Tuvute subira kwanza kuipongeza serikali

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Mramba,Yona na mafisadi wengine kweli wamepelekwa mahakamani lakini bado hawajahukumiwa. Hata hatufahamu hatima ya mali zao ambazo wamezipata kwa njia za kifisadi.Lakini wapo pia mafisadi wengine wengi ambao bado wako mtaani wanatanua huku wakitung'ong'a.Wengi tunawajua ingawa serikali hii ya ajabu inasema haiwajui ingawa ina vyombo vyote vya usalama.Sijui hata kitengo cha usalama kina kazi gani, nadhani kimepoteza maana kabisa.Kingevunjwa tu,kwa vile kinapoteza bure hela ya walalahoi.Katika hali hii tutafanya makosa kabisa kuanza kuipongeza serikali katika hatua hizi za awali kabisa.Ni vema tukasubiri mpaka wale wote wenye tuhuma wafikishwe mahakamani,wahukumiwe na kufilisiwa.Wote tunaifahamu historia ya serikali yetu.Ni ya kibabaishaji mno.Hatuna shaka kabisa kwamba shutuma dhidi yao ni za kweli kabisa.Kipato chao cha halali kisingewafanya wawe matajiri wa kutupwa kiasi hicho.Tunaisubiri serikali.
 
Wandugu,

Mimi naona huu ni kama usanii mwingine wa hii serikali kwani kwa sasa serikali nzima ya ccm inaona hakuna jipya la kufanya ili kuaminiwa kwani wamesharibu mpaka kijijini, ile kuvuta attension ya wananchi na kurusidha imani wanajaribu kufanya haya ya kutengeneza kesi tata.

At the end wote tutakuwa mashahidi hawatafika segerea kama wengi wanavyodhani na hakuna fedha zozote zitakazorudishwa zaidi ya kiini macho kinginge.

ni kweri hatuna haja ya kuipongeza serikali kwa kuwafikisha hawa mahakamani, kwani kufikishwa mahakami ni one step na kuchukuliwa hatua ni another step, mahakama zetu zenyewe ziko corrupt na zina sheria tofauti kwa walionazo na wasionazo

Nwakilisha
 
Huo ndio ukweli mtupu. Tamthilia ya nguvu ndo inachezwa na imejipatia watazamaji kilaini tu! Wajinga ndio waliwao! Tunazindi kuingizwa mkenge wallahi. Kwa nini BPM na DY waende keko kwa VX kama si usanii mkubwa wa mwaka 2008? Kwa hiyo kila mahabusu akajichukulie usafiri wake??
 
Nani kasema wameenda KEKO? Naomba ajitokeze hapa adhibitishe, hawa jamaa wamerudishwa majumbani kwao, watakuwa wanaletwa kwa siri kila siku ambayo kesi yao inatajwa. Ila wako kwenye kifungo cha ndani majumbani mwao.

Kweli serikali yetu ni ya kisanii.
 
Moods, hii iunganishwe na ile ya "Who's next at Kisutu Magistrate" ili twende sawa.
 
Mimi naona cha msingi wahusika wapatikane na hatia na vielelezo vyote viwekwe bayana. Huu utakuwa wimbo midomoni mwa watu. Badala ya kufanya kazi unabaki kushobokea ya watu. Lililompata Mramba laweza kumpata yoyote ukiwa na hatia ama kusingiziwa. Tuangalie maendeleo tufichue uozo sehemu nyingine ili wale waliokuwa wakibweteka vitini mwao wajue wanaonekana. Hakuna mtu asiyekuwa na dhambi nchi hii. Dhambi ni dhambi iwe kubwa au ndogo na mwenzako akinyolewa na wewe tia maji. Tuanze kuwajibika kila mmoja kwa upande wake.
 
Huo ndio ukweli mtupu. Tamthilia ya nguvu ndo inachezwa na imejipatia watazamaji kilaini tu! Wajinga ndio waliwao! Tunazindi kuingizwa mkenge wallahi. Kwa nini BPM na DY waende keko kwa VX kama si usanii mkubwa wa mwaka 2008? Kwa hiyo kila mahabusu akajichukulie usafiri wake??
Kweli hii ni moja ya zile tamthilia kali za ki-TZ. Kwanza ni pale mtu alipopewa muda wa kushughulikia send-off na pili ni pale wanapopelekwa "keko" kwa VX. Tuwe macho. Tukishangilia sana watajua tumeridhika, watazima moto polepole. Tusiache kupiga kelele za "haki itendeke" maana usanii sasa umepanda daraja!
 
Bw Tikerra Vyombo vya usalama katika histori ya Tanzania vimekuwa vikitetea kwanza kabisa maslahi ya watawala wa dola katika wakati husika. Kukamatwa kwa Yona na Mramba ni mkakati wa vyombo hivyo hivyo vya usalama kuilinda dola iliyopo madarakani na watawala wake. Katika wakati huu ambapo kuna mikakati ya makusudi ya kuificha Kagoda na waumbaji wake, mbinu nzuri ni ku divert attention ya wakereketwa. Hawa mafisadi wa serikali ya awamu ya tatu hatimaye wataondoka na wakubwa wao wa serikali hiyo ya awamu ya tatu. Mheshimiwa Raisi wa JMT atambue kuwa watanzania wa sasa si wa wakati ule, na hawatapumzika mpaka fisadi wa mwisho ktk awamu ya nne ameshughulikiwa, vinginevyo kitaeleweka 2010. Mungu ibariki Tanzania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom