Tuwasaidie wandishi wetu wa habari:

Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,315
7,113
Albino walia kuathiriwa na mafuta


na Stella Ibengwe, Shinyanga


amka2.gif

CHAMA cha watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) mkoani Shinyanga kimesema mafuta aina ya ENAT Vitamin "E"Crime wanayopaka kwa ajili ya kujikinga na mionzi ya jua yanawaathiri.

Hayo yalielezwa jana na mwenyekiti wa chama hicho, Eunice Manumbu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa ambapo aliitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iwe inafanya utafiti wa kina kabla ya kuwapatia mafuta ya kupaka.

Manumbu alisema mafuta hayo wakiyapaka ngozi zinavimba, hivyo serikali kupitia wizara husika ni vema iwe inafanya uchunguzi juu ya mafuta ya ngozi wanayoyatumia kabla ya kuyasambaza.

"Mafuta ambayo yameshaonyesha madhara ni aina ya ENAT Vitamin "E"Crime yanayotolewa na kampuni ya MEGA Life Services PTY ya nchini Australi; tunaitaka wizara ifanye uchunguzi na suala hili lichunguzwe kwa umakini mkubwa kwani linaweza kutusababishia ugonjwa wa saratani ya ngozi.

"Madhara ambayo yameanza kuwapata albino wenzetu yametufanya tuanze kujipaka mafuta ya ng'ombe maarufu kama samli ili kuepuka kupatwa na madhara ambayo yanatokana na mafuta hayo," alisema.
Alisema mafuta wanayopaka ambayo hayana madhara yanauzwa sh 18,000 hadi 45,000 na hufanya kazi hadi miezi mitatu hadi sita.


HAPO KWENYE RED WANA-JF NDIYO MAFUTA GANI HAYO?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom