Tutasaidiwa vyandarua hadi lini?

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
lC.gif
John Bwire​
rC.jpg

JUMATANO ya wiki iliyopita viongozi 20 wa bara la Afrika walikutana mjini New York, Marekani na kuunda umoja mpya wa kupambana na malaria unaoitwa African Leaders Malaria Alliance (ALMA).
Ilielezwa wakati wa uzinduzi wa mshikamano huo mpya kwamba tayari dola bilioni 3 zimeshapatikana kwa ajili ya mapambano hayo, na kwamba vyandarua maalumu vyenye dawa ya kujikinga na mbu vipatavyo milioni 240 vitakuwa vimesambazwa Afrika ifikapo mwishoni mwa mwaka kesho.
Ni jambo jema kwamba viongozi wetu wa Afrika wameamua kuanzisha mshikamano huo mpya kupambana na malaria – ugonjwa ambao katika Afrika huchangia robo tatu ya vifo vyote vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Ni matarajio yetu, hata hivyo, kwamba umoja huo utabuni na kutekeleza mikakati yake wenyewe ya kupambana na malaria badala ya kuishia kupokea, kila mwaka, vyandarua vya misaada kutoka kwa wahisani.
Tunasema hivyo, kwa sababu tatizo la malaria katika Afrika halitatokomezwa kwa misaada ya vyandarua kutoka nchi tajiri; bali litamalizwa kwa kutokomeza mazingira ya mazalio ya mbu. Na hilo linahitaji mkakati wa pamoja wa nchi zote za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Isitoshe, vyandarua ni kama nguo tu ambazo baada ya miaka miwili au mitatu zinachakaa na kuhitaji kubadilishwa. Kama hivyo ndivyo; je, tutasaidiwa vyandarua na wahisani hadi lini?
Ingekuwa ni vyema kama ALMA italenga katika kutafuta misaada ya wahisani ya kujengewa viwanda vya kutengeneza vyandarua hivyo katika nchi kadhaa za Afrika badala ya kusubiri, kila mwaka, kugawiwa vyandarua hivyo na nchi hizo.
Ni matumaini yetu kwamba ALMA italenga katika kufanikisha jambo hilo; ili ituondolee aibu hii ya bara la Afrika ya kusaidiwa na wahisani wa nje hata vyandarua!


SOURCE: Raia Mwema
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom