Tuwe makini kununua magari show rooms za magomeni-ubungo-mwenge

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Hizi show rooms nazipatia mashaka sana, watu wengi wanaoibiwa magari hapa Dar ni wale walionunua magari yao kwenye show rooms za maeneo hayo. Na uchunguzi wangu mdogo niliofanya magari mengi kwenye show rooms hizi ni yale magari yaliyotembea kwa muda hapa TZ, kwahiyo yanakuwa ni magari ya watu fulani ambao wameomba wawekewe kwenye hizo show rooms ili wauziwe, na hata utakapokuja kulinunua hutapata nafasi ya kuonana na mtu mwenye hilo gari. Baada ya muda hilo gari utaibiwa katika mazingira ya kutatanisha, ni kana kwamba mtu alikuwa na copy ya ufunguo wa hilo gari. wengi wanaoibiwa hayo magari ni wale wanaoishi maeneo hayohayo, wataibiwa maeneo ya sinza, mwenge, pale mlimani city ndio usiseme, maeneo ya udsm, changanyikeni, mbezi etc.

Kwahiyo tuweni makini sana tunaponunua magari kwenye show rooms hizi. Maana ni jinsi gani inavyouma kuibiwa gari ambalo umelipata baada ya kujinyima mambo mengi na kulinunua halafu mtu anakuja kulichukua kama vile la kwake.
 
Huna haja ya kuogopa kama unajua tatizo ukinunua magari ya huko badili lock zote esy unachotakiwa kufanya mnafanya makubaliano kiasi cha kwamba unachotoa hata ukiweka hela za lock uujaumia sana easy
else wayapeleke wapi hayo magari jamani msiponunua nyie
 
Sitonunua gari bongo hata siku moja,gari naagiza nje magari ya yard ni ya wizi na mabovu we unanua gari alina lisence plate(plate number) then wanakwambia subiri wafanye registration after week itakua tayari then no ya gari ikija BCR xxx ambayo inazaidi ya miaka miwili ndio utashangaa kwanin namba isiwe hizi za kisasa hz BWT xxx
 
kuna watu wawili nawajua wamefanyiwa mchezo huo pale m city kuwauliza walinunua yard za sinza tena kwa bei ya kutupa hazikupita wiki tatu wakaibiwa.ni bora uagize tu mizungu ya unga ndii imefungua yardi full uzushi na uizi kuweni makini na hizi yard jamani
 
kuna yard moja ipo mwananyamala ndani ndani..., huu mwaka wa pili naona magari yale yale lakn haifungwi! i smell somethn fishy kwny hzi yards....,
 
Show room chache utakuta mmiliki/muuzaji wa magari yote ni mtu mmoja. Zilizo nyingi ni mkusanyiko wa wajasiriamali wanayapeleka na kuyaweka pamoja kwa makubaliano ya kuuza na kutoa % fulani kwa mwenye yard. Hivyo magumashi ni rahisi kuwepo. Watu wengine sio waaminifu wanakuuzia gari zao ambazo walikuwa wanatumia lakini bado wanabaki na nakala ya funguo. Zipo baadhi ya yadi zinauza magari mazuri na yapo kwenye hali nzuri na kwa uaminifu mkubwa.
 
Halafu huwa wanakudanganya hiyo gari unayotaka kununua mwenyewe anafanya kazi bank, na mambo kibao kiasi kwamba uhisi mwenye gari si mtu mwenye shida. kuna watu watatu waliibiwa hizo gari na wote kila mmoja anasema aliambiwa mwenye gari ni mfanyakazi wa bank tena cha kushangaza zaidi wote wanafanya kazi NMB.
 
sio kidogo kwa kweli, kuna mtu wangu wa karibu naye amelizwa siku si nyingi maeneo ya udsm inawezeka ndio mchezo huo huo. Lakini hao zao si nyingi.
 
Asee polen
nimekusanya weee ndo
inakaribia ya
bodaboda tena used!

Hata pale lumumba na kidongo chekundu magari mengi ni ya wizi au mabovu kuna dalali anaitwa DIBLO ni hatari sana,watz tunapenda vitu vya bei nafuu sana
 
Hapo ndiyo nachokaga na hizi biashara za wizi wizi!! Niilikuwa na mpango wa kununulia gari Dar nikirudi, sasa mipango naipeleka ng'ambo!! Na kama kuna mtu anatusoma na anafanya hizo biashara bora ajibu hizi shutuma. Kama biashara hailipi, badilisha.
 
Why to bother? Kuna securty systems kibao Tanzania hii, kuna comprehensive insurance. Cha muhimu ukinunua gari popote hakikisha unatransfer ownership haraka ili uhakikishe una rights zote na hilo gari.
Tukumbuke kuwa siyo kila mtu mwenye akili au uwezo wa kuagiza, na wengine huwa wanona tabu kusubiri gar kwa zaid ya miez 2. As long as tatizo linajulikana, ukinunua gar showroom hakikisha tu unalipa security ya kutosha!
 
Wale wa mikoani ndo wanauziwa sana magari ya wizi kiujumla polisi na TRA wanajua kwani %kubwa ya madalali wa lumumba na kidongo ndo marafiki zao,nawashauri usikubali kuuziwa gari bila kwenda TRA kulikagua
 
Huna haja ya kuogopa kama unajua tatizo ukinunua magari ya huko badili lock zote esy unachotakiwa kufanya mnafanya makubaliano kiasi cha kwamba unachotoa hata ukiweka hela za lock uujaumia sana easy
else wayapeleke wapi hayo magari jamani msiponunua nyie

Show room yako iko wapi Pidd?
Halafu hebu jivue gamba kwenye hiyo avatar jamani! Hicho kitoto hakiwezi kupata afya wala kufurahi hata siku moja?
Unyanyasaji wa watoto huu!

Hizi show rooms nazipatia mashaka sana, watu wengi wanaoibiwa magari hapa Dar ni wale walionunua magari yao kwenye show rooms za maeneo hayo. Na uchunguzi wangu mdogo niliofanya magari mengi kwenye show rooms hizi ni yale magari yaliyotembea kwa muda hapa TZ, kwahiyo yanakuwa ni magari ya watu fulani ambao wameomba wawekewe kwenye hizo show rooms ili wauziwe, na hata utakapokuja kulinunua hutapata nafasi ya kuonana na mtu mwenye hilo gari. Baada ya muda hilo gari utaibiwa katika mazingira ya kutatanisha, ni kana kwamba mtu alikuwa na copy ya ufunguo wa hilo gari. wengi wanaoibiwa hayo magari ni wale wanaoishi maeneo hayohayo, wataibiwa maeneo ya sinza, mwenge, pale mlimani city ndio usiseme, maeneo ya udsm, changanyikeni, mbezi etc.

Kwahiyo tuweni makini sana tunaponunua magari kwenye show rooms hizi. Maana ni jinsi gani inavyouma kuibiwa gari ambalo umelipata baada ya kujinyima mambo mengi na kulinunua halafu mtu anakuja kulichukua kama vile la kwake.

Nadhani hipo haja ya kuhakikisha unabadilisha securty system unapokuwa umenunua gari lililokwisha tumika hapa nchini hususani katika majiji ya DAR ES SALAAM , MWANZA, MBEYA NA ARUSHA.
 
Back
Top Bottom