Tuwazomee wote wanaotufilisi... Heko MwanaHalisi , Heko Saed Kubenea kwa uzalendo

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
CHENGE KUFURU TUPU, AMILIKI BILIONI 25 (Kayumba hana hata mia mfukoni)


Na Saed Kubenea

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua.

Chenge amekuwa mfanyakazi serikalini kwa karibu miaka 30 na hafahamiki kuwa mfanyabiashara.

Kiwango kinachotajwa ni pamoja na fedha zilizogunduliwa na makachero wa Uingereza katika akaunti zake za nchi za nje.

Fedha zilizoko kwenye akaunti yake ya nchini, Na. 011101006950 katika benki ya NBC Limited, ni Sh. 25,794,805.89 za Tanzania hadi Ijumaa iliyopita, tarehe 11 Aprili 2008.

Katika akaunti yake ya Uswisi, ambako ana akaunti ya fedha za kigeni, Chenge amehamishia dola za Marekani 467,000, sawa na zaidi ya nusu bilioni kwa fedha za Tanzania.

Fedha za Uswisi zimelimbikizwa katika akaunti Na. 030105000364. Zilihamishwa kutoka akaunti Na. 011105011782 ya kampuni ya TANGOLD Limited, tangu 22 Februari 2006 kupitia NBC Limited.

Taarifa za kuaminika ambazo MwanaHALISI imezipata zinasema Chenge ni Mkurugenzi wa kampuni ya TANGOLD Limited ambayo ina dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni za Tanzania katika NBC Limited tawi la Makao Makuu.

Aidha, kampuni hiyo inahifadhi Sh. 1,379, 359,367.39 katika akaunti Na. 011103024852 tawi hilohilo la NBC Limited.

Habari tulizopata wakati tukienda mitamboni, zinasema kwamba makachero wa Uingereza wanafuatilia uhalali wa Euro 3 milioni (sawa na zaidi ya Sh. 8 bilioni za Tanzania) zinazodaiwa kuwa Chenge alizipeleka kwenye akaunti zake nje ya nchi.

Taarifa nyingine ambazo hatukuweza kuzithibitisha haraka, zinasema Chenge alihamisha kwa mkupuo dola 600,000 za Marekani kwenda kwenye akaunti ya ofisa mwandamizi mmoja aliyekuwa Benki Kuu miaka kadhaa iliyopita, na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma nchini.

TANGOLD ni kampuni ambayo inadaiwa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na ambayo inadaiwa pia kuwa ndiyo imerithi mali na madeni ya kampuni ya Meremeta Limited iliyokuwa ikijihusisha na uchimbaji madini, Buhemba, mkoani Mara.

Hata hivyo, kuna utata juu ya lini kampuni hiyo ilianzishwa nchini. Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi aliuambia Mkutano wa Tisa wa Bunge kuwa TANGOLD iliundwa mwaka 2006 kupitia Task Force maalum ya serikali, kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni ilianzishwa mapema 2000 au kabla.

Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba tarehe 1 Januari 2000 walikuwa na akaunti ambayo haikuwa hata na senti moja katika akaunti zake mbili hadi 29 Desemba 2005 zilipoingizwa dola 13,340,168.37.

Fedha hizo zilikuwa zinatoka Hazina kupitia Benki Kuu (BoT).

Kwa akaunti ya fedha za Tanzania, tarehe 1 Agosti 2005, TANGOLD Limited ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, Sh. 4,703,221,229.08 kwa hundi Na. 241741 na kufanyiwa uhamisho wa haraka (special clearance).

Chenge, akiwa mkurugenzi, anahusika na uhamishaji, ulimbikizaji na ulipaji wa fedha kutoka akaunti za TANGOLD.

Wakurugenzi na waidhinishaji malipo wengine wa kampuni hiyo ni, Daudi Ballali, Gray Mgonja, Vincent Mrisho na Patrick Rutabanzibwa.

Ballali alikuwa gavana wa BoT, Mgonja akiwa Katibu Mkuu Hazina, Mrisho akiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu Maji na Umwagiliaji.

Matumizi ya fedha kutoka akaunti hizi ambako kuna mkono wa Chenge ndiyo yanaongeza utata.

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

Miongoni mwa waliolipwa ni viongozi wa CCM, waandishi wa habari na wengine ambao hawakuweza kutambulika. Muhimu ni kwamba karibu fedha hizo zote zililipwa wakati uchaguzi wa CCM mwaka jana ambapo Chenge aliwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Alishinda kwa kura nyingi.

Akaunti ya TANGOLD inaonyesha kutoingiza kiasi chochote cha fedha kwa miaka mitano, kati ya Januari 2000 na Desemba 2005.

Source : Mwanahalisi
 
Hii habari ni ya lini? nakumbuka kuisoma mwaka jana.

Ni ya mwaka 2008 mkuu, nimeileta hapa kuwakumbusha wadau juu ya uharamia uliowahi kufanywa na watu ambao leo tunawaita waheshimiwa, hawa hawa ambao leo ndio wanasababisha wabunge wetu wapigwe na polisi (namzungumzia Mary Chitanda)
 
Back
Top Bottom