Tutarajie IGP Mwema mara moja kutangaza amri hii

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wakuu, tutarajie muda wowote kuanzia sasa yule kada Namba 1 wa CCM katika jeshi la polisi kuutangazia umma kwamba kuanzia sasa itakuwa ni kosa la jinai kwa watu wowote, wanaokwenda mahakamani kwa ajili ya kesi zao wanazoshitakiwa, au kwenda kusikiliza kesi nyingine yoyote, iwapo watu hao wataondoka hapo mahakamani kwa miguu.


Baada ya kesi ni lazima watu wote waondoke mahakamani kwa kutumia usafiri wa magari.
 
Nchi za Kiafrika bana! Yaani watawala wakianza kupoteza sifa za kukubalika na umma basi huwa tayari hata kunzisha vijisababu vya kuleta vurugu. Huwa wanaona potelea mbali, kuliko aibu, bora nchi iingie vitani.

Nauliza: Hivi maelfu ya Wa-Ivory Coast walikoufa hivi karibuni ilikuwa ni lazima, au ujeuri tu wa waliokuwa madarakani?
 
Nchi za Kiafrika bana! Yaani watawala wakianza kupoteza sifa za kukubalika na umma basi huwa tayari hata kunzisha vijisababu vya kuleta vurugu. Huwa wanaona potelea mbali, kuliko aibu, bora nchi iingie vitani.

Nauliza: Hivi maelfu ya Wa-Ivory Coast walikoufa hivi karibuni ilikuwa ni lazima, au ujeuri tu wa waliokuwa madarakani?


Na kinachonigaragaza chini mie ni kuwaona watawala majukwaani wakiimba amani, utafikiri amani huja tu kwa kuimbwa. Amani huja kwa kutokana misingi madhubuti ya haki ambayo ndiyo msingi mkuu wa utawala bora.
 
Nchi za Kiafrika bana! Yaani watawala wakianza kupoteza sifa za kukubalika na umma basi huwa tayari hata kunzisha vijisababu vya kuleta vurugu. Huwa wanaona potelea mbali, kuliko aibu, bora nchi iingie vitani.

Nauliza: Hivi maelfu ya Wa-Ivory Coast walikoufa hivi karibuni ilikuwa ni lazima, au ujeuri tu wa waliokuwa madarakani?

Vijisababu vya KI INTELIJENSIA!
 
Ingekuwa ni mimi nisingekubali kuidhalilisha taaluma yangu eti tu ili kutiii mamlaka ya akina fulani...
 
Nakubaliana na yule aliyetoa thread moja humu ndani ikisema kuwa ni bora Lema akashindwa hiyo kesi ya uchaguzi dhidi yake ili uchaguzi mdogo ufanyike na tuone magamba kama watachukuwa kiti hicho. Juzi nilipopita Arusha na kukaa siku 4 nikitokea Nairobi niliona kama vile CCM haipo pale.

Halafu utaona uchaguzi mdogo ukifanyika -- Igunga CCM walitumia bil 3 katika kampeni, Arusha watatumia mara 10m ya hapo! Hela za wananchi bila shaka -- kwani waonyeshe mashamba au viwanda wanavyovimiliki.
 
Viongozi wetu wanasahau kuwa ni sehemu ya jamii!! Wanasahau kuwa siku wakifa jamii hiyo hiyo italazimika kusimamisha shughuli na kuwazika. Wanasahau pia kuwa uongozi ni dhamana na wala siyo umajigambo na kujiona wewe ndo kila kitu hakuna akutishaye. Pamoja na kelele zote, wataendelea kujisahau kwa makusudi au kujaribu jaribu kuona jamii inasemaje.
 
Kwa dhati kabisa napenda kumshauri mbunge Lema kuwa busara itumike na kuwaasa wafuasi wake waache kwenda mahakamani kwa wingi nia njema tu ili muda huo wautumie kuzalisha. Maana hakuna wanachokifanya wakiwa hapo mahakamani. Lema nae ajikite sasa kutekeleza yale aliyowaahidi wananchi kipindi cha uchaguzi badala ya kukimbizana na mapolisi kila kukicha. Lema ajitahidi kukwepa sana malumbano na polisi. Muda unazidi kwenda kasi na hautamsubiri. Tunahitaji uboreshaji wa maendeleo ya mji wa Arusha kama alivyotuahidi wakati wa kampeni. Muda wa kutathmini utendaji wake hautazingatia muda alioutumia kupambana na polisi. Nawaomba waliokaribu nae wamshauri. Kipindi cha "honeymoon" kimeisha sasa ni kazi inayoonekana. Lema, tambua mbinu za wapinzani wako(CCm). CCM wamepanga kukupotezea muda kwa kukupambanisha na polisi ili ushindwe kufanya yale yampasayo mbunge makini kufanya kwa kuwaletea wananchi maendeleo. Kazi ni kwako.
 
Ukiona hivyo ujue sasa hawana hoja ya msingi katika kumzuia Lema hivyo kutafuta jambo lolote lile ili mradi wamkatishe tamaa.
 
Magamba mengi tu ccm na hayabanduki ng'ompaka ccm na ccm-b wangoke madarakani
 
nakubaliana na yule aliyetoa thread moja humu ndani ikisema kuwa ni bora lema akashindwa hiyo kesi ya uchaguzi dhidi yake ili uchaguzi mdogo ufanyike na tuone magamba kama watachukuwa kiti hicho. Juzi nilipopita arusha na kukaa siku 4 nikitokea nairobi niliona kama vile ccm haipo pale.

Halafu utaona uchaguzi mdogo ukifanyika -- igunga ccm walitumia bil 3 katika kampeni, arusha watatumia mara 10m ya hapo! Hela za wananchi bila shaka -- kwani waonyeshe mashamba au viwanda wanavyovimiliki.

utulivu wetu ndio unaotugharimu
 
Back
Top Bottom