Tutibu kiini cha tatizo sekta ya nishati ya umeme!

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
Kwa nafasi ya Uwaziri Kivuli wa Nishati na Madini, nafahamu kuna ufisadi na ubadhilifu ndani ya TANESCO ambao uchunguzi ni muhimu kwa ajili ya uwajibikaji. Kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa TANESCO na maafisa wengine wa shirika hilo kupisha uchunguzi ni muhimu, lakini si muarubaini wa uozo wa kimfumo katika sekta ya nishati nchini nitatoa vielelezo vya kina wakati nitakapo wasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni katika wizara ya Nishati na Madini.
Hata hivyo ni vyema nikatahadharisha mapema kuwa tukio hili linapaswa kutafakariwa kwa upana kwa kuwa linahusisha masuala mengi ambayo mengine Bodi ya Wakurugenzi imeyaacha nyuma ya pazia. Ukweli wote utakapotoka hadharani wengine zaidi watapaswa kuwajibika au kuwajibishwa kwa maslahi ya Taifa!
Kwa nyakati mbalimbali toka mpango wa dharura wa umeme uwasilishwe bungeni, nimekuwa nikiitahadhalisha na kuihoji serikali (kama sehemu ya jukumu langu la kibunge) kwa uzembe, ufisadi na udhaifu wa kiutendaji katika serikali ambao hasara yake utairejesha nchi katika mgao wa umeme hali ambayo imedhihirika hivi sasa!

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: TUTIBU KIINI CHA TATIZO SEKTA YA NISHATI YA UMEME!
 
Back
Top Bottom