Tutawapiga Virungu mkigoma..

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Kwa wale walioko nje na hawakubahatika kuiona hii basi ipitieni hii hotuba.

Mtasikia jinsi watu walivyoambiwa (TUCTA) kuwa watakula virungu vya FFU.....

Mkwara ulisaidia kwani TUCTA waliogopa virungu na Plaster........

Huu Mkwara kwa kweli ulikuwa Mzito. Mbayuwayu wakarudi kujipanga upya.



 
Last edited by a moderator:
Nadhani ulimi wa Mhe. Rais umeteleza. Hangeweza kututishia eti tutapigwa virungu endapo tutagoma. Kugoma ni haki ya mfanyakazi endapo haridhiki na ujira wake. Tena anaonekana alisahau kwamba huu ni mwaka wa Uchaguzi!!

Kama washauri wa Rais watamridhisha aombe radhi kwa wafanyakazi, basi wapiga kura wamjibu kwamba Rais anayehamaki na kusema ovyo hafai kupewa kura zetu arudi madarakani. Alihamaki hata pale aliposema eti hahitaji kura 350,000 za wanaTUCTA. WaCCM wamesikika wakikanusha kwamba Mhe. Kikwete hakusema hivyo! Walio-record speech yake siku ile waituchezee tena.

Kwa ujumla huyu Mhe. hastahili kupewa ngwee ya pili. Tunaye Dk. SLAA ambaye ameonyesha umahiri na umakini ktk kuchambua na kushughulikia matatizo ya umma.
 
Kuna watu wengi tu wanaona hilo siyo kitu kikubwa sana kumyima kura.

Alipopita mikoani na kusema kaongeza tayari mishahara, wengi walifurahi. Ila inashangaza kuwa pesa hizo zilikuwa hazijaidhinishwa na Bunge na walipombana akasema "nitaendela kumwaga hela na ahadi".

Walipompeleka kwa Tendwa, ikaonekana lazima achague mawili:

1. Awe mwanaume wa kweli na akiri kuwa aliongeza mishahara kinyemela na hivyo AZUILIWE KUGOMBEA.

2. Atangaze hajaongeza mishahara na wananchi wamuone ni Muongo.

Kama wanasiasa walivyo, alichagua hili la pili na bado anaendelea kuahidi Viwanja vya ndege, Meli na kujenga Dubai na Carlifonia hapa Tanzania,
 
Kwa wale walioko nje na hawakubahatika kuiona hii basi ipitieni hii hotuba.

Mtasikia jinsi watu walivyoambiwa (TUCTA) kuwa watakula virungu vya FFU.....

Mkwara ulisaidia kwani TUCTA waliogopa virungu na Plaster........

Huu Mkwara kwa kweli ulikuwa Mzito. Mbayuwayu wakarudi kujipanga upya.





Jamani mie ni mzee hapa Dar naomba mnisaidie nielewe manake labda uwa natatizwa nikisikia Rais wangu anazungumza na wazee wa Dar esalaam, na uwa na hamu sana kwenda huko but sijui hao wazee criteria gani ipo kuchaguliwa kuhudhuria na ni wazee wa vyama vyote au na kama wengine sisi tusio na chama au wanachaguliwa waje au ni wa chama kimoja, manake mie nami ni mzee ningependa kujua kama ni kuapply or any proceess to follow , angalau na mimi mzee wa Dar es salaam nipate nafasi ya kumsikiliza Rais wangu ikitokea fursa nyingine!!! Naomba nieleweshwe tafadhali!!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna rais hapa ,hivi ajui hizi hotuba zinaifadhiwa pumba zote hizi zitamdhuru baadae.
FFU ni kwa ajili ya mgomo ama vurugu .kwa nini anaunganisha mgomo(strike/demostration) na vurugu?
Kwa nini anaongelea kuua?
Na nimeona wengi aliokuwa wanashangilia ni wale vijana kama wa kupiga matarumbeta .

Mkwere hizi spin za hali ya chini.
 
Mheshimiwa,
Hujamalizia hotuba nzima ya mgombea wa CCM hasa ile ambayo anazisusa kura za wafanyakazi. Kwa kuwa muda muhimu wa kura unakaribia, fanya ima fa ima uwakumbushe wafanyakazi wajue la kufanya. Tafadhali!


Kwa wale walioko nje na hawakubahatika kuiona hii basi ipitieni hii hotuba.

Mtasikia jinsi watu walivyoambiwa (TUCTA) kuwa watakula virungu vya FFU.....

Mkwara ulisaidia kwani TUCTA waliogopa virungu na Plaster........

Huu Mkwara kwa kweli ulikuwa Mzito. Mbayuwayu wakarudi kujipanga upya.



 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha. Njemba imewakumbusha jinsi Nyerere alivyopiga watu virungu kule Kilombero na huyo mwana heri kutetea virungu na hata watu kuuliwa kule Kiombero. Sasa JK kupiga mkwara wa virungu inakuwa nongwa ila Nyerere kutenda na kuamuru hivyo virungu ni vitu vya kukalia kimya. :smile-big: :smile-big: :smile-big:

Wenzenu tushapigwa sana virungu na mabomu ya machozi kwa amri ya Mrema na Mkapa. Sasa zamu yenu nyie mnaojifanya mna uchungu sana na nchi hii kula virungu na mabomu ya machozi baada ya uchaguzi kama mkifanya kosa la kuandamana na sijui kuingia mitaani. :becky: :becky: :becky:
 
Back
Top Bottom