Elections 2010 Tuweke bayana idadi ya wliojiandikisha kupiga kura Vyuo Vikuu

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,690
20,445
Nimegundua moja ya mbinu za kuiba kura inaweza kuwa ni ile ya kutumia advantage ya kura zisizopigwa vituoni. Kutokana na idadi kubwa ya wanavyuo wa Higher Learning Institutions kuwa katika uwezekano mkubwa wa kutopiga kura, kuna possibility wezi wa kura wakatumia nafasi hiyo kuweka kura zao kwani idadi ya waliopiga kura haitakuwa katika tishio la kuzidi idadi ya waliojiandikisha. Kwa maana hiyo tunaweza kutrace possibility ya wizi iwapo difference itakuwa ndogo wakati katika hali ya kawaida difference inatakiwa iwe kubwa kwani wengi hawatapiga kura. Kwa kuanzia, naweka idadi ya wapiga kura waliojiandikisha katika baadhi ya vituo vya kura vya UDSM:


  1. Utawala-1 : watu 497
  2. Utawala-2 : watu 497
  3. Utawala-3 : watu 497
  4. Utawala-4 : watu 497
  5. Utawala-5 : watu 497
  6. Utawala-6 : watu 472

Eneo la Cafeteria:


  1. DARUSO-1 : watu 468
  2. DARUSO-2 : watu 468
  3. DARUSO-3 : watu 468
  4. DARUSO-4 : watu 468
  5. DARUSO-5 : watu 468
  6. DARUSO-6 : watu 468
  7. DARUSO-7 : watu 468

Baadaye nitarudi kuongeza vituo zaidi vya Chuo Kikuu UDSM katika maeneo yaliyosalia ya Shule ya Msingi Mlimani. Naombeni wengine wanaoweza kupita maeneo ya vyuo vikuu waweke idadi ya waliojiandikisha hapa.
 
Back
Top Bottom