Tuwe Macho na Mafia Dance Festival (1-15 August 2010)

Kabwela

Member
Feb 11, 2008
76
5
Ndugu Watanzania nilimepata fursa ya kuwa maeneo ya visiwa vya Mafia. Kuna Ujio wa Mafia Dance Festival (http://www.mafiadancefestival.com) ambayo inategemea kufanyika kuanzia tarehe 1 mpaka 15 Agosti 2010 na tamasha hilo linategemewa kuwa na washiriki 3,500 kutoka nchi mbalimbali duniani. Kwa ukubwa na miundombinu ya Kisiwa cha Mafia hasa makao makuu ya wilaya hiyo (mji wa kilindoni kwa wanoufahamu) ni vigumu kuweza kubeba idadi hiyo ya watu (yawezekana wataleta disposable equipments).

Tatizo kubwa hasa la tamasha hilo ni tofauti na lile la Jahazi Zanzibar ni kuwa mara ya mwisho lilifanyika Spain 2006 na limekatailwa nchi nyingine duniani kwa kuwa linahusisha sana ucheza uchi, uvutaji mkubwa wa vilevi na madawa ya kulevya pamoja na ngono holela popote washiriki wanapokuwepo kutokana na vilevi na mila za washiriki hasa wa nchi za ulaya. wazee wa Visiwa hivyo wanalalamika sana na kulikataa hilo tamasha na wakiuuliza uongozi wa wilaya wanasema hajataarifiwa na yeyote kuhusoiana nalo ingawa kwenye tovuti ya wawandaaji wanaonesha kuwa wanaandaa kwa ushirikiano na halmashauri ya wilaya wakiwa na baraka za wizara ya Maliasili na Utalii.

Kutokana na mchanganyiko huu nimelazimika kuwaomba waTZ hasa wahusika watupe majibu kwani hili tamasha likifanyika litaharibu taswira ya utalii kwenye visiwa hivyo kwani mahoteli yote yaliyo eneo la uhifadhi (Marine Park) kwa pamoja wamekataa kukubali kuwapa nafasi za malazi washiriki wa tamasha hilo ingawa waandaaji hasa waliopo Afrika ya kusini kuwafuata na kuwabembeleza sana lakini ilishindikana kuwashawishi.

Watanzania ni kweli tunapenda uwekezaji na maendeleo na kutambulika maeneo yetu ya utalii lakini hili la kucheza uchi, kufanya ngono hadharani, kubwia na kuvuta madawa ya kulevya holela halitotusaidia sana zaidi ya kuharibu watoto wetu. Wazee wa mafia wanasema serikali inataka kuwaletea Tsunami kama ilivyotokea Asia kutokana na mambo yalivyokuwa yakifanyika ufukweni.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Mzee uko Xenophobic kimtindo. I think we have other bigger problems to solve than this which exists only in your head.
 
huo ni mpango wa cia kudhibiti na ku destroy islamic influence
pwani ya east africa.
 
Mzee uko Xenophobic kimtindo. I think we have other bigger problems to solve than this which exists only in your head.
Ab,
Ili uweze kupambana na makubwa ni lazima uwe na uwezo wa kutatua haya madogo. Na hili kwa kiasi fulani linahitaji ufumbuzi kwani si Dogo kama unavyodhania.
 
1.Usije kuwa scammed kirahisi . wahamasishaji wa hiyo shughuli hawana physical contact zaidi ya email. Hakuna hata simu ya organiser. Hakuna hata Link Travel agent. Shtuka wewe usiamini kila unachoona kwenye mtandao.

2.hakuna hoteli inaweza kukataa mteja kama ana mshiko . Awe Teja, Changuduoa , awe wa short time , etc

3 Hakuna serious inverstor wa festival anayetafuta faida anaweza kuhangaika kuandaa tamasha mafia.bado hujashtuka tu.

Otherwise
4.Waache waje wabikiri virgin island zetu. Kama kutoka dar kufika mafia ni mbali kuliko Mafia to capetown unategemea nn??zaidi kwa sababu tunategemea utalii lazima tukubali na madhara yake.
 
Kwa hasira kina GT na wana Mafia wasiichague tena CCM kuliwakilisha Jimbo lao ikifika wakati wa uchaguzi mkuu!
 
haya ukumbi ni wako kunipa hiyo elimu unayoijua wewe peke yako

kwa ufupi ni kuwa
ili kudhibiti islamic fundamentalist
cia wana sera rasmi ya ku sponsor mambo mengi ambayo
yana kwenda kinyume na islamic fundamentalistic ideas...
na wana sponsor thru ngos na organisations mbalimbali...
tazama matamasha ya kimataifa ya burudani Zanzibar..
na yote utaona kuna wazungu nyuma yake....
sio Zanzibar tu nchi nyingi zenye waislam wengi au maeneo yenye waislam
wengi,huwezi kukuta tamasha hilo mbeya au bukoba,but zanzibar au mombasa
au mafia.
 
huo ni mpango wa cia kudhibiti na ku destroy islamic influence
pwani ya east africa.

uislamu umeanza lini east africa, na kwa nini sasa ndio waanze kuuangalia kwa nia ya kuudestroy, mbona marekani uislamu upo mwingi tu na unakuwa na hawajaudestroy, au Wamarekani wanataka uislamu uwe kwao tu

nilikuwa nafurahia sana post zako, lakini kwa hili umeteleza
 
kwa ufupi ni kuwa
ili kudhibiti islamic fundamentalist
cia wana sera rasmi ya ku sponsor mambo mengi ambayo
yana kwenda kinyume na islamic fundamentalistic ideas...
na wana sponsor thru ngos na organisations mbalimbali...
tazama matamasha ya kimataifa ya burudani Zanzibar..
na yote utaona kuna wazungu nyuma yake....
sio Zanzibar tu nchi nyingi zenye waislam wengi au maeneo yenye waislam
wengi,huwezi kukuta tamasha hilo mbeya au bukoba,but zanzibar au mombasa
au mafia.

Hujui hata unachoongea maskini.

Hayo matamasha yanafanyika ufukweni mazee. Sasa waende kuandaa Bukoba au Mbeya ili iweje?

Ni kweli CIA inaplot mambo mengi kwa ajili ya American interest, na agenda yao ni uchumi kwa sababu wao ni ma-capitalist, kila wakati wapo mbioni kusecure masoko, malighafi au cheap labour kwa ajili ya watu walio nyuma ya utawala wa US. Lakini kusema kwamba US inakula sahani moja na Usilam for the sake of Islam is a BIG Bull $hyt. Kama wangetaka kufanya hivo waangeenda Indonesia and the like, kwenye most populated Muslim countires kwenye sayari hii.
 
uislamu umeanza lini east africa, na kwa nini sasa ndio waanze kuuangalia kwa nia ya kuudestroy, mbona marekani uislamu upo mwingi tu na unakuwa na hawajaudestroy, au Wamarekani wanataka uislamu uwe kwao tu

nilikuwa nafurahia sana post zako, lakini kwa hili umeteleza

we una tatizo la kuelewa...
nimefafanua zaidi kuwa wanacho dhibiti ni
islamic fundamentalistic ideas na sio uislam as a whole kwa ujumla..
mfano siasa kali huwa wanapromoti wanawake na wanaume wasichanganyike pamoja
kwa hiyo matamasha kama hayo yana husisha wanawake na wanaume
kuchanganyika pamoja,free sex na kadhalika.alcohol na mengineyo.
 
Hayo matamasha hayajaandaliwa kwa ajili ya watu wa Mafia. Get that straight into your head. Hivo kusema sijui ku-influence blah bl;ah is beyond comprehension kwamba mvuvi au mkulima wa Mafia ataenda kushiriki hili tamasha. Inahitaji ukichaa ku-imagine vitu kama hivo.
 
Hujui hata unachoongea maskini.

Hayo matamasha yanafanyika ufukweni mazee. Sasa waende kuandaa Bukoba au Mbeya ili iweje?

Ni kweli CIA inaplot mambo mengi kwa ajili ya American interest, na agenda yao ni uchumi kwa sababu wao ni ma-capitalist, kila wakati wapo mbioni kusecure masoko, malighafi au cheap labour kwa ajili ya watu walio nyuma ya utawala wa US. Lakini kusema kwamba US inakula sahani moja na Usilam for the sake of Islam is a BIG Bull $hyt

ufukweni mbona husikii matamasha namibia hivi?
burkina faso wana ufukwe???
nimeeleza hapo juu,hawana lengo la kudestroy uislam kama dini..
but ku destroy imani kali ya kidini,
na unaposema hao ni ma capitalist unaji contadict mwenyewe...
mfano Afghanistan,taliban walipiga marufuku bidhaa nyingi za wamarekani..
na usisahau islamic fundamentalistic ideas inakwenda against na bidhaa
za U.S kama films,music, na cultural products kwa ujumla.
 
Hayo matamasha hayajaandaliwa kwa ajili ya watu wa Mafia. Get that straight into your head. Hivo kusema sijui ku-influence blah bl;ah is beyond comprehension kwamba mvuvi au mkulima wa Mafia ataenda kushiriki hili tamasha. Inahitaji ukichaa ku-imagine vitu kama hivo.

kama hayahusishi watu wa mafia kwa nini yafanyike mafia...????
unaweza sema tamasha la busara zanzibar halihusishi watu wa zanzibar??
hivi huko mafia kuna wakulima wazee tu?hakuna vijana watakaoshiriki
matamasha hayo???

hakuna teenagers mafia sio??????

wewe bado huelewi kitu naona.
 
ufukweni mbona husikii matamasha namibia hivi?
burkina faso wana ufukwe???
This is pointless. Maana wangechagua Namibia au kwingine, wewe au mwingine angetoa kisingizio kingine tena. Google hilo tamasha ujue maudhui yake, pia uone mara ya mwisho walifanyia wapi..Usikurupuke.

nimeeleza hapo juu,hawana lengo la kudestroy uislam kama dini..
but ku destroy imani kali ya kidini,

Una ushahidi kuwa Mafia kuna simani kali ya kidini? Lete uthibitisho acha maelezo ya jumla na assmptions.

na unaposema hao ni ma capitalist unaji contadict mwenyewe...
mfano Afghanistan,taliban walipiga marufuku bidhaa nyingi za wamarekani..
na usisahau islamic fundamentalistic ideas inakwenda against na bidhaa
za U.S kama films,music, na cultural products kwa ujumla.

Unazidi tu kujizongazonga..Hapo najicontradict kitu gani? kusema kwamba US ni ma-capitalist? Hilo la bidhaa unalitoa kutoka wapi? Na unao uthibisho kuwa hili tamasha ni bidhaa ya US?
unaleta assumptions based on assumptions based on another assupmtions on and on. Nenda ka-google ujue hilo tamasha undani wake kabla ya kukurupuka na hizi theories zako zisizo na kichwa wala miguu.
 
kama hayahusishi watu wa mafia kwa nini yafanyike mafia...????
unaweza sema tamasha la busara zanzibar halihusishi watu wa zanzibar??
hivi huko mafia kuna wakulima wazee tu?hakuna vijana watakaoshiriki
matamasha hayo???

hakuna teenagers mafia sio??????

wewe bado huelewi kitu naona.

Naona tunajadili hisia na assumptions zako badala ya fact.mpaka dakika hii hujaleta fact hata moja. Inashangaza.
 
Naona tunajadili hisia na assumptions zako badala ya fact.mpaka dakika hii hujaleta fact hata moja. Inashangaza.

ndo maana nikakwambia hujui maana ya cia.....
nafikiri hata unaposikia waandishi wa habari wa marekani
wamekamatwa huko North Korea na Iran huwa unaamini
ni kweli waandishi wa habari........
mimi na wewe tupo two worlds apart.....
hata definition yako ya facts iko very interesting....
 
Back
Top Bottom