Tuzo ya Forbes ni Uongo, wapotoshaji wakamatwe na kufikishwa mahakamani

Lazima tuhakukishe vyombo vya habar viatuandika vizuri-serikali ya kidikteta.
 
dah kama magazeti ya callibre ya citizen na mwananchi yanaweza ku run story bila kuangalia autheticity yake basi tena kwa kweli,nitaendelea kusoma daily mail Uk ,guardian na the telegraphy online .
 
Nianze kwa kuonesha masikitiko yangu kuhusu mjadala unaoendelea kuhusu mambo ya Forbes 'kumshindanisha' Rais Magufuli. I see it very cheap kumzungumzia na kumhusisha Rais wa Tanzania na masuala ya Forbes. Forbes ni nini katika level ya Urais?

Rais wa Tanzania ni sawa na Rais, kiongozi, au mfalme wa nchi yoyote ile duniani. Ni mtu wa hadhi ya juu. Kubishania kama Rais anashindanishwa kwenye Forbes au la ni kumkosea adabu Rais wetu. Ni kumtweza. Yeye si mfanyabiashara au msanii au mwanariadha wa kuwekwa au kutowekwa kwenye Forbes. Leo nalazimika kuwa mkali.

Rais Magufuli si mtu wa mchezomchezo. Ni mamlaka kuu nchini. Tumkosoe kwa kumuimarisha ili atende vyema. Lakini, tusimshushe sana hadi level za vijarida na vimitandao kama Forbes. Anastahili makubwa zaidi.

Tumsaidie rais wetu kwa kumpongeza, kumkosoa, kumshauri na kumuombea. Hatupaswi kumpenda au kumponda kwakuwa yumo au hayumo kwenye Forbes and the like. Rais wetu ni nembo yetu, dira yetu, alama yetu na kioo chetu kama nchi. Hata kejeli za Eric Omondi wa Kenya katika 'How to be Magufuli' ni za kuzipuuza na kuzilaani.

Rais wetu azungumziwe kwenye level za kimaendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. 'Tu-deal' naye katika hayo. Ndiyo maana tunamuomba na kumkosoa apunguze ubabe na kuruhusu demokrasia kwakuwa hakuna ustawi wa nchii bila demokrasia. Forbes si level ya Rais wetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Ninaunga mkono hoja. Ninashangaa gazeti la uhuru kushupalia habari hizo ukurasa wake wa kwanza!
 
Tuhuma hizi ni sehemu ya anti-intellectualism movement ambayo kwa namna flani imejitokeza kuwa kama mbadala wa ajenda muhimu ya kupinga ufisadi, iliyoisaidia sana Chadema kuonekana sauti ya wanyonge na mbadala halisi wa chama tawala CCM, kabla ya chama hicho kikuu cha upinzani kuachana na ajenda hiyo kwa sababu ambazo sote twazifahamu.

Mie sina tatizo na watu kutoa maoni yao kuhusu kiongozi wao, iwe kumsifia au kumkosoa. Lakini katika kufanya hivyo, ni vema tukazingatia kuweka mbele ukweli kuliko kutunga uongo. Madhara ya uongo yapo wazi: kupoteza kuaminika katika macho ya jamii.

Tuanze na madai kuwa hakuna Forbes Africa iliyotangaza tuzo hiyo. Hivi kweli kulikuwa na ugumu gani kutumia Google search kubaini kama kitu hicho kipo au la? Lakini wa kulaumiwa zaidi sio aliyezusha tuhuma hizi bali wote walioamini kabla ya kujiridhisha.

Tuzo za Forbes Person of the Year zimekuwepo kwa miaka minne sasa, na huu ni mwaka wa tano. Orodha ya washindi wa tuzo hiyo ni kama ifuatavyo
2011: Mshindi wa kwanza zilipoanzishwa mwaka huo alikuwa Sanusi Lamido Sanusi (aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria)
Screenshot_2016-10-26-19-29-16-1.png


2012: mshindi alikuwa James Mwangi (Afisa Mtendaji Mkuu wa Equity Bank Kenya).
Screenshot_2016-10-26-19-29-35-1.png


2013: mshindi alikuwa Akinwumi Adesina (aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini, na sasa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika).
Screenshot_2016-10-26-19-29-57-1.png



2014: mshindi alikuwa Aliko Dangote (Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni Ya Dangote, Nigeria).
Screenshot_2016-10-26-19-30-13-1.png




2015: mshindi alikuwa Mtanzania mwenzetu, kijana bilionea Mohammed Dewji (Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya METL).

Screenshot_2016-10-26-19-30-27-1.png


Seriously, wanaotoa tuhuma hizo wanajifanya kusahau jinsi Mo alivyomwagiwa pongezi lukuki baada ya kuibuka mshindi kwenye tuzo hizo?

Bwana Yericko Nyerere anadai kuwa Tuzo hizo ziliandaliwa Lumumba. Mwaka huu 2016 au tangu tuzo zilipoanzishwa mwaka 2011? Na je mwaka jana Mtanzania Mo aliposhinda ni kazi ya Lumumba pia au kuna kingine?

Kuhusu tuzo za mwaka huu, Rais Magufuli sio 'mgombea' pekee. Idadi kamili ya wanaowania tuzo hiyo ni hii hapa chini

Rais Ameenah Gurib wa Mauritius
Screenshot_2016-10-26-19-40-44-1.png


Rais John Magufuli wa Tanzania
Screenshot_2016-10-26-19-40-49-1.png


Wananchi wa Rwanda
Screenshot_2016-10-26-19-40-55-1.png


Mwendesha Mashtaka Mkuu nchini Afrika ya Kusini Thuli Madonsela
Screenshot_2016-10-26-19-40-40-1.png


Mwanzilishi wa Capitex Bank Michiel Leroux
Screenshot_2016-10-26-19-40-36-1.png



Hivi inaingia akilini kwamba 'watu wa Lumumba' wameweza kuwashawishi VIPs hao waliotajwa hapo juu kuwemo kwenye kundi la wanaowania tuzo hiyo, kwa minajili tu ya 'kumnadi Magufuli.'?

Kuthibitisha kuwa waliotoa tuhuma hizo wana upungufu mkubwa katika kuhakiki tovuti, wamekimbilia kudai www.poy2016.com ni 'magumashi' bila hata kufanya "whois lookup." Data zipo pichani na nitazieleza chini ya picha
Screenshot_2016-10-26-19-45-35-1.png


Vitu vya kuzingatia katika whois lookup hiyo ni jina SID WAHI na CNBC AFRICA. Pichani chini ni sehemu ya wasifu wa huyo bwana
Screenshot_2016-10-27-01-14-57-1.png


Kwa lugha nyepesi, familia ya Wahi ni wamiliki wa Kundi la Makampuni ya ABN ambayo ni wanahisa waanzilishi wa CNBC AFRICA na FORBES AFRICA. Sasa hii sio kitu ngumu kama sayansi ya roketi au operesheni ya ubongo: aliyesajili www.poy2016, pia alisajili www.poy2015.com, www.poy2014.com, kwa rekodi fupi.

Na kilichopo kwenye tovuti ya www.poy2016.com ni kama inavyoonekana pichani

Screenshot_2016-10-27-01-33-34-1.png


Sawa, kwa minajili ya mjadala tu, basi tuseme 'watu wa Lumumba' walianza kuhangaikia suala hili tangu mwaka 2011 (ilhali by then, possible candidate wa CCM 2015 was Lowassa...kabla upepo haujabadilika). Lakini inawezekana kweli kwa 'watu wa Lumumba' kuihadaa hata BBC Swahili ambao nao wameweka habari hii kwenye mtandao wao?


Screenshot_2016-10-26-19-24-30-1.png


Kama nilivyoeleza awali, ni haki ya kila Mtanzania kumkosoa Rais Magufuli (kama ilivyo haki kupongeza pia). Hata hivyo, haki hiyo inaambatana na wajibu, na wajibu huo ni kuwa na hakika katika criticisms au pongezi zetu.
Umekurupuka.. Sio kwamba tuzo hazipo lla nominations mnazozipigia kura ni uongo
 
Sasa tunakoelekea tutaanza kuwashindanisha viongoz na kina Diamond plutnumz na Kiba..

Kama hii habari ina ukweli...
 
Nishampigia kura tena Rais wangu. Go go JPM...

OK, Let's assume kuwa this is true na Rais JPM ndiyo ameshinda, hiyo zawadi itatolewa nchi gani na watatumia LUGHA GANI kutoa hiyo tuzo?
Nina mashaka sana jamaa huenda akaingia mitini na kumtuma mwakilishi wake kati ya aidha Mabalaa bin Majaliwa au Samia Suluhishi au Mafiga wa Agostili kuficha udhaifu wake!
Mimi naomba tu siku ya Kutoa AWARD kuwe na mahojiano maalumu kati ya JPM na Media za kimataifa kwa KIINGEREZA, nasistiza tena in ENGLISH kupima kama kweli huyu mtu alipaswa kuwa AFRICA PERSON OF THE YEAR 2016!!!!!!!
 
mleta mada embu google Forbes Africa...ujua ulichoongea ni matapishi matupu na uache kudanganya watu kwa faida ya nani!? au ulitaka awe lowassa!?
 
Back
Top Bottom