TUWAAMBIE CCM FINITO!Tuwaonyeshe mlango wa kutokea

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Kuwa Mwanachama au Kiongozi wa chama cha upinzani nchini ni KAZI. Lazima ukidhi vigezo vikuu vitatu:
  1. UJASIRI
  2. UVUMILIVU na
  3. UMAKINI


  • Bila ujasiri huwezi kukabiliana dhulma katika jamii
  • Bila uvumilivu huwezi kukabiliana na changamoto za kisiasa katika jamii
  • Bila umakini haraka unapoteza ujasiri

Tumeona ni jinsi gani viongozi waliokosa baadhi au sifa zote (kutoka vyama vya upinzani) nilizotaja hapo juu walivyoweza kudhoofisha upinzani nchini. Wapo Augustine Mrema (Uvumilivu na Umakini), Dr. Kaborou n.k.
t
Makamanda wa CDM wamekuwa mstari wa mbele katika kufungua darasa jipya kwa watanzania, darasa lenye hoja dhabiti za kufungua mirija ya ufahamu wa Watanzania, kuyeyusha fikra mgando na hatimaye kupata mapambazuko ya kisiasa ndani ya Taifa letu. Bila ujasiri wa Mh. Mbowe, Dr.Slaa, Zitto Kabwe, Halima Mdee na makamanda wengine waliokuwapo kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wananchi wa Tanzania tulikuwa tumefungwa kwenye wingu zito usioona nyuma wala mbele na kusahau ule wajibu tulio nao wa kufikiri kwa bidii.

Wakati wa Mwl. Julius Nyerere ulikuwa ni wakati wa kutafuta uhuru wa kujitawala (Uhuru wa bendera), na baada ya hapo demokrasia ilifinyangwa. Rejea Detention Act, Kufutwa kwa vyama vingi,n.k. mkakati uliolenga kutumikia fikra moja "Zidumu fikra za Mwenyekiti". Sasa ni wakati wa uhuru wa kifikra unaolenga kufungua mirija ya ufahamu kutatua changamoto za nyakati na hatimaye kuelekea kwenye uhuru wa kiuchumi.

Leo tuna vijana ambao ni hazina kubwa kwa Taifa, tena vijana walio na fikra pana (kuliko Wassira, fikra pana kuliko Makinda, fikra pana kuliko Augustine Mrema) kutoka CDM. Vijana walio nyuma kifikra kama Nchemba na Lusinde kutoka CCM. Wenye fikra pana kama January(wrong choice) na Nape (ila anatumiwa na mafisadi) kutoka CCM ila wamekosa jukwaa sahihi la kusimama.

Tuwaambie CCM Finito. Tuwaonyeshe Mlango wa kutokea.

Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom