Tuwaokoe hawa watoto!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa asubuhi ninapoelekea kazini nikiwa barabarani ocean road upande wa baharini namuona mama mmoja na watoto watano hukaa hapo pembeni ya bahari toka asubuhi mpaka jioni kila siku, akiwa na wanawe watano tena wenye afya nzuri na wasafi tu, na wanne kati yao wanatakiwa wawe shuleni.

Siku moja nililazimika kumsogelea kwa karibu sana ili nijue kama ni kichaa ama lah! Ukiangalia afya za watoto na usafi wa huyu mama utagundua ni mtu anayetokea familia yenye uwezo kuweza kuwapeleka hawa watoto shule lakini tatizo inaonyesha huyu mama amerukwa na akili kwa kiasi fulani.

Binafsi inaniuma sana kuona hawa watoto mda wote wanashinda baharini badala ya kwenda shule, ni vigumu sana kwa mtu binafsi kama mimi kuingilia kati hili suala ili kuwaokoa hawa watoto, ila naamini Serikali inaweza ikachukua hatua kuwanusuru hawa watoto kwasababu hawasomi shule japo ukiwaangalia ni watoto active, wasafi na wana afya nzuri mda wote wapo na mama yao hapo baharini ni zaidi ya mwaka mmoja sasa wanafika hapo kuanzia saa 12 alfajiri na kuondoka kuanzia saa11 jioni.

Ninaamini huyu mama hana ndugu mwenye akili timamu, kwasababu wasingeweza kuacha watoto wapoteze mwelekeo kwasababu tuu mama yao kapungukiwa akiri na anawalazimisha kwenda kukaa nao pembeni ya bahari kwa kipindi chote hicho

Wana JF naombeni ushauri mimi kama mtu binafsi nifuate hatua gani ili kuanza mchakato wa kuhakikisha hawa watoto hawapotezi dira ya maisha yao?
 
Halafu kwa story iliyopo ni kwamba kila mtoto pale ana baba yake!
Huu ni unyama usioelezeka, wanaume tumekosa kabisa wanawake wa kutembea nao mpaka tuende kwa yule mama? Tena unakutana naye kimwili kavu kavu bila kinga yoyote!
 
Kuna baadhi ya watu tunaishi nao, tunacheka nao lakini mioyoni mwao ni wauaji wakubwa
 
Pamoja na hayo yote huyu mama nae hana akili timamu , pia nawea kusema ni jeuri. Kwanza alisha sema yeye hataki kufanya biashara ndogo ndogo, yeye ana profession yake. Inasemekana alikuwa mwalimu sijui maisha yalimchanganya vipi. Ndugu zake walishataka kumchukua akakataa, anachotaka ni kukaa mbele ya mahoteli makubwa kama Movenpick anapapeda sana coz anajua kuna wa2 wazito. Lakini kwa upande mwingine hao wanaompa hizo mimba ni kama wanyama
 
Mimi nipo concerned sana na hawa watoto tuu, wanatakiwa wasaidiwe kwani wao hawana makosa
 
Naona hapa unapaswa uwasiliane na ndugu zake wakupe full story. Hapo utapata pa kuanzia.
 
Back
Top Bottom