Tuwe creative kutengeneza story fupi.

hahahahaah! hii thread inaifanya wikendi iende fresh, watu8 unatisha kaka. Ngoja niende nikawatazame vijana wa Emirates nikirudi huenda nitakuta hadithi imefika mwisho.

Hahahah pamoja mkuu hebu na wewe weka yako mistari tamthiliya hii isogee, si ajabu kina Ray, Wema n.k wakanyofoa ideas kadha wa kadha kutoka hapa na watafyatua filamu
 
Last edited by a moderator:
watu8 umetisha yaani umenikumbusha mbali tangu safari ya Katavi na Preta kutoka kijijini mpanda ndani ya gari ambalo dereva Autorun alikuwa anaendesha bila kufuata sheria za usalama barabarani. Mpaka Dar ndani ya jiji la maraha ambapo Preta anakutana na Bishanga na kupata kibarua..lol

Ndio hivyo mkuu tunajaribu kutupiamo ubunifu kama matakwa ya uzi husika ututakavyo....
 
Last edited by a moderator:
wana Chit Chat mbona tumeisusa hii thread....hebu onesheni ujuzi wajameni...
 
"Nashukuru sana kwa ushauri ulionipatia mama, moyo wangu umefarijika na hakika umenirudishia tena tabasamu usoni pangu", Preta alimshukuru mamaye. "Usijali mwanangu, siku zote tambua, dunia hadaa walimwengu shujaa",alimalizia Kaunga kumuasa mwanawe.
Mlango wa mbele ulifunguliwa na ni Katavi alikuwa akirejea kutoka Samaki samaki. Wakati huo Preta alikuwa anamalizia kumimina juisi ya mchanganyiko wa parachichi na embe."Eenh mmefungwa ngapi huko?", lilikuwa ni swali la kichokozi toka kwa Preta. "Mwaka huu lazima tubebe kombe, sisi ndio wa Darajani bwana, leo tumeshinda 2 - 1", Katavi alizungumza kwa kujiamini. "Haya bwana mi yangu masikio tu, hahaha, vipi nikumiminie na wewe juisi?", Preta aliuliza. "Mhhh nitashukuru kweli, tafadhali", Katavi alisisitiza.
Dakika tano baadaye wawili hawa walikuwa juu ya viti katika bustani tulivu mbele ya nyumba yao, nia ya kukaa mahali hapo ilikua ni kufanya mazungumzo ya kipi kinamsibu Preta.
"Katavi.....", Preta aliamua kuvunja ukimya na alianzisha mazungumzo......
"Najua una shauku sana ya kutaka kujua ni kipi kinanisibu, si ndio?", Preta alimuuliza Katavi, Katavi akajiweka vizuri pale kwenye kiti ili kumsikiliza Preta. "Kusema ukweli ndugu yangu sisi wanawake tunyanyasika sana huko maofisini, wakati mwingine mtu unatamani hata uache kazi ukae tu nyumbani", alisema Preta. "Ni kwanini dada unasema hivyo?", aliuliza Katavi kwa sauti ya upole sana............................
 
Last edited by a moderator:
Preta alimuangalia Katavi usoni kwa macho matulivu kabisa, "masikini kaka wa watu anavyonionea huruma, ila hata nikimwambia sijui kama ataweza kunisaidia naona ndio nitazidi kumtia mawazo kabisa", aliwaza Preta. " ila acha tu nimwambie huenda akanipa ushauri mzuri nikichanganya na alionipa mama yangu Kaunga huenda nitazidi kuwa na amani", aliendelea kuwaza Preta. Ule ukimya wa Preta ulimpa mashaka Katavi, "dada mbona hasemi kitu ananiangalia tu, au ni mimi ninamkwaza kwa kukaa kwake bila kazi?, itabidi huku nikitafuta kibarua wakati huohuo namtafuta na binamu yangu" Katavi nae aliwaza hivyo...........................
 
