Nakubaliana na wale wanaosema isiitwe majina ya Wanasiasa. Wazo langu tuzo zinaweza kuwa na majina ya vivutio vyetu vya utalii. Hii itasaidia kutangaza vivutio vyetu vya utalii ndani na nje ya nchi.
Hapa kuna mfano yaweza itwa Serengeti (mbuga), Ngorongoro (mbuga), manyara (mbuga), Mikumi (mbuga) nk, ama yaweza itwa Amboni (machimbo ya kitalii), Mlingotini (eneo la utalii Bagamoyo), Kilwa (sehemu ya utalii). Pia tunaweza kutumia kutangaza maziwa, mfano Ziwa Victoria, Rukwa, Nyasa (tena hili ni muhimu manake wamalawi wanasema mpaka na TZ ni mwisho wa maji, na huliita Ziwa Malawi), Tanganyika, Singida, Kindai nk. Tunaweza kutangaza mito yetu kama Mara, Kagera, Ruvuma nk.