Tuungane kwa pamoja tuwasaidie wahanga wa mabomu ya gongo la mboto...

onasaa

New Member
Jan 12, 2011
1
0
Najua wengi TUmeguswa na hili la mlipuko wa mabomu ya Gongolamboto, mna hasira, uchungu na majonzi mengi. Ila nafikiri kwa sasa kinachohitajika zaidi si kutafuta mchawi au kuorodhesha mapungufu na mahali pa kutupia lawama.

Bali kama Taifa tuu...ngane kwa pamoja tuwasaidie wahanga na waathirika kwa namna zote zilizo ndani ya uwezo wetu. Kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu wake kama mzalendo wa nchi hii.

Baada ya hapo ndio tuulizane vizuri, tumefikaje hapa?, tatizo liko wapi? nani katufikisha? na nini kifanyike ili haya yasitokee tena..?
 
Nafikiri suala la mabomu haya si natural disaster bali ni man made disaster the only way to make those responsible accountable is not for us to pay for their mess but to let them pay full compasation not ubani kama walivyozoea for their mess. Kulifanya suala hili kuwa la michango basi tujiandae kila siku kuchangishana, maana mahospitalini kila siku watu wanakufa kwa uzembe, barabarani kila siku watu wanakufa kwa uzembe.

Si pingi kwa mtu aliyeguswa binafsi kuchangia alicho nacho ninapinga kwa watu kuanza kampeni za kisiasa na kuchangisha pesa kwa ajili ya waathirika wa mabomu haya wakati wale wa mbagala hatujapewa ripoti kamili walivyolipwa na kusaidiwa na michango yetu. Mtu yeyote atakayeanza kuleta kampeni za tuwachangie tusitafute mchawi basi yeye ndiyo mchawi mwenyewe.
 
Taito yako ni nzuri, lakini natamani sasa tungejadiri namna gani yasitokee kawe, kigamboni, mabibo, lugalo etc. Mimi napendekeza kumuondoa amiri jeshi mkuu na maofisa wake wote aliowateua,
 
Back
Top Bottom