Last edited by a moderator:
Mazungumzo baina ya Preta na Katavi yalichukua sura ngeni sana baada ya kutawaliwa na ukimya mwingi,ilikuwa kama kikao ambayo haikuwa na mwenyeketi na wahusika wote walikuwa kama bubu Katavi akajikaza akakumbuka maneno ya aliyekuwa rafiki yake wa zamani aitwaye watu8 kuwa "mwanaume lazima siku zote uwe na ujasiri",akiliza Katavi sikajinasua katika giza na kuanza kupata mwanga ndipo midomo ya Katavi ilipomwambia Preta,"Hivi unajua leo ni Ijumaa ,tunaweza kunywa bia moja moja?"ingawa Katavi bado alikuwa na ushamba wa jiji lakini alishawahi kwenda kunywa bia kwenye bar na rafiki yake Arushaone ambaye ni jirani yake Preta,kwa vile Preta alizongwa na mawazo naye akajikuta akikubaliana na mawazo ya Katavi,moja kwa moja wakaanza kuelekea baa,wakaangiza mishikaki huku wakipata Castle,kila mtu alikuwa hajanywa bia yapata wiki kama tatu kwahiyo bia ilikuwa inaonekana tamu na ujazo wa pombe ulikuwa unapungua kwa haraka,mara wakajikuta wapo bia ya pili huku wakitafuna mishikaki,mara chupa za zikabaki kavu wakaongeza zingine Preta alianza kuwa na maneno ya kuvutia,Katavi alikuwa anachanganya stori ambazo zilihusu maisha yake ya tabu na mateso,Preta hakufurahishwa nazo na kuanza kuchomekea stori za mapenzi na kujadili mahusiano na wapenzi wao wa zamani.
................Excy nilikuwa nimekaa kwenye meza ya nyuma yao na kuona kila kilichoendelea,nilisikia kila kitu walichoongea maana walikuwa wanaongea kwa sauti ya juu,ila Preta na Katavi walionekana kwenye ulimwengu wa mapenzi yaliyorahisishwa na bia bila wao wenyewe kujitambua,gafla wakaanza kuelewa na yapata mida ya saa nne usiku,wakaanza kuelekea nyumbani kwa Preta,walipoingia ndani Preta alimkumbatia Katavi na kumwambia "Unajua mara ya kwanza nilipokuona kwenye basi nilikupenda ila ulipotapika nilikudharau ila mwenzio nilijawa na huruma ndo maana mpaka leo upo na mimi"halafu akamkumbatia tena,Katavi hakuamini.
..................Hisia za mapenzi zilizotawaliwa na pombe zikamjia,ila alijizuia Preta akasikika akimwambia Katavi sema kweli leo silali mwenyewe naogopa,twende chumbani kwako",katavi alikosa ujasiri maana alikuwa Nyumbani kwa Preta na pia akawaza kama atakataa labda Preta anaweza kufanya maamuzi ya ajabu kutokana na pombe,Katavi akamshika Preta kiuno,wakaelekea chumbani,wakakaa juu ya kitanda,Katavi akamvuta Preta polepole juu ya kitanda,akamlaza kifuani,Preta alijihisi kama kinda la ndege linalolishwa na mama yake,akamwambia Katavi kwa sauti ya upole,"mwenzio sema kweli nakupenda,nimejaribu kuficha hisia zangu ila nimeshindwa,"kisha akamwangalia Katavi machoni,kila moja aliona macho ya mwenzake yanavutia,wakapeana busu na kukumbatiana tena...........
 
Katavi kwa wasiwasi na mashaka moyoni mwake, akajisemea "mh!! Lakini Preta aliwahi sema ana mpenzi wake na mimi ni rafiki tu,nikifanya kweli hapa asubuhi nitamwangalia usoni kweli,pombe zimetutokana kichwa wakati huo? " .. Liwalo na liwe toto kama hili nikiliacha vilevile anaweza kuniona mzembe.....
Ndipo sasa...... Katav

Sent from my torch 9700
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom