Tuyavumilie mabalaa na mateso yote haya kwa kuwa tulimwasi Mungu

mangifera

Member
Oct 15, 2011
47
34
Wandugu, katika utawala wa CCM awamu ya nne, Mungu alituinulia watu miongoni mwetu akatuonyesha jinsi serikali ya CCM inavyotenda maovu, akatuonyesha ufisadi mkubwa kama wa EPA, Meremeta radar nk. Katika ufisadi ule hakuna aliyekana kuhusika ikwemo serikali yenyewe.
Cha kushangaza wezi walewale wakaja kutuomba watuongoze(kipindi hiki cha pili), wakaja na khanga, wali, tshirt na kofia. Mwisho wa siku tukaamua kuwachagua wezi watuongoze. Kitendo hiki kilimkasirisha sana Mungu wetu, aliyekuwa ametuwekea kila kitu tuamue. Baada ya hapo akaamua kuondoka maana hatukumtii. Wezi tuliochagua ni wa shetani, wala si wa Mungu.
Na hizi ndizo ishara za kuachwa na Mungu: Mabalaa mengi kama ajali za majini, angani na nchi kavu, njaa, kukosa huduma muhimu kama mahospitalini, umeme, maji na nyingine nyingi. Hata wana wa Israeli kipimo chao cha kumkosea Mungu ni adhabu na mabalaa makubwa, hadi walipotubu na kumwangukia tena.
Kwa Mawazo yangu ni kuwa Mungu ameondoka ameenda Rwanda. Hili ndilo taifa lililotubu baada ya mabalaa makubwa. Na sasa ameifanya Rwanda kuwa taifa la mfano ulimwenguni.
Kwa hiyo tuyavumilie,tuliyataka wenyewe, tunahitaji toba ya kweli, ikiwemo kuwaondoa viongozi na chama hiki dhaifu na kumtii Mungu kwa kuchagua viongozi waadilifu.
Vinginevyo taifa litaangamia.
 
Umenena ukweli sana ndugu ila we subiri wale watumwa wa kuzimu waje uone watakavokuwa wanakubeza hapa! Tanzania tuko mbali sana na uwepo wa Mungu, wale wa rohoni wanaelewa what imean
 
Uko sahihi kabisa, mimi jana nilishangaa kusikia eti ndege ya ATC imevunjika kioo cha dirisha ikiwa angani halafu mchana nasikia meli imezama, halafu jioni nasikia spika kakataa kuahirisha bunge halafu leo nikasikia eti mwenye meli hana ofisi alikuwa anatumia mawakala.Ama kweli tumemuasi mungu cha moto tutakiona hadi tuikatae CCM
 
Hakuna aliewachagua CCM ! Kwani WaTz wote wakiikataa kwa kupitia kisanduku cha kura ,bado CCMwanaibuka washindi na wanawapiga watu changa la macho kwa kuwapa ubunge wawatakao tumeona.
 
Ninaamini kuwa ni Watanzania wapuuzi wachache walioshiriki kugeuza matokeo ya kweli kuwa ya uongo na uongo huo ukawapa ushindi wa kidhaifu viongozi wezi wa CCM.Kosa letu tunalolikosea mbele za Mungu ni kuomba Haki badala ya Kudai haki,kwani hata vitabu vya dini vimeleza wazi kuwa Haki HUDAIWA,Haki HAIOMBWI,na unapodai haki unakua tayari kwa lolote.Watanzania tumeka mazuzu ktk kudai haki hata kama tunajua hii ni haki yetu bado tunakua waoga kudai haki.Kama tungekua hatutaki utani,leo hii spika makinda angetakiwa kuwa amejiuzuru,leo hii viongoz wote wezi wangekua wamefirisiwa.Lakini bado najipa matumaini kuwa MATESO YAKIZIDI UJUE SAA YA WOKOVU IMEKALIBIA,Mungu ibariki Tanzania,poleni wahanganga wote wa ajali ya meli
 
Uko sahihi kabisa, mimi jana nilishangaa kusikia eti ndege ya ATC imevunjika kioo cha dirisha ikiwa angani halafu mchana nasikia meli imezama, halafu jioni nasikia spika kakataa kuahirisha bunge halafu leo nikasikia eti mwenye meli hana ofisi alikuwa anatumia mawakala.Ama kweli tumemuasi mungu cha moto tutakiona hadi tuikatae CCM

imekaa pouwa sana hii, 100% tru
 
Back
Top Bottom