Tutoe Elimu ya Sekondari Bure kwa Njia Hii

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
409
31
Kutokana na hali halisi inayolikabili taifa katika sekta ya elimu hasa kwa ngazi ya msingi na sekondari, pamoja na mapendekezo ya kuboresha maslahi ya walimu, mazingira ya kujifunzia na vitendea kazi, naomba tuanzishe utaratibu wa kutoa elimu ya sekondari bure kwa wanafunzi watakaoweza kupata sifa zifuatazo na ambao watajiunga na shule za Serikali.

1. Mwanafunzi ambaye katika mtihani wa mwisho wa shule ya msingi atafaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na pia awe amefaulu somo la Hisabati kwa angalau kiwango cha alama ya B.

2. Wanafunzi wote ambao watafaulu kwa kupata Division One au Two kwa mitihani ya kidato cha nne na Hisabati wawe wamefaulu kwa kiwango cha angalau C na wasiwe na F katika somo lolote lile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom