Tuvunje jungu kwa tahadhari

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,489
86,005
Salaam Alyeikum
Tunakaribia kuanza mwezi mtukufu, mwezi wa toba na kumrudia Muumba, nikiwa kama Ndugu na jamaa wa karibu wa ndugu zangu waislamu nawatakia maandalizi mema na saumu njema kwenu.

Ombi langu kwenu kama ni lazima kuvunja jungu tukavunje kwa namna dini inavyoelekeza na sio kwa namna ilivyozoeleweka miongon mwa wengi ila hatimae saumu (swaumu) zetu zenye maana mbele za Mungu isije ikawa tumeshinda njaa bure na kujitesa bure. Ni imani yangu kuwa tutatenda mema kwa kipindi hiki na hata baada ya hapo ili kufunga kwetu kuwe na Maana.

Pia kwa nafasi zenu/zetu ningeomba tuikemee ile mihadhara yenu/yetu yenye nia ya kuanzisha na kujenga chuki na dharau dhidi ya dini za wengine kwa madai ya mwezi mtukufu lakini pia ile kuamshana asubuhi asubuhi kwenda kuswali kuwe na namna ya staha tukikkumbuka pia kuwa wenzetu nao wana namna ya kuabudu, tusijipende wenyewe.

Mwisho, nawatakia kuvunja jungu kwema na maandalizi mema ya mwezi wa Ramadhani unaoanza hivi karibuni. Waslaam (mtoto wa Mama'Mkubwa)
 
sasa hio lugha ndio siilelewi kabisa
 
Jamani tukavunje jungu kwa amani leo na kama inawezekana kutokutenda dhambi kwa siku 30 basi ongezeni ziwe nyingi zaidi ila nasikitika kitimoto itakosa wateja..........
 
Jamani tukavunje jungu kwa amani leo na kama inawezekana kutokutenda dhambi kwa siku 30 basi ongezeni ziwe nyingi zaidi ila nasikitika kitimoto itakosa wateja..........
Twende fiesta tukatende dhambi za mwisho mwisho!

Shimbonyi alyeikum!
 
Ni ujinga na ujahili kwa mtu hasa Muislamu kufuata ada ya kipumbavu ya kuvunja jungu (eti kufanya madhambi ya mwisho mwisho kabla ya kuingia mwezi Mtukufu wa Ramadhani). Ada hii haiko katika Uislamu bali majahili wasioujua Uislamu ndio ambao wamekuwa wakiinasibisha na Waislamu.Tunatakiwa kujiandaa vyema kukmaribisha mgeni (Ramadhani) kwa kiu ya ibada na kusoma Qur'ani na sio kwenda disco kwa mara ya mwisho au kunywa pombe na maasi mengine machafu eti kwa kuwa ndani ya mwezi wa RAMADHANI hakuna fursa hii. tuachane na ada hizo chafu.
 
afadhali umeliweka sawa maana juzi pale manzese kuna jamaaa wa dini hio wanahubiri watu wavunje jungu ili watulie......niliwashangaaa sana japo mimi si muisalamu lakini niliona wana uelewa mdogo haya asante, tuje na hili na mihadhara inayoendelea hadi asubuhi hatulali usiku mna kazi ya kukashifu dini za wengine, hebu tujirekebishe kwa hilo pia.
Ni ujinga na ujahili kwa mtu hasa Muislamu kufuata ada ya kipumbavu ya kuvunja jungu (eti kufanya madhambi ya mwisho mwisho kabla ya kuingia mwezi Mtukufu wa Ramadhani). Ada hii haiko katika Uislamu bali majahili wasioujua Uislamu ndio ambao wamekuwa wakiinasibisha na Waislamu.Tunatakiwa kujiandaa vyema kukmaribisha mgeni (Ramadhani) kwa kiu ya ibada na kusoma Qur'ani na sio kwenda disco kwa mara ya mwisho au kunywa pombe na maasi mengine machafu eti kwa kuwa ndani ya mwezi wa RAMADHANI hakuna fursa hii. tuachane na ada hizo chafu.
 
Wallahi ungekuwa karibu ningekunyonga ...haki ya nani vil....sasa na huyu mbuzi katoliki wangu ninaemuuza nilipie ada za watoto itakuaje sasa...mana mwezi huu naskia hakuna biashara kabisa yaani wee acha tu
Twende fiesta tukatende dhambi za mwisho mwisho!

Shimbonyi alyeikum!
 
Back
Top Bottom