Tuzo ya MO Ibrahim yakosa mshindi.

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,102
53,351
Mwaka huu hakuna mshindi wa
tuzo ya Mo Ibrahim ambayo
hutolewa kwa viongozi wa Afrika
walioonyesha uongozi bora
Tuzo hiyo ya dola milioni tatu
nukta mbili, hutolewa kwa
kiongozi wa Afrika
aliyechaguliwa kwa njia ya
demokrasia na ambaye
aliimarisha hali ya maisha ya
wananchi wake na kisha
kuondoka ofisini kwa khiari.
Kamati iliyokutana kumteua
mshindi iliafikiana kuwa hakuna
kiongozi aliyetimiza matakwa
yote yaliyohitajika kuweza kuwa
mshindi wa tuzo hiyo.
Mwaka jana Rais wa Cape Verde
Pedro Verona Pires ndiye
alishinda tuzo hiyo.
Aliongoza vita dhidi ya watawala
wa kikoloni wa Ureno , aliongoza
siasa za vyama vingi na kusifiwa
kwa kuimarisha maisha ya
wananchi wake.
Tuzo hiyo hutolewa katika
kipindi cha miaka kumi na
mshindi hupokea dola laki mbili
kila mwaka maishani mwake.
Akitangaza uamuzi huo, Ibrahim
alisema "mtu hutandika
anapotaka kulala. Ikiwa lengo
letu ni kutoa tuzo kwa uongozi
bora, lazima tutii vigezo vyetu
wenyewe. Hatuwezi kujihujumu
wenyewe''
''Sisi hatupo kwenye biashara ya
kutoa ujumbe mzuri usio na
manufaa, ikiwa tutafanya
kinyume na kazi yetu, basi
tutapoteza ushawishi wetu.
Kamati ya tuzo hiyo ilitizama
baadhi ya washidani lakini
hakuna aliyetimiza matakwa yetu
yote. '' alisema mwanachama wa
kamati ya tuzo hiyo, Salim Ahmed
Salim.
Washindi wengine wawili, katika
miaka sita tangu kuzinduliwa
kwa tuzo hiyo, walikuwa marais
wa Botswana Festus Mogae na
aliyekuwa Rais wa Msumbiji
Joaquim Chissano.
Mapema mwezi huu wakfu wa
Mo Ibrahim ulimtuza tuzo
maalum ya dola milioni moja,
Askofu mstaafu wa Afrika Kusini
Desmond Tutu kwa kupigania
haki za wananchi wa Afrika
Kusini.
 
Back
Top Bottom