Tuwe wakweli: Tatizo La Zanzibar sio Muungano, ni Udini

Status
Not open for further replies.
namuunga mkono huyu aliyesema wamekuja kivingine, kama wanataka uvunjike kwa nini tuwalazimishe vunja tupa kule.

Umenikumbusha juu ya waraka wa kichochezi juzi hapo Unguja- "hatuwataki Wapemba," "hatuitaki SUK," "Tunataka Muungano wa serikali mbili, lakini Pemba isiwepo".
 
Sio kweli Mkiristu kwenye BLM ni Mwakanjuki pekee, alishakuwepo John Okello, Isack Sepetu na kuna wakristu wengi tuu wenye majina ya Kiislamu.

Hata kina Wolfgang Dourado, Agustino Ramadhani, Charles Hillary etc ni Wakristo Wanzanzibari!.

Kanisa lilianzia Zanzibar na Bagamoyo kufuatia kupigwa marufuku biashara ya utumwa. Soko lilikuwa Bagamoyo na Zanzibar, Kanisa liliwalipia fidia watumwa ili kuwagomboa na ndio Wakristu wa kwanza!.

Kiukweli udini halihawahi kuwa tatizo Zanzibar!.

Mkuu Pasco nimependa mchango wako wa ujenzi kwa taifa letu.
 
Viongozi wetu hawatuambii ukweli kwamba tatizo la zanzibar sio kero za Muungano, ni ubaguzi wa kidini. Viongozi wanafanya hivyo kwa makusudi wakidhani kwamba wakieleza ukweli wataamsha chuki za kidini. Mimi ni muumini wa ukweli maana maandiko yananiambia "ukweli utaniweka huru". Ukiondoa Bri. Gen. Adam Mwakanjuki ambaye pia ana asili ya uislamu, hakuna Mkristo aliye shika nafasi ya juu katika SMZ na mpaka sasa SUK (sERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA).

hata ukijiuliza maswali mawili madogo utapata jibu.
Mosi: Kwanini harakari za "kupinga muungano" ziendeshwe na kikundi cha kidini JUMIKI (Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu?

Pili: Kwanini harakati hizo ziambatane na kuchoma makanisa na magari ya wachungaji? Ni Misikiti mingapi imechomwa?

Ni wazi kwamba muungano umepoteza maana kwa sasa, lakini tatizo sio muungano, ni udini. Kwa Zanzibar, Mtu yeyote anayetoka bara wanamchukulia kama Mkristu na ni adui.

Nilikua Z'bar siku 3 zilizopita, nilipata taarifa kwamba mjumbe mmoja wa baraza la wawakilishi alipokua akichangia hoja na Mhe. Jussa Ladhu kuhusu sehemu ya bahari ya zanzibar kufanywa ya muungano na Mhe. Tibaijuka alitumia maneno "Tusipokuwa makini na mambo haya tunaweza kujikuta WAKRISTU toka bara wanakuja kututawala!"

Inasemekana ndo sababu Rais wa Z'bar Dr. Shein anakuwa mzito kuchukua hatua kwa ghasia za namna hii maana naye ni mdini.

Nawasilisha.

Okay. Uislam ndio unawatuma hivyo, je ni nani wa kulaumiwa? CCM au Wazanzibar? Walipokuwa wakichoma Makanisa siku zilizopita serikali ya mapinduzi Zenji ilikuwa inachekelea tu!!! Na haya ndio madhara yake wala wasilalamike.
 
Viongozi wetu hawatuambii ukweli kwamba tatizo la Zanzibar sio kero za Muungano, ni ubaguzi wa kidini. Viongozi wanafanya hivyo kwa makusudi wakidhani kwamba wakieleza ukweli wataamsha chuki za kidini. Mimi ni muumini wa ukweli maana maandiko yananiambia "ukweli utaniweka huru".

Ukiondoa Bri. Gen. Adam Mwakanjuki ambaye pia ana asili ya uislamu, hakuna Mkristo aliye shika nafasi ya juu katika SMZ na mpaka sasa SUK (SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA).

Hata ukijiuliza maswali mawili madogo utapata jibu.
Mosi: Kwanini harakati za "kupinga muungano" ziendeshwe na kikundi cha kidini JUMIKI (Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu?

Pili: Kwanini harakati hizo ziambatane na kuchoma makanisa na magari ya wachungaji? Ni Misikiti mingapi imechomwa?

Ni wazi kwamba muungano umepoteza maana kwa sasa, lakini tatizo sio muungano, ni udini. Kwa Zanzibar, Mtu yeyote anayetoka bara wanamchukulia kama Mkristu na ni adui.

Nilikua Z'bar siku 3 zilizopita, nilipata taarifa kwamba mjumbe mmoja wa baraza la wawakilishi alipokua akichangia hoja na Mhe. Jussa Ladhu kuhusu sehemu ya bahari ya zanzibar kufanywa ya muungano na Mhe. Tibaijuka alitumia maneno "Tusipokuwa makini na mambo haya tunaweza kujikuta WAKRISTU toka bara wanakuja kututawala!"

Inasemekana ndo sababu Rais wa Z'bar Dr. Shein anakuwa mzito kuchukua hatua kwa ghasia za namna hii maana naye ni mdini.

Nawasilisha.
Mkuu wangu kama hujafanya research yako na kuupata ukweli sii vizuri kuweka fikra zako wewe binafsi hapa kijiweni ili kutaka kufurahisha baraza au kujenga Udini ambao wewe mwenyewe unao isipokuwa unauficha nyuma ya mada hii.

Ni vizuri kwanza wewe mwenyewe ujiulize maswali haya na kuyapatia majibu kabla hujaweka dhana yako wewe kama unavyofikiria maana swala la Muungano limezungumziwa na watu wengi sana toka Malecela, Nyalali, Jumbe, Karume na viongozi wengine kibao lakini hata siku moja hujasikia SAUTI ya serikali ktk kujibu hoja hizo. Hakuna Udini ktk kero za muungano isipokuwa kuna ujinga mkubwa unafanywa kiasi kwamba swala hili limekuwa donda ndugu na linawakwaza sana watu wa chini kwa kuaminishwa kwamba ni Bara inayowakwaza.

Jana tu kuna jamaa yangu, mshikaji na muislaam kapigwa chuma cha kichwa na kalazwa hospital yupo mahutut..hivi sasa tunavyozungumza nimemaliza kuongea na mkewe, sababu tu ni Mbara na hatakiwi huko japokuwa ameajiriwa Zanzibar. Na zaidi ya hapo hakuna sura wala aya hata moja ktk Kuran wala hadith inayozungumzia fujo na ghasia zinazofanyika Zanzibar kama ni faradh au sunna ya Uislaam isipokuwa ni watu walio shindwa maisha kutokana na uongozi mbovu, hivyo vyombo vya dini vinaweza kabisa kuingilia japokuwa sii jukumu lao. Hapa ndipo tulipofika na bado kama serikali itashindwa kulitafutia ufumbuzi swala hili litakwenda bali zaidi ya mipaka, mbona bara mapadre wanasema mengi tu na mnadai ni haki yao kutetea uhuru, haki na usawa?

Wazanzibar na hao UAMSHO ni watu waliodanganywa na kina Maalim Seif, muafaka waloingia walifikiria CUF watapewa nafasi kubwa ya kuongoza lakini wamejikuta hawana mbele wala nyuma kwa sababu tatizo la Zanzibar sii la Kimfumo bali ni la VIONGOZI wao wenyewe kugombea sahani la biriani na kwa manufaa yao wenyewe.

Unajua ukimfumania mkeo na mwanamme mwingine kisha badala ya swala hilo kulimaliza wewe na mkeo ukachukua sheria ya kumtafuta mgoni wako na kumshambulia yeye, hii inaonyesha wazi kwamba huamini kwamba mkeo ndiye mkosefu ila kaghiribiwa na huyo jamaa. Unashindwa kutazama mapoungufu yako mwenyewe na wala kumuuliza mkeo alichokosa toka kwako pengine unajua udhaifu wako mwenyewe.
Huu ni mtazamo wa kiimani ambao watu wengi wa Zanzibar wanataka sisi bara tuwakabidhi Panga mkononi na kuwa mhanga wa penzi lao wakati viongozi wao wenyewe kina Maalim Seif wakidai walighiribiwa hivyo sii makosa yao bali ya Bara na ndiye mgoni wao. Lakini wasishangae bado viongozi hao hao wanaendelea kuzini nje ya ndoa yao maana muungano hawautaki sasa kwa nini wanaendelea kushika mamlaka ya kuongoza ndani ya muungano wasioutaka?.

Nachowaomba Wazanzibar ni moja tu, wamfuate rais wao dr.Shein wamuulize yeye msimamao wake kuhusu Muungano, wawafuate wajumbe wa baraza la Mapinduzi wawaulize msimamo wao kuhusu Muungano uvunjike au uwepo kisha kwa kutumia viongozi hao wazo linalowawakilisha wote lipelekwe ktk vyombo vinavyohusika. Na kama hawa viongozi watashindwa kufanya hivyo basi Wazanzibar watajua nani mbaya wao maana nijuavyo mimi na kwa uhakika mkubwa HAKUNA KIONGOZI yeyote ndani ya baraza la Mapinduzi anayetaka kuvunja Muungano. Na kama ndivyo basi hawa wananchi, wanaharakati na wanachama wa UAMSHO watu wa kuwashambulia ni baraza la Mapinduzi, viongozi wenu wenyewe na sii kusingizia Bara. Pateni majibu yenu kutoka kwa viongozi wenu na sii kufikiria mgoni wenu Bara ndiye atawapeni panga..
 
Kama kuna kitu kimoja ambacho chdema wanakitamani basi ni kuuvunja muungano, maana huo ukiwepo wao madaraka hakuna kabisa. Kura za Waunguja na Wapemba watasikia redioni tu. Ndio maana nikawafungulia nyuzi kuwaambia waungane rasmi na uamsho.

Nilimuona juzi Lissu kwenye ITV akitetea hizo fujo na akitetea wanaotaka kuongelea kuvunjika muungano wapewe fursa. Kwi kwi kwi teh teh teh!

Chadema jiungeni tu na Uamsho msione haya. Maana huko visiwani hamna chenu.

Wacha kukurupuka. Uchaguzi wa uzini uliofanyika siku za karibuni CHADEMA ilishika nafasi ya pili juu ya CUF.
CCM ilishinda, wakafuatia CHADEMA, kikafuatia chama cha CUF. kwahiyo utaona CHADEMA wanafanya vizuri kuliko unavyoeleza, chambua mambo sawasawa na ondoa ushabiki wa vyama hapa.
 
Mkuu wangu kama hujafanya research yako na kuupata ukweli sii vizuri kuweka fikra zako wewe binafsi hapa kijiweni ili kutaka kufurahisha baraza au kujenga Udini ambao wewe mwenyewe unao isipokuwa unauficha nyuma ya mada hii.

Ni vizuri kwanza wewe mwenyewe ujiulize maswali haya na kuyapatia majibu kabla hujaweka dhana yako wewe kama unavyofikiria maana swala la Muungano limezungumziwa na watu wengi sana toka Malecela, Nyalali, Jumbe, Karume na viongozi wengine kibao lakini hata siku moja hujasikia SAUTI ya serikali ktk kujibu hoja hizo. Hakuna Udini ktk kero za muungano isipokuwa kuna ujinga mkubwa unafanywa kiasi kwamba swala hili limekuwa donda ndugu na linawakwaza sana watu wa chini kwa kuaminishwa kwamba ni Bara inayowakwaza.

Jana tu kuna jamaa yangu, mshikaji na muislaam kapigwa chuma cha kichwa na kalazwa hospital yupo mahutut..hivi sasa tunavyozungumza nimemaliza kuongea na mkewe, sababu tu ni Mbara na hatakiwi huko japokuwa ameajiriwa Zanzibar. Na zaidi ya hapo hakuna sura wala aya hata moja ktk Kuran wala hadith inayozungumzia fujo na ghasia zinazofanyika Zanzibar kama ni faradh au sunna ya Uislaam isipokuwa ni watu walio shindwa maisha kutokana na uongozi mbovu, hivyo vyombo vya dini vinaweza kabisa kuingilia japokuwa sii jukumu lao. Hapa ndipo tulipofika na bado kama serikali itashindwa kulitafutia ufumbuzi swala hili litakwenda bali zaidi ya mipaka, mbona bara mapadre wanasema mengi tu na mnadai ni haki yao kutetea uhuru, haki na usawa?

Wazanzibar na hao UAMSHO ni watu waliodanganywa na kina Maalim Seif, muafaka waloingia walifikiria CUF watapewa nafasi kubwa ya kuongoza lakini wamejikuta hawana mbele wala nyuma kwa sababu tatizo la Zanzibar sii la Kimfumo bali ni la VIONGOZI wao wenyewe kugombea sahani la biriani na kwa manufaa yao wenyewe.

Unajua ukimfumania mkeo na mwanamme mwingine kisha badala ya swala hilo kulimaliza wewe na mkeo ukachukua sheria ya kumtafuta mgoni wako na kumshambulia yeye, hii inaonyesha wazi kwamba huamini kwamba mkeo ndiye mkosefu ila kaghiribiwa na huyo jamaa. Unashindwa kutazama mapoungufu yako mwenyewe na wala kumuuliza mkeo alichokosa toka kwako pengine unajua udhaifu wako mwenyewe.
Huu ni mtazamo wa kiimani ambao watu wengi wa Zanzibar wanataka sisi bara tuwakabidhi Panga mkononi na kuwa mhanga wa penzi lao wakati viongozi wao wenyewe kina Maalim Seif wakidai walighiribiwa hivyo sii makosa yao bali ya Bara na ndiye mgoni wao. Lakini wasishangae bado viongozi hao hao wanaendelea kuzini nje ya ndoa yao maana muungano hawautaki sasa kwa nini wanaendelea kushika mamlaka ya kuongoza ndani ya muungano wasioutaka?.

Nachowaomba Wazanzibar ni moja tu, wamfuate rais wao dr.Shein wamuulize yeye msimamao wake kuhusu Muungano, wawafuate wajumbe wa baraza la Mapinduzi wawaulize msimamo wao kuhusu Muungano uvunjike au uwepo kisha kwa kutumia viongozi hao wazo linalowawakilisha wote lipelekwe ktk vyombo vinavyohusika. Na kama hawa viongozi watashindwa kufanya hivyo basi Wazanzibar watajua nani mbaya wao maana nijuavyo mimi na kwa uhakika mkubwa HAKUNA KIONGOZI yeyote ndani ya baraza la Mapinduzi anayetaka kuvunja Muungano. Na kama ndivyo basi hawa wananchi, wanaharakati na wanachama wa UAMSHO watu wa kuwashambulia ni baraza la Mapinduzi, viongozi wenu wenyewe na sii kusingizia Bara. Pateni majibu yenu kutoka kwa viongozi wenu na sii kufikiria mgoni wenu Bara ndiye atawapeni panga..
Umenena kwa kweli!!!
 
Tatizo la udini lipo kwani hao 0.4% ndiyo wanaochomewa makanisa, hao pia wana uhuru wa kuabudu kama walivyo 99.96%. kumbuka hata mkifanikiwa kuwamaliza hao mtaanza Shia na Sunni kama ilivyo Iraq,somalia na Libya. Nawapeni ushauri wa bure Msiwabague wakristo na kuwafanya waishi maisha ya dhiki katika nchi yao. Mungu wa kweli hasaidiwi katika kuchoma makanisa, hiyo ni kazi ya shetani Kuchinja kuua na kuharibu. Wanaofanya hivyo ni maajenti wa shetani na kama wameaminishwa kuwa wataiona pepo kwa kuwaua wakristo wamedanganywa na wao wamedanganyika. Nini tatizo kama ni muungano na tuachane tu kwa amani mbona tulikuwa na East African community tukaachana na baadaye tumerudiana tena na hatukuchomeana nyumba wala kupigana. Vipi leo tuchomeane nyumba za ibada wakati uhusiano wetu kibinafsi ni mkubwa sana. Binafsi sioni nafaidika nini na muungano kama biashara tunafanya na watu wa nchi mbalimbali.tukianzisha vurugu hata anayechoma kanisa pia hatapona vita vinavyohusisha imani ni hatari kuliko vya watusi na wahutu. Mungu apishe mbali na vurugu na kama ni kuvunja muungano na uvunjike kwa amani. Mungu wa amani tupitishe salama katika hili pia. Amen

Ieleweke kwamba tatizo la udini Zanzibar sio la Wazanzibari, ni kikundi cha uamsho. Wazanzibari wengi hawana tatizo na wakristu wanaoishi zanzibar. Wana uamsho wana tatizo, na wanajaribu kufanya kampeni kupata washiriki wengi ili waweze kuchoma makanisa, kuchoma mabaa, kumwagia tindikali wauzaji wa maduka ya pombe na wamiliki wa mabaa n.k. Na naona wanahisi muungano unaleta wakristu zaidi zanzibar na wao wangependa asilimia ya wakristu iendelee kupungua na waislamu iendelee kuongezeka.
Kujumuisha tatizo la udini kwamba ni la Wazanzibari nahisi sio sahihi, mpaka hapo ushahidi wa kutosha utakapoonyesha hivyo.
 
Muungano hauna maana yoyote kama watu wataendekeza chuki za kidini na ukabila
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom