My Take
Je Afrika haina viongozi bora wastaafu, tutawezaje kupiga hatua kama viongozi wetu ni wa hovyo?au vigezo vya kumpata mshindi ni vigumu?
 
Mo Ibrahim aanzishe tuzo ya "Vasco Da Gama" i.e Rais wa afrika aliyefanya ziara nyingi za kimataifa. Ili nasisi TZ tuweze kupata hiyo tuzo.
 
Kama wastaafu hakuna aliye bora na hao ndo kidogo walionekana kuunza maadili basi itakuwa ngumu kuwapata washindi manake hawa tulo nao madarakani ni bure kabisa!
 
Watapataje washindi iwapo viongozi hawataki kuondoka madarakani hadi waondolewe kwa kugongwa kwa tindo? Yaani kufia juu ya kidonda? Na akigongwa kwa tindo, basi ha-qualify kupata tuzo.

Watapataje tuzo iwapo hata pale viongozi wakiondoka madarakani basi huhakikisha vyama vyao vinabakia? Mi naona kamati ya Tuzo ya Mo Ibrahim ibadilishe kanuni ili kuwapa hata wale waliokufa (posthumously) (eg Mwl Nyerere, Samora na Augustino Neto, Thomas Sankara, Murtaka Muhammed) au hata walio hai bado lakini walistaafu miaka mingi nyuma kama vile Mzee Mandela, Jerry Rawlings na Kenneth Kaunda.
 
Anachofanya MO Ibrahim na wasaidizi wake kina Salim Ahmed Salim ni mchezo fulani wa kurudisha pesa badala ya kumpa hata kilaza bora. Janja ya nyani kwisa jua.
 
Tuzo ya Mo Ibrahim ambayo imekuwa ikitolewa kwa viongozi wastaafu wa kiafrika waliofanya vizuri katika Utawala bora kwa mara nyingine tena mwaka huu imekosa mshindi.

My Take
Je Afrika haina viongozi bora wastaafu, tutawezaje kupiga hatua kama viongozi wetu ni wa hovyo?au vigezo vya kumpata mshindi ni vigumu?

angekabidhiwa mama maria nyerere kwa niaba.
 
Angalia marais wote wastaafu ambao hawajapata hiyo then uone kama hata kuna mmoja andeserve hiyo,all of them are rotten...
 
Anachofanya MO Ibrahim na wasaidizi wake kina Salim Ahmed Salim ni mchezo fulani wa kurudisha pesa badala ya kumpa hata kilaza bora. Janja ya nyani kwisa jua.

arushaone,,,,,kama wewe ni mfuatiliaj wa siasa za afrika unadhan nani unahis ali-deserve???huko hakuna kuchakachua,,,,,
ila ntaishangaa kamat ya tuzo endapo mwaka 2016(panapo majaaliwa) itampa JK
 
Back
Top Bottom