Tuzo ya Forbes Africa ni ya kweli watu wenye nia mbaya wanataka kupotosha

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,831
Kwanza kabisa kuna thread imewekwa hapa ikidai kuwa tuzo hizo ni za uongo. Huyo mtu analengo la kupotosha watu.

Nitajikita kitaalam zaidi.
Kuna kitu kinaitwa whois ambacho hutoa details za domain. Hebu check hapa
Whois poy2016.com
Utakuta hiyo domain imesajiriwa na Sid Wahi na email yake ipo pale.

Sid wahi ni nani?
Taarifa zake hizi hapa
Contributors: Sid Wahi - CNBC Africa

Yaani ni mmoja wa shareholders wa ForbesAfrica.

Ndugu zangu tuache propaganda za kitoto. Ni ujinga sana watu wazima wanajaribu kupotosha kwa siasa za maji taka. Namuomba Jericko Nyerere aache utoto haujengi katika nchi ya wastaarabu.

==================

Na Rashid Chilumba

Kijana mmoja anayejiita Yericko Nyerere ameandika maandiko mfululizo ya kichekesho hivi Leo kuhusu kuwemo Rais John Magufuli kwenye kinyanganyiro cha mtu mashuhuri Africa kwa mwaka 2016.

Kwanza Kutwa nzima alianza kwa kuupamba ukurasa wake wa Facebook kwa viandiko vya kijinga kuwa Hawezi kumpigia kura Rais Magufuli kwenye shindano hilo la mtu mashuhuri kwa madai anapambanishwa na watu wenye hadhi ndogo hivyo ni tuzo hiyo inamdhalilisha Rais.

Muda si mrefu akageuka ghafla, amekuja na andiko jipya linalodai kuwa hata hilo shindano ambalo Rais Magufuli ametangazwa kuwania tuzo halipo na halijawahi kuwepo bali taarifa hizo za shindano ni za kuunga unga. Upuuzi.

Andiko hili jipya siyo tu linadhihirisha Ujinga uliotukuka na wivu mkubwa walionao Wakosoaji wa Rais Magufuli Kama Yericko Nyerere bali ni ishara kuwa wakosoaji hawa sasa wana MSONGO mkubwa wa mawazo juu ya mafanikio ya Ndugu Rais

Jambo hili linaweza Kuwaua haraka kabla hata ya siku ambazo Mungu amewaandikia kuishi duniani.

Yaan Yericko baada ya kuona andiko lake la Mwanzo la kebehi na Istizahi la kuwataka watu wasimpigie kura Rais Magufuli kwa sababu za kijinga limekosa mashiko kwa umma sasa ameamua kujipa kazi ya kulifuta kabisa shindano lenyewe kwa kudai halipo na halijawahi kuwepo. Huu ni Upuuzi wa kiwango cha Uprofessa.

Sikuwa na Mpango kabisa wa kuandika chochote kuhusu maandiko ya Yericko, niliamua Kumpuuza, lakini nimegundua ujinga wa Yericko unaweza kuambukizwa. Ni vyema kumrudisha shule.

Hivyo andiko hili linalenga kumrudisha Yericko Nyerere darasa la sita B shule ya Msingi Naminywili Mkuranga ili ajifunze upya.

Tuingie darasani.

[HASHTAG]#Kwanza[/HASHTAG] tuzo la mtu mashuhuri wa mwaka barani Africa ni nini? (What is Forbes Africa Person of the Year?)

[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG]:

Tuzo ya Forbes kwa mtu mashuhuri wa mwaka Africa ni miongoni mwa tuzo nyingi zinazotolewa kikanda na Jarida mashuhuri duniani la Forbes kwa mtu fulani ambaye ametoa mchango wowote katika kanda aliyopo.

Tuzo Kama hizo hutolewa pia na Forbes barani Asia na America kila mwaka.

[HASHTAG]#Tuzo[/HASHTAG] hii ipo na ilianzishwa lini?

[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG]:

Tuzo hii ipo na ilianzishwa rasmi mwaka 2012 kwa lengo la kumtunuku mwafrika yeyote aliyekuwa na ushawishi mkubwa hasa katika eneo la biashara na uchumi kila mwaka.

Watu walioteuliwa hushindanishwa kwa kupigiwa kura na mshindi ni Yule aliyejikingia wingi mkubwa wa kura na hupewa tuzo katika dhifa rasmi inayoandaliwa katika Mji wowote miongoni mwa Miji katika nchi za Africa. Mwaka huu itatolewa mwezi Novemba Mjini Nairobi.

[HASHTAG]#Swali[/HASHTAG]

Waafrika gani wamewahi kushinda tuzo Hii katika Miaka iliyopita?

[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG]

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 waafrika kadhaa wameshinda tuzo Hii ya Forbes. Orodha yao ni kama ifuatavyo:

1. 2012 winner – James Mwangi, CEO of Equity Bank, Kenya

2. 2013 winner – Akinwumi Adesina, the then Minister of Agriculture in Nigeria, now head of the African Development Bank.

3. 2014 – Aliko Dangote, Chairman and CEO of the Dangote Group, Nigeria.

4. 2015 – Mohammed Dewji, CEO of MeTL Group, Tanzania

[HASHTAG]#Swali[/HASHTAG]

Je ni watu wadogo ndo hushindanishwa?

[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG]

Huu ni ujinga mwingine wa Yericko Nyerere ambao ni lazima afundishwe kuuepuka.

Tuzo hiyo inayo sifa za kuwashindanisha watu mashuhuri kuliko tuzo nyingine yoyote barani Africa ukiondoa ile ya Marais wastaafu ya MO Ibrahim.

Mfano:

Mshindi wa mwaka Jana wa tuzo Hii Mtanzania MO Dewji alichuana na kuwabwaga watu wafuatao:

- Nkosazana Dlamini Zuma Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika,

- Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

- Na Arumna Oteh makamu wa Rais wa Benki ya Dunia.

Si hivyo tu, Rais Magufuli anachuana mwaka huu pamoja na watu wengi, yumo Rais wa Mauritius na taifa zima la Rwanda (Yaan nchi nzima ya Rwanda)anachuana nayo halafu Useme tuzo huhusisha watu wadogo?

Maneno hayo hutamka ikiwa tu hukupata chanjo za kifaduro, pepopunda, unyafuzi na dondakoo wakati wa utoto wako.

Maelezo hapo juu siyo tu yanajibu Hoja za kichekesho za Yericko bali pia yanaonesha ujinga na wivu usio Msingi kutoka kwa Wakosoaji wa Rais Magufuli Kama Yericko .

[HASHTAG]#Mwisho[/HASHTAG]

Tunajua Yericko Nyerere hajawahi kumpenda Rais Magufuli na kwa jinsi alivyo haiwezi kutokea ammpende maana huenda rizki zake nyingi zimebanwa na Ndugu Rais.

Lakini muhimu zaidi katika hili ni Kumtaka Kuacha kusema uongo hata kwa mambo yenye ukweli kwa sababu za kijinga na wivu.

Watanzania wengi kwa mujibu wa takwimu wana imani na Rais Magufuli, wataendelea kupiga kura na kwa mwendo ulivyo atashinda tuzo hiyo.

Hivyo Hakuna haja ya watu wa aina ya Yericko kunena uongo kupata umaarufu au kumdhoofisha Rais.

Hila na ghiliba za aina hiyo zimepitwa na wakati na ni Upumbavu mkubwa.

Ikiwa mtu humpendi na huwezi kusema mazuri yake Kama yalivyo ni bora kukaa kimya. Maana lifa na fila havitangamani.

POVU LA NINI?

Ili kuondoa ujinga kichwani tembelea viungo tovuti (links) hizo hapo chini usome na Upige kura.

https://www.google.com/amp/www.forbes.com/sites/mfonobongnsehe/2015/12/03/tanzanias-richest-man-mohammed-dewji-is-forbes-africas-man-of-the-year/amp/?client=ms-android-tecno

Forbes Africa Person of the Year 2016 nominees: 2 presidents, 2 South Africans, 1 country | Africanews
 
post: 18229936 said:
Kwanza kabisa kuna thread imewekwa hapa ikidai kuwa tuzo hizo ni za uongo. Huyo mtu analengo la kupotosha watu.

Nitajikita kitaalam zaidi.
Kuna kitu kinaitwa whois ambacho hutoa details za domain. Hebu check hapa
Whois poy2016.com
Utakuta hiyo domain imesajiriwa na Sid Wahi na email yake ipo pale.

Sid wahi ni nani?
Taarifa zake hizi hapa
Contributors: Sid Wahi - CNBC Africa

Yaani ni mmoja wa shareholders wa ForbesAfrica.

Ndugu zangu tuache propaganda za kitoto. Ni ujinga sana watu wazima wanajaribu kupotosha kwa siasa za maji taka. Namuomba Jericko Nyerere aache utoto haujengi katika nchi ya wastaarabu.
Hakuna chochote. Tangu lini Forbes Africa wakawatumia Shareholders wake kumsaidia kazi? Ok,mbona taarifa zozote za Forbes Africa hazijawahi kutolewa na Sid Wahi?
 
Hao ni vijana wa mzee mamvi...hawana lolote na ni 3% tu..
 
Hakuna chochote. Tangu lini Forbes Africa wakawatumia Shareholders wake kumsaidia kazi? Ok,mbona taarifa zozote za Forbes Africa hazijawahi kutolewa na Sid Wahi?
Tatizo lako ni ufinyu wa exposure ndio inakusumbua.
Kwani shareholder hawezi kuajiriwa na kampuni?

Nimekupatia link ifuatilie acha kulia lia kama huna akili nzuri.
Jitahidi kujielimisha kidogo na uache uzuzu.
 
Siyo vizuri katika jamii inayoelekea kustaarabika. Watu wa nchi zingine wanatuona wapuuzi kama yeye. Anatakiwa abadilike aache kwenda kwa mihemuko.

Kuna watu wangapi sasa amewapotosha?
Siyo vizuri kuandika uongo.
Huyo nimeshaamua kumpotezea muda mrefu uliopita. Yaani sijui alipoteleaga wapi leo hii kaibuka na vijistori visivyo na mbele wala nyuma. Halafu makamanda wanammwagia sifa kwa "uwezo" wake wa kijasusi. Ha ha ha, duniani kuna watu.
 
So what is the movie behind the scene series?
After all kama ni mimi ningekataa kushirikishwa.. .. Acheni kufanya mzaha na issue ya urais nyie.. It is the top job in the world, ...yeye Maguful calibre yake huwezi linganisha na hao wasiofahamika, eti people of Rwanda...
BTW, hiyo tuzo ina faida gani hasa kipindi hiki? Et Forbes Africa...
Zaid ya hapo, hao hao tuliokataa demokrasia yao na misaada yao, leo ndio tunalilia watupe tuzo..... Really?
Mlishajiuliza kwanin kuna Forbes person of the year na Forbes Africa person of the year?
Tusiendeshwe hivyo jamani... Dah..si bora haya mambo tuwaachie tu TWAWEZA?
 
So what is the movie behind the scene series?
After all kama ni mimi ningekataa kushirikishwa.. .. Acheni kufanya mzaha na issue ya urais nyie.. It is the top job in the world, ...yeye Maguful calibre yake sio hao wasiofahamika, eti people of Rwanda...
BTW, hiyo tuzo ina faida gani hasa kipindi hiki? Et Forbes Africa... Tusiendeshwe hivyo jamani... Dah..si bora haya mambo tuwaachie tu TWAWEZA?
Acha kulia lia wewe.
 
Kwanza kabisa kuna thread imewekwa hapa ikidai kuwa tuzo hizo ni za uongo. Huyo mtu analengo la kupotosha watu.

Nitajikita kitaalam zaidi.
Kuna kitu kinaitwa whois ambacho hutoa details za domain. Hebu check hapa
Whois poy2016.com
Utakuta hiyo domain imesajiriwa na Sid Wahi na email yake ipo pale.

Sid wahi ni nani?
Taarifa zake hizi hapa
Contributors: Sid Wahi - CNBC Africa

Yaani ni mmoja wa shareholders wa ForbesAfrica.

Ndugu zangu tuache propaganda za kitoto. Ni ujinga sana watu wazima wanajaribu kupotosha kwa siasa za maji taka. Namuomba Jericko Nyerere aache utoto haujengi katika nchi ya wastaarabu.
Sasa ndio umekanusha kitu gani, nani kasema tuzo za Forbes siyo za kweli? uongo unaosemwa ni shindano hilo kwa sasa halipo.
 
Mimi nasubiri nione mwisho wa hii movie maana naona mapicha picha tu.
 
Rais wa nchi anashindanishwa na wauza karanga wa nchi nyingine hlf mnashangilia anaongoza?! Kapimweni akili zenu nyie kama ziko sawa...... Angepambanishwa na marais kama Uhuru Kenyetta, Buhari, Santos n.k, lkn siyo watu wasiojulikana kwa lolote, rais wa nchi anadhalilika mnashangilia?!
 
Acha ujinga wewe Malcolm X feki. Rais wa Mauritius Ameenah Gurib ni muuza karanga? Aliko Dangote aliyewahi kushinda hiyo tuzo ni muuza karanga? Wewe kaa hapo hapo ufipa na roho yako ya korosho. Ulie tu.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom