Sio kweli Mkiristu kwenye BLM ni Mwakanjuki pekee, alishakuwepo John Okello, Isack Sepetu na kuna wakristu wengi tuu wenye majina ya Kiislamu.
Hata kina Wolfgang Dourado, Agustino Ramadhani, Charles Hillary etc ni Wakristo Wanzanzibari!.
Kanisa lilianzia Zanzibar na Bagamoyo kufuatia kupigwa marufuku biashara ya utumwa. Soko lilikuwa Bagamoyo na Zanzibar, Kanisa liliwalipia fidia watumwa ili kuwagomboa na ndio Wakristu wa kwanza!.
Kiukweli udini halihawahi kuwa tatizo Zanzibar!.
Nakubaliana na wewe udini siyo tatizo kuu la ZNZ. Tatizo la Znz ni hali mbaya ya maisha inayochangiwa na ukosefu wa ajira n.k
Kijamii mtu anapokosa fursa muhimu za kujiendeleza kiuchumi, ili kujiliwaza ujiunga na wenzake kama yeye katika vikundi vya kidini, kikabila, kikanda n.k na kuona wote walio nje ya kundi lake kijamii kama maadui.