Avocado
Member
- Aug 23, 2010
- 97
- 4
Namekuwa nikifuatilia sana vyombo vya habari na hii ni mara ya pili katika kipindi kisicho pungua mwaka mmoja nimesikia Tanzania ikitunukiwa TUZO kwenye nyanja za ELIMU na AFYA,kwa kweli nimeakuwa na mashaka sana juu ya hao wanao toa, na wanaopokea hizo TUZO kwa kweli sijui vinatumika vigezo gani kupewa TUZO hizo,ukiangalia jinsi waziri wa mambo ya nje Mh Membe anavyokuwa kifua mbele kuzizungumzia TUZO hizo utadhani kuna kitu kikubwa sana kimefanyika hapa Tanzania,wiki mbili zilizopita kulikuwa na taarifa kuwa dawa mseto za malaria zimeadimika nchini na ilisemekana kuwa kuna vigogo wameziuza nje ya nchi,na uhaba huo wa dawa pia waziri alikiri kuwa upo, lakini akajitetea kuwa bajeti ni kidogo ! Na akasema wanahitaji kama dola milioni mia tano($500M.) kupitia bajeti ijayo ili kupata dawa za kutosha, Malaria ni ugonjwa unaua zaidi kuliko magonjwa mengi,na kwa kifupi hili ni janga na janga ni vita, je tutahitaji kusubiri bajeti ijayo kuingia vitani ? Wakati tunaisubiri bajeti hiyo maisha ya watanzania wakawaida hasa vijijini tunayaweka wapi ? Mimi nilidhani JK alipozindua kwa mbwembwe ile kampeni ya MALARIA HAIKUBALIKI alikuwa amejipanga ! Kumbe hata dawa hakujua zipo au hazipo !!
Hili la TUZO ya ELIMU ambayo Tanzania aliipata mwaka jana sijaelewa vizuri naomba wadau mnisaidie, ilikuwa ni TUZO ya uwingi wa majengo ya shule au ubora wa taaluma ? na kwanini pia tukubali kupewa TUZO ambazo hazina Tija ?Kuna sifa gani kupewa TUZO ya kuandikisha wanafunzi wengi halafu mwisho wa siku wote wanafeli ? Hebu angalieni matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010 ni AIBU napenda kumshauri aliyepokea ile TUZO ya ELIMU airudishe alikoitoa ''we don't deserve that shit '' ! Na hiyo ya MALARIA pia wairudishe,vingozi wetu wanafanya propaganda huko nje ya nchi ili kukidhi matakwa yao ya kiutawala na kuwapendezesha hao wafadhili huko nje lakini hali halisi ni kinyume kabisa hapa nchini,hakuna haja ya kuwaonyesha jirani zako kuwa wewe na familia yako mna Good time kumbe njaa kali ,ni heri ieleweke mna njaa ili msaidiwe kwa hali na mali. Viongozi wetu waache kupenda sifa za kimataifa wakati kitaifa hali ni mbaya. Unasifiwa kuwa umezaa watoto wengi unafurahi na unachukua zawadi,jiulize mwisho wa siku, inakuwaje ?
Mungu tusaidiae !